Kampuni ya Boeing imekabidhi ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F, Magufuli atajwa

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing ya nchini Marekani imekabidhi ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F kwa Wakala wa Ndege za Serikali Tanzania (TGFA) tayari kwa safari ya ndege hiyo kutoka Marekani na kuja hapa nchini Tanzania.

Makabidhiano hayo yamefanywa katika kiwanda Boeing kilichopo Jiji Seattle nchini Marekani kwa Wawakilishi wa Serikali ya Tanzania ambao ni Balozi wa Tanzania Washington, Marekani Mhe. Elsie Sia Kanza, Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TGFA Capt. William Budodi.

Ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 767-300F ndio ndege ya kwanza kununuliwa hapa Barani Afrika, na ni ndege iliyojibebea sifa lukuki katika usafirishaji wa mizigo kwa kutumia anga Duniani.

Boeing 767 -300F ina uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na kuruka kwa masaa 10 ambapo ndege hiyo inatarajiwa kuwasili nchini mnao tarehe tatu Juni huku mapokezi ya ndege hiyo yanatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Ndege hiyo imenunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya matumizi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
 
Hatua nzuri ila umenistua hapo uliposema ndege yetu 767 ndio inakuwa freighter ya kwanza hapa Africa !!! Inaoneka a bado hatujajifunza kitu kuhusiana na kununua ndege ambazo ni mpya angani, kuna taarifa za kusimama kwa muda usio julikana kwa A220 zetu , kutokana na hitilafu ya engine , pratt and whitney bado hana taatifa sahihi ni lini atatatua tatizo hilo.
 
Hatua nzuri ila umenistua hapo uliposema ndege yetu 767 ndio inakuwa freighter ya kwanza hapa Africa !!! Inaoneka a bado hatujajifunza kitu kubusiana na kununua ndege ambazo ni mpya angani, kuna taarifa za kuzimama kwa muda usio julikana kwa A220 zetu , kutokana na hitilafu ya engine , pratt and whitney bado hana taatifa sahihi ni lini atatatua tatizo hilo.
Utalipwa fidia
 
Back
Top Bottom