Ndege Mpya ya Mizigo ya ATCL Kuanza Kazi Wiki Ijayo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767-300F iliyonunuliwa na serikali itaanza kazi ya kusafirisha mizigo nje ya nchi Juni 26, mwaka huu.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Sarah Reuben
Reuben alisema kuanzia Jumatatu ijayo, ndege hiyo itaanza kusafirisha mizigo kwenda kwenye miji ya Mumbai nchini India, Kinshasa na Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na nchini Dubai.
"Tunayo furaha kutangaza huduma zetu za kusafirisha mizigo kwenda Dubai, Mumbai, Kinshasa na Lubumbashi ambazo zitaanza Juni 26, mwaka huu," alisema.

Kutokana na kuanza kwa safari hizo, alitoa wito kwa wafanyabiashara kufikia viwango vipya katika biashara zao
kimataifa kwa kutumia ndege hiyo ya mizigo ya ATCL.

Siku chache kabla yaKuwasili kwa ndege hiyo nchini, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema ndege hiyo ina uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na kuruka kwa saa 10. Pia alisema ni ndege nzuri na ya kisasa, inatumia mafuta kidogo, ina kiwango kidogo cha kelele na inaweza kuingia kwenye viwanja vikubwa duniani.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, ndege hiyo pia itakuwa inatoa huduma kwa kukodiwa na wafanyabiashara kulingana na uhitaji utakaojitokeza, hivyo Watanzania watakuwa wanaitumia lakini akitokea mfanyabiashara yeyote ana mzigo wake wako tayari kumkodisha ndege hiyo.

Hivi karibuni wafanyabiashara waliozungumza na gazeti la HabariLEO walisema kuwa ndege hiyo itasaidia bidhaa zao kupenya kwa urahisi kwenye masoko ya Ulaya, Asia na Amerika. Hii ni ndege ya kwanza ya mizigo kununuliwa nchini na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.​
 
Asante kwa taarifa, imenunuliwa ifanye kazi hiyo na sasa itaanza kufanya kazi yake...
 
Kazi nzuri.

Wakitaka kufanikiwa waache longolongo, uswahili na incompetence.

Route ya Lubumbashi na Kinshasa imekaa poa, hiyo miji ina fursa sana kwa wachakalikaji.
 
Fursa zimeanza halafu mshindwe kusafirisha na nyie kisa ooh mitaji

Halafu kwa usahihisho tu Dubai sio nchi
 
Back
Top Bottom