Hawa unaruhusiwa kufuga iwapo una kibali..Kama unataka kuwafuga fuata taratibu zote za kisheria then ione wizara ya mali asili na utalii wao watakuambia nn cha kufanya
Yan kwa Maelezo mafupi tu ya huyu ndege inatosha kuamini kweli Mungu yupo na si wa kawaida japo wapo watu na eti "wamesoma" wanakwambia Mungu hayupo na kama yupo wanakwambia thibitisha...Hv hz elimu tunazosoma ni kwa ajili ya ajira au kuelimika?
Hapana nimemaanisha yai moja la mbuni lina mayai 24 ya kanga. Yaani ukubwa wa yai la mbuni inabidi uunganishe mayai 24 ya kanga ndo yafikie ukubwa wa yai la mbuni
Mbuni yupo katika order inayofahamika kama STRUTHIONIFORMES na family yake ni STRUTHIONIDAE na jina lake la kisayansi (scientific name ) ni STRUTHIO CAMELUS. Mbuni ndiye ndege mkubwa kuliko wote duniani na ndege hawa wanapatikana barani Africa pekee. Mbuni anafikia hadi urefu wa futi 7 mpaka 8 na uzito wake ni 130-150KG na anataga mayai kuanzia 6-12 na hutamia kwa siku 40 na yai lake moja lina uzito wa kg 1.6 na pia yai lake moja lina mayai 24 ya kanga. Na katika kipindi cha kutamia mayai familia ya mbuni huchagua dume mkuu na jike mkuu ambao watashirikiana katika kuyatamia, dume atatamia usiku kutokana na yeye kuwa na rangi nyeusi na jike atatamia mchana kwa sababu yeye ana rangi ya kijivu (grey colour ). Na huwa wanafanya hivi kwa sababu hawa ndege wana kitu kinachoitwa camouflage colour (Rangi ya manyoya yao ambayo inaendana na mazingira wanayoishi) kwa hiyo dume akitamia usiku itakuwa ni vigumu kuonekana na maadui kutokana na rangi yake nyeusi ambayo humfanya asionekane na maadui kwa urahisi halikadhalika kwa upande wa jike yeye hutamia mchana kutokana na rangi yake ya kijivu ambayo humfanya afananie na nyasi na vifaranga vya mbuni hupevuka vikishafikisha miaka 3-5. Hawa ndege huwa wanaishi katika familia na dume huweza kujamiana na jike yoyote yule katika ile familia. Mbuni pia ndiye ndege mwenye kasi zaidi nchi kavu na anauwezo wa kukimbia hadi kilometers 70 kwa saa pia mbuni katika miguu yake ana vidole vyenye kwato mbili kwa kila miguu ambayo humuwezesha yeye kuweza kumudu mazingira yake anayoishi pia kumuokoa na hatari ya maadui kwa kukimbia pale anapovamiwa. Mbuni ni ndege ambaye hana uwezo wa kuruka kama ndege wengine yeye hutegemea tu kasi katika kujihami na maadui na zipo sababu sinazomfanya mbuni asiweze kuruka kama ndege wengine, sababu ya kwanza ni uzito wake mkubwa na pia katika miguu yake ana kitu kinachoitwa uroto (borne marrow, kwa wale wanaokula makongoro kuna mafuta yanayopatikana katikati ya miguu hayo ndiyo borne marrow ), sababu nyingine inayomfanya mbuni asiweze kuruka ni kuwa hawana kitu kinachoiwa keel ( mfupa unaopatikana maeneo ya kifuani ambayo humuwezesha ndege kuruka ), sababu nyingine ni kuwa mifupa ya mabega yake imeungana kwa pamoja ambayo humuwia vigumu yeye kuweza kuruka na pia uchache wa manyoya yake. Tofauti kubwa kati ya jike na dume la mbuni ni rangi, jike anakuwa na rangi ya kijivu na dume anakuwa na rangi nyeusi pia jike anakuwa mdogo kuliko dume na pia manyoya ya mbuni hutumika kutengenezea vitu kama wallet, hand bag, viatu pamoja na na jackets. Na miguu yake mirefu pamoja na shingo yake refu humuwezesha kuona mbali na hata kuwaona maadui kwa ukaribu zaidi. Mbuni ni ndege ambao hawategemei sana kunywa maji kwa sababu wao hupata maji yao kutoka katika majani wanayokula pia wakati mwingine hula wadudu, mijusi na na rodent wadogo wadogo na maadui wakubwa wa mbuni ni simba, cheetah, pamoja na binadamu ambao huwawinda kwa sababu ya nyama. Na maisha yao kwa ujumla ni miaka 50 na hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa ndege ni NGORONGORO CRATER, TARANGIRE NATIONAL PARK na SERENGETI NATIONAL PARK.
Hawana mbuni lakini katika bara la America wana ndege ambaye anafanana sana na mbuni ambaye anaitwa Rhea huyu ukimuangalia amefanana sana na mbuni lakini sio mbuni
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.