TabletFellow
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 918
- 274
kwahiyo ni nege mpya used
Do they ever?
ukisoma akikisha una kitambaa cha kufutia machozi
Mwaka 1978, Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimfukuza kazi aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na uchukuzi, Augustine Mwingira na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege (ATC), Laurance Mmasi, katika tukio ambalo linaweza kufananishwa na tukio lililoibuliwa na ripoti ya CAG kuhusu ufisadi katika Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Katika tukio hilo la Mwalimu Nyerere, Shirika la Air Tanzania (ATC) lilikodi ndege kutoka kwa raia wa Lebanon, George Hallack, ndege ambayo ilikuwa mbovu, ikiwa ‘imeruka' kwa saa ambazo ni pungufu ya zile zilizohitajika kwa mujibu wa utaalamu wa ripoti za watalaamu.
Ilibainika kuwapo kwa njama katika mkataba huo ambao ndege iliyokodiwa iliishia kuegeshwa katika uwanja wa ndege na ‘kuoza.' Ni kutokana na hali hiyo, Mwalimu akawafuta kazi Waziri na Mkurugenzi wa ATC.
Tukio hilo linafanana na hili la sasa. Katika tukio la sasa, menejimenti ya Shirika la Ndege (ATCL) imekodi ndege aina ya Airbus, namba A320214 kutoka Shirika la Wales Trading la Lebanon, Oktoba, mwaka 2007, nchini Lebanon ambayo ripoti za watalaamu zilibainisha kuwa ni ndege mbovu lakini shirika lilikodi bila kuzingatia maslahi ya taifa.
Akizungumzia tukio hilo, Mbunge Amina Mohamed Mwidau ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), anasema: "...kwa kweli katika mashirika ambayo tumeyapitia (kuyakagua) shirika ambalo lilinifanya nikaumwa kichwa na kusikia kizunguzungu na nikalala na homa ni ATCL."
Mwidau ambaye alizungumza maneno hayo bungeni na mbunge mwenzake kuingilia kwa kuropoka "kwa nini asianguke kutokanana na kizunguzungu hicho, alisema menejimenti ya ATCL ilionyesha kiburi kikubwa kwa kuingia mkataba na Wales Trading bila ridhaa wala dhamana ya Serikali.
"Waliingia mkataba kwa miezi takriban saba bila ya dhamana ya Serikali. Mbali ya hilo, lakini pia ilinisikitisha sana kwa sababu kulikuwa na timu ya wataalamu ambayo ilitoa taarifa kuwa si jambo la busara kukodi ndege ile kwa sababu baada ya miezi takriban sita itaenda tena matengenezo makubwa kwa kitaalamu ni 12 years checks ambayo najua Waziri Nundu pale anafahamu.
"Ni matengenezo makubwa ambayo ndege hiyo inatakiwa ibadilishwe vitu vingi, lakini wao walidharau, walidharau ushauri wa wataalamu wale ambao wako kwa ajili ya kushauri shirika na wanalipwa, wakaweza kusaini mkataba ule ambao ni wa miaka sita, ni takribani ni miezi 72.
"Lakini pia kilichonisikitisha zaidi ni pale walipokubaliana katika mkataba ule, rate ya kukodisha ndege ile itakuwa ni dola 374,000 kwa mwezi, kama imeruka au haijaruka na ndege ile ilikaa miezi takribani 48 katika mikono ya ATCL. Katika miezi hiyo 48 ni miezi saba tu ambapo ndege ile iliweza kuruka lakini miezi 41 ilikuwa chini.
"Kwa ujumla mpaka kufikia tarehe 30 Januari, 2010 Shirika la Wales Trading lilileta hesabu yake kwa ATCL inaonyesha kuwa deni lile lilikuwa limesimama kwenye takriban pesa za Kitanzania bilioni 323 ambayo ni sawa sawa na dola milioni 200...pesa inayoweza kununua ndege mbili ambazo ni aina hiyo hiyo ya Airbus 320 ambayo ukiangalia kwenye website ya Airbus utakuta bei ya ndege moja mpya (a brand new aircraft) ya aina hiyo imesimama kwenye dola milioni 88.3.
"Kwa hiyo, tungeweza kupata ndege mbili mpya na chenji ikabakia, lakini manejementi hii imeonyesha dharau kwa sababu timu ya wataalamu ime-prove ni kweli ndege ile imeruka miezi saba na ikaenda matengenezo. Imenisikitisha sana kwa sababu watendaji wale walionyesha dharau na inaonyesha kuwa hawapo peke yao lazima wana mashiko sehemu wanayoyategemea na ndiyo maana wakafanya kiburi kile cha hali ya juu."
Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ni kama vile ndiye ‘nyota' wa mkutano uliopita wa Bunge na hasa baada ya kuwataka wabunge kutia saini zao kwa lengo la kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ripoti za CAG kuonyesha ufisadi unaojirudia kila mwaka miongoni mwa taasisi za umma.
Zitto ambaye ameshikilia rekodi yake ya kuwa kinara wa mkutano miwili mfululizo ya Bunge, akiibuka na pingamizi la posho kwa wabunge katika mkutano Februari, mwaka huu na sasa, akiibuka na ajenda ya ‘kumng'oa' Waziri Mkuu, hoja zote zikipata ushabiki ndani na nje ya Bunge, amelifanya Bunge kuwa na rekodi ya kipekee lakini pia, hatua yake ya kutaka Waziri Mkuu ang'olewe inampa nguvu zaidi CAG tofauti na wengi wanavyotafsiri.
Zitto mwenyewe amelieleza gazeti hili akisema: "Vyovyote itakavyokuwa, kufanikiwa au kutofanikiwa kumng'oa Waziri Mkuu, ripoti za CAG zitaheshimiwa kwa kufanyiwa kazi ili makosa ya ufisadi yasiwe yanajirudia na yakijirudia basi, siku nyingine Waziri Mkuu atang'oka, rekodi zimeshajiandika."
Hivi..........Ndege Mpya maana yake nini nini hasa??!!
naona kitufe cha 'like' kinarespond kuwa kuna makosa.....Can I have a Tissue, Please?......:A S-cry::A S-cry:
Kweli mapendekezo ya bunge hayafuatwi ilisemwa kampuni ifilisiwe na kampuni mpya ianzishwe now waturudishs kwenye deni lingine la lebanon.Ndege mpya ya ATCL kutua Dar leo mchana
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limepata ndege nyingine aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili leo hii Mchana (Alhamisi) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo jana ilieleza.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikoperekwa kwa ajili ya uchunguzi huo.Wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu leo hii mchana.Ndege hiyo imeshawekwa chata ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunetegemea itaanza kufanya safari mara moja, Taarifa hiyo ilisema.Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida (economy class).Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Bw. Paul Chizi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita alitoa maelezo kwa uchache juu ya ujio wa ndege hiyo lakini hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na ndege hiyo.Chizi alisema kuwa mipango ya ujio wa ndege hiyo ilikuwa ni mipango ya muda mfupi iliyowekwa ili kuboresha huduma za ndege alisisitiza kuwa kampuni tayari ina mpango wa muda mrefu ambao utafanyiwa kazi kikamilifu.ATCL hivikaribuni imezindua tovuti ikiwa katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuongeza ubora wa ndege hiyo ya kitaifa.Tovuti hiyo itawawezesha wateja kupata taarifa ya safari za ndege bila ya kufika katika ofisi za kampuni hiyo au mawakala na kuwawezesha wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijami
kila binadamu aombalo kwa nia ya kweli na haki kutoka moyoni mwake hakika Mwenyezi Mungu hataacha lipite! Tegemea majibu mkuuMwaka 2015 Raisi atakayechukua Nchi atakuta madeni kila kona.
hadi IKULU ajiandae kujenga yake kwani itakuwa imefidia Deni kama ilivyo Bandari ya Mtwara.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WALAAAANI MAFISADI NA VIONGOZI WA SERIKALI.
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
ukisoma akikisha una kitambaa cha kufutia machozi
Mwaka 1978, Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimfukuza kazi aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na uchukuzi, Augustine Mwingira na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege (ATC), Laurance Mmasi, katika tukio ambalo linaweza kufananishwa na tukio lililoibuliwa na ripoti ya CAG kuhusu ufisadi katika Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Katika tukio hilo la Mwalimu Nyerere, Shirika la Air Tanzania (ATC) lilikodi ndege kutoka kwa raia wa Lebanon, George Hallack, ndege ambayo ilikuwa mbovu, ikiwa imeruka kwa saa ambazo ni pungufu ya zile zilizohitajika kwa mujibu wa utaalamu wa ripoti za watalaamu.
Ilibainika kuwapo kwa njama katika mkataba huo ambao ndege iliyokodiwa iliishia kuegeshwa katika uwanja wa ndege na kuoza. Ni kutokana na hali hiyo, Mwalimu akawafuta kazi Waziri na Mkurugenzi wa ATC.
Hiyo ndio hofu yangu! Btw, umeona jina la huyo meneja? Jina lake tu linanikatisha tamaa, Chizi?!!!!" Kuna shirika tena hapo?
Ndege mpya ya ATCL kutua Dar leo mchana
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limepata ndege nyingine aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili leo hii Mchana (Alhamisi) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo jana ilieleza.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikoperekwa kwa ajili ya uchunguzi huo."Wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu leo hii mchana."Ndege hiyo imeshawekwa chata ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunetegemea itaanza kufanya safari mara moja," Taarifa hiyo ilisema.Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida (economy class).Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Bw. Paul Chizi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita alitoa maelezo kwa uchache juu ya ujio wa ndege hiyo lakini hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na ndege hiyo.Chizi alisema kuwa mipango ya ujio wa ndege hiyo ilikuwa ni mipango ya muda mfupi iliyowekwa ili kuboresha huduma za ndege alisisitiza kuwa kampuni tayari ina mpango wa muda mrefu ambao utafanyiwa kazi kikamilifu.ATCL hivikaribuni imezindua tovuti ikiwa katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuongeza ubora wa ndege hiyo ya kitaifa.Tovuti hiyo itawawezesha wateja kupata taarifa ya safari za ndege bila ya kufika katika ofisi za kampuni hiyo au mawakala na kuwawezesha wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijami
Ngoja Precision wasikie WATAIANGUSHA SASA HIVI ! hao jamaa Noma sana ! hao ndio wanahusika na ndege kuanguka anguka ili kuua mashirika hayo! ATC kaza buti hakika mkijipanga vizuri mtaweza, Kila la KHERI , na safari zote za serikali na mashirika ua umma inabidi mpewe nyie ili kuiinua shirika ! hapo ndio soo la precision linapoanza