Jamani, mie nashangaa sana. Hizi Boeing za zamani kama hii 737-500 zinajulikana kuwa fuel guzzlers. Hata hii ya sasa, Boeing 737-800 inasemekana bado ina rate kubwa ya utumiaji mafuta ukilinganisha na equivalent Airbus kwa mfano. Sasa leo hii kwa bei za mpao za mafuta bado tunaingia mkataba wa kukodisha ndege ambayo inajulikana kuwa sio economical kwenye kutumia mafuta? Je, tumesahau kwamba kwa sasa hivi the biggest concern kwa airlines ni gharama za mafuta? Yaani mie nachoka kabisa.
Nahisi kwa kuwa tatizo letu kubwa limekuwa mikataba, safari hii tumepeleka team ya wanasheria sharp kukodi ndege, tukasahau kwamba mkataba mzuri sio kwa kuwa tu una vipengele vizuri vya sheria, bali suala la aina ya technology ya ndege ni muhimu pia.
Kwanza hizi Boeing 737-series zina tatizo kubwa la fusilage fatigue. Sijui kama wamefikiria hili.