Ndege mkubwa kuliko ndege wote duniani

Ndege mkubwa kuliko ndege wote duniani

Mbuni anayepatikana hasa Afrika Mashariki ndiye ndege mrefu na mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kufikia urefu wa futi 9 na uzito wa kilo 156. Japokuwa ndege huyu ana mabawa cha kushangaza hana uwezo wa kuruka kama ndege wengine wenye sifa sawa ambao tumezoea kuwaona wakiruka angani.

1. Uzito mkubwa wa mbuni upo kwenye miguu yake ambayo ndiyo silaha yake kubwa dhidi ya maadui zake. Yasemekana teke moja la Mbuni laweza kumuua BINADAMU NA hata Simba...

2. Wakati hayawani na ndege wengine wakiwa na tumbo moja, Mbuni wana Matumbo matatu.........

3. Mbuni ndiye ndege mwenye kasi kuliko ndege wote ama hata wanyama wenye miguu miwili, Kasi ya Mbuni ni Km 70/saa na HATUA MOJA YA MBUNI inaweza kufika hata m5. Mbuni ana Kasi Kuliko hata Farasi . Mnyama mwenye kasi kuliko viumbe wote ni Duma...Duma wanaweza kukimbia kwa kasi zaidi kuliko nyingine yoyote nchi mnyama kwa haraka kama 112-120 km / h (70-75 mph)

4. Yai la Mbuni ndilo kubwa kabisa kupita mayai ya ndege wote likiwa na urefu wa sm15. Yai hili pia ni gumu kiasi kwamba unaweza kusimama juu yake

Uzito wa yai la ndege huyu ni takribani kg. 1.4 ambao ni zaidi ya mara ishirini ya uzito wa yai la kuku na ili kupika yai la mbuni hadi lichemke inachukua zaidi ya saa moja. Kadhalika Mayai ya mbuni huatamiwa kwa muda wa siku 42 hadi kutotolewa vifaranga na kwa wastani mbuni hutaga mayai kati ya 40 hadi 100 kwa mwaka

5. Manyoya ya mbuni yana historia ya kusisimua sana kwasababu hapo zamani katika dola ya Misri ya kale yalikua yakitumika kama alama ya haki na kwa kipindi cha sasa yamekua yakitumiwa na wataalam wa mavazi kwa ajili ya kuweka nakshi kwenye mitindo mbalimbali ya mavazi.

6. Jicho la mbuni kenye sm 5 ndilo Jicho kubwa kuliko wanyama wote duniani likimsaidia kuweza kuona mbali na hasa maadui zake. Jicho la Mbuni ni Kubwa kuliko hata Ubongo wake

7. Mbuni hawana meno hivyo hutegemea sana mawe kusagia vyakula vyao. Mbuni hakosi kutembea na mawe popote unapomkuta na yasemekana si chini ya Kg 1

8. Dume la Mbuni Linangurumo kama za SIMBA

9. Wanahistoria wengi wanaamini kuwa mbuni wamekua wakiwindwa tangu maelfu ya miaka ya zamani sio kwasasbabu ya nyama tu, bali pia kwa uzuri wa manyoya unaovutia sana. Tahadhari ni kwamba Usicheze kabisa na mbuni kwenye anga za yai lake

10. MBUNI ni ndege mwenye ushirikiano zaidi ya binadamu hasa katika kipindi cha kuatamia mayai mbuni hugawana majukumu ambako jike huatamia wakati wa mchana na dume huatamia wakati wa usiku

11. Mguu wa mbuni una vidole viwili vyenye kucha kwa mbele na kidole cha nje huwa hakina kucha wakati ndege wengine huwa na vidole vitatu hadi vine na uwepo wa vidole hivi humsaidia kuwa na mwendo kasi wa ajabu sana kuliko ndege wengine duniani.

The Masai Ostrich
 
Duma wanaweza kukimbia kwa kasi zaidi kuliko mnyama ama ndege yoyote yule duniani kwa haraka kama 112-120 km / h (70-75 mph) .......basi linalokimbia km80/saalinaachwa mbali sana na Duma na ukizingatia foleni n heri upande duma ili uwahi
Kiumbe mwenye kasi kuzidi wote duniani ni pellegrin falcon.
 
Kiumbe mwenye kasi kuzidi wote duniani ni pellegrin falcon.
They are commonly referred to as the Duck Hawk. Peregrine falcons are the fastest-
flying birds in the world at 390/h
 
Amavubi, ahsante sana kwa somo hilo la Mnyama / Ndege Mbuni. Nimeelimika kweli.

Mimi siku zote nilijua Ndege MBABE kuliko wote ni Tai (Eagle), hapa sijasema kuhusu kasi na uwezo wa kuona mbali. Sasa nisaidie amavubi, kwa ubabe wa Tai, anaweza kumdhibiti Mbuni?!

Ahsante
 
Mgeni ni wewe kwa Taarifa yako hiyo familia nahusiana nayo na Hao bata mzinga walikuwa wakija kula na hata kulala kwa mzee Ali Fuse Na Pia Nimeshakuambia Mbuni huruhusiwi kuwafuga ni Nyara ya Serikali
mkuu kwani bata mzinga sio nyara ya serikali? au nyara za serikali zikoje
 
Duma wanaweza kukimbia kwa kasi zaidi kuliko mnyama ama ndege yoyote yule duniani kwa haraka kama 112-120 km / h (70-75 mph) .......basi linalokimbia km80/saalinaachwa mbali sana na Duma na ukizingatia foleni n heri upande duma ili uwahi
lakini kumbuka duma hawezi fikisha kilometa nyingi kwani akikimbia umbali mrefu huweza kufa sabab joto la mwili wake likipanda kushuka ni kazi
 
Mbuni yupo katika order inayofahamika kama STRUTHIONIFORMES na family yake ni STRUTHIONIDAE na jina lake la kisayansi (scientific name ) ni STRUTHIO CAMELUS.

Mbuni ndiye ndege mkubwa kuliko wote duniani na ndege hawa wanapatikana barani Africa pekee. Mbuni anafikia hadi urefu wa futi 7 mpaka 8 na uzito wake ni 130-150KG na anataga mayai kuanzia 6-12 na hutamia kwa siku 40 na yai lake moja lina uzito wa kg 1.6 na pia yai lake moja lina mayai 24 ya kanga.

Na katika kipindi cha kutamia mayai familia ya mbuni huchagua dume mkuu na jike mkuu ambao watashirikiana katika kuyatamia, dume atatamia usiku kutokana na yeye kuwa na rangi nyeusi na jike atatamia mchana kwa sababu yeye ana rangi ya kijivu (grey colour ). Na huwa wanafanya hivi kwa sababu hawa ndege wana kitu kinachoitwa camouflage colour (Rangi ya manyoya yao ambayo inaendana na mazingira wanayoishi) kwa hiyo dume akitamia usiku itakuwa ni vigumu kuonekana na maadui kutokana na rangi yake nyeusi ambayo humfanya asionekane na maadui kwa urahisi halikadhalika kwa upande wa jike yeye hutamia mchana kutokana na rangi yake ya kijivu ambayo humfanya afananie na nyasi na vifaranga vya mbuni hupevuka vikishafikisha miaka 3-5.

Hawa ndege huwa wanaishi katika familia na dume huweza kujamiana na jike yoyote yule katika ile familia. Mbuni pia ndiye ndege mwenye kasi zaidi nchi kavu na anauwezo wa kukimbia hadi kilometers 70 kwa saa pia mbuni katika miguu yake ana vidole vyenye kwato mbili kwa kila miguu ambayo humuwezesha yeye kuweza kumudu mazingira yake anayoishi pia kumuokoa na hatari ya maadui kwa kukimbia pale anapovamiwa.

Mbuni ni ndege ambaye hana uwezo wa kuruka kama ndege wengine yeye hutegemea tu kasi katika kujihami na maadui na zipo sababu zinazomfanya mbuni asiweze kuruka kama ndege wengine, sababu ya kwanza ni uzito wake mkubwa na pia katika miguu yake ana kitu kinachoitwa uroto (borne marrow, kwa wale wanaokula makongoro kuna mafuta yanayopatikana katikati ya miguu hayo ndiyo borne marrow ), sababu nyingine inayomfanya mbuni asiweze kuruka ni kuwa hawana kitu kinachoiwa keel ( mfupa unaopatikana maeneo ya kifuani ambayo humuwezesha ndege kuruka ), sababu nyingine ni kuwa mifupa ya mabega yake imeungana kwa pamoja ambayo humuwia vigumu yeye kuweza kuruka na pia uchache wa manyoya yake.

Tofauti kubwa kati ya jike na dume la mbuni ni rangi, jike anakuwa na rangi ya kijivu na dume anakuwa na rangi nyeusi pia jike anakuwa mdogo kuliko dume na pia manyoya ya mbuni hutumika kutengenezea vitu kama wallet, hand bag, viatu pamoja na jackets.

Miguu yake mirefu pamoja na shingo yake ndefu humuwezesha kuona mbali na hata kuwaona maadui kwa ukaribu zaidi. Mbuni ni ndege ambao hawategemei sana kunywa maji kwa sababu wao hupata maji yao kutoka katika majani wanayokula pia wakati mwingine hula wadudu, mijusi na rodents wadogo wadogo.

Maadui wakubwa wa mbuni ni simba, cheetah, pamoja na binadamu ambao huwawinda kwa sababu ya nyama. Na maisha yao kwa ujumla ni miaka 50 na hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa ndege ni NGORONGORO CRATER, TARANGIRE NATIONAL PARK na SERENGETI NATIONAL PARK.

f68f2a24d3984010758dbef899512b2e.jpg
 
Back
Top Bottom