Ndege Mpya ya ATCL katika picha

Ndege Mpya ya ATCL katika picha

Huyu wa zamani ata twiga wake alikuwa ametulia anakula majani yake vizuri tuu hana shida na mtu, ila huyu wa sasa ,ni kiboko.
 
engine zipoe,imetoka mbali sana
We jamaa umewaka. Mtaalamu barafu kasema inaitwa 'Water Canon Salutation'. Kuikaribisha ndege mpya. Kama hujui kaaga kimya man.

Engine zipoe mbona hawafanyii hivyo ndege zote? Pamoja na hayo, asante kwa nia yako njema kunijibu.
 
Kwanini sasa serikali isingenipa mtu mwenye pesa kama mimi? Kwa hiyo ataukishikiwa bastola hapo utakiri kwamba Udart haina mapungufu?
Udart ina mapungufu mengi tu, ila point yangu ni udart sio aerikali, inajua hilo??
 
Kuanzia Leo tutakutana sana na wataalamu wa ndege wa kitanzania, kuna mtu hapa ananielezea saluti ya kumwagiwa maji kama ana phd ya maswala ya ndege wakati ht ndege hajawahi kupanda
 
Tununapooza zile tuktuk
Mkuu msome barafu akishadadia ujio wa hii ndege mpya kwenye uzi tofauti anasema ile inaitwa Water Canon Salutation. Nafikiri ni mapokezi maalumu ya ndege mpya.

Hiyo gharama yote ukijumlisha unaona kabisa walionunua ndege wamepoteza mwelekeo tayari. Wameacha ya msingi wanatafuta ufahari eti na sisi tuna ndege.
 
So you mean kama nchi hatuwezi kusimamia BOEING! Hahaaa!
Tunaweza. Ona kuna size kama hiyo boeing ya fastjet. Japo wanapunguza idadi ila zipo na zinatinga.

Lakini serikali walionunua hiyo ndogo chanjo tu hospitali wanashindwa kusimamia ndo itakua ndege?
 
Mkuu msome barafu akishadadia ujio wa hii ndege mpya kwenye uzi tofauti anasema ile inaitwa Water Canon Salutation. Nafikiri ni mapokezi maalumu ya ndege mpya.

Hiyo gharama yote ukijumlisha unaona kabisa walionunua ndege wamepoteza mwelekeo tayari. Wameacha ya msingi wanatafuta ufahari eti na sisi tuna ndege.
JPM walks the talk, aliahidi elimu bure, wanafunzi kukaa ktk madawati, ndege mpya, etc, sio wale wa kuongea tu na wasio na msimamo wa wanachokiongea!
 
Ya zamani
Cszw0EaXEAA-UQ8.jpg

Ya sasa
Cszw0EZWYAEvf9O.jpg

Mnaoponda ndege mpya, Mungu anawaona...
Hahaha,eti Mungu anawaona!hiyo inatofauti gani na shabiby bus?si bora wangenunua mabasi ya serikali!!!
 
Mmeshaambiwa mara nyingi kwamba ndege kubwa zina gharamankubwa sana kuziendesha na hazitui viwanja vidogo. Hao wenye hizo kubwa wenyewe (fastjet) wameshatangaza kuzirudisha na kuchukua ndogo....Aaagr...mnakera na nyie
Wakitoka ndogo watafunga kabisa shirika.

Unadhani watanzania wangapi wanamudu ndege kwa pesa zao? Wengi wanasafiria ndege kwa hisani ya serikali au makampuni yao.

Pa kuwekeza kwa sasa ni elimu elimu elimu (madawati, maslahi ya waalimu wajuzi, vitabu, maabara, vifaa, n.k), afya (madawa, chanjo, maslahi ya madaktari na wahudumu wajuzi), miundombinu ya reli kwa ajili ya mizigo na hifadhi ya jamii (nyumba bora kwenye mazingira bora, bima zilizo makini za afya, maslahi na malezi kwa wastaafu na wazee, n.k.)

Ndege acha sekta binafsi ipambane na serikali iwe refa. Wakishindwa ni hasara yao. Kwa hutu tudege ni hasara ya kodi yetu na/au huduma mbadala ambayo ingeweza kunufaisha wote.
 
Hivi vibarkowa Air TZ ni zaidi ya demokrasia Unguja na Pemba. Disabuse your minds colonial masters.
 
Ndoto za alinacha.

Halitakaa lirudi kwa kutumia serikali kuliendesha. Waachie tu sekta binafsi ipambane serikali wawe marefa.
..Mbona walioondoka wameshindwa kuonesha juhudi kama hizi? au ulikuwa ukifurahi kusikia nchi kubwa kama hii shirika lina ndege moja na wafanyakazi 200! Hebu kwenye ukweli tuseme kweli na sio kila kitu kukandamiza tu!
 
Back
Top Bottom