Ndege mkubwa kuliko ndege wote duniani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Mbuni anayepatikana Africa na hasa Afrika Mashariki ndiye ndege mrefu na mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kufikia urefu wa futi 9 na uzito wa kilo 156.
ostrich-facts.jpg

1. Uzito mkubwa wa mbuni upo kwenye miguu yake ambayo ndiyo silaha yake kubwa dhidi ya maadui zake. Yasemekana teke moja la Mbuni laweza kumuua BINADAMU NA hata Simba...
9de25fe2eb970d7bde439427f01cdf0c.jpg

2. Mbuni wana Matumbo matatu.........
hqdefault.jpg

3. Mbuni ndiye ndege mwenye kasi kuliko ndege wote ama hata wanyama wenye miguu miwili, Kasi ya Mbuni ni Km 70/saa na HATUA MOJA YA MBUNI inaweza kufika hata m5. Mbuni ana Kasi Kuliko hata Farasi

Duma wanaweza kukimbia kwa kasi zaidi kuliko mnyama ama ndege yoyote yule duniani kwa haraka kama 112-120 km / h (70-75 mph) .......basi linalokimbia km80/saalinaachwa mbali sana na Duma na ukizingatia foleni n heri upande duma ili uwahi
Ostriches-fast-furious-run-faster-728.jpg

4. Yai la Mbuni ndilo kubwa kabisa kupita mayai ya ndege wote likiwa na urefu wa sm15. Uzito wa Yai moja la mbuni ni sawa na uzito wa dazani mbili za mayai ya kuku. Yai hili pia ni gumu kiasi kwamba unaweza kusimama juu yake
images
\
Uzito wa yai la ndege huyu ni takribani kg. 1.4 ambao ni zaidi ya mara ishirini ya uzito wa yai la kuku na ili kupika yai la mbuni hadi lichemke inachukua zaidi ya saa moja. Kadhalika Mayai ya mbuni huatamiwa kwa muda wa siku 42 hadi kutotolewa vifaranga na kwa wastani mbuni hutaga mayai kati ya 40 hadi 100 kwa mwaka
321322-18514-5.jpg

5. Manyoya ya mbuni yana historia ya kusisimua sana kwasababu hapo zamani katika dola ya Misri ya kale yalikua yakitumika kama alama ya haki na kwa kipindi cha sasa yamekua yakitumiwa na wataalam wa mavazi kwa ajili ya kuweka nakshi kwenye mitindo mbalimbali ya mavazi.

6. Jicho la mbuni kenye sm5 ndilo Jicho kubwa kuliko wanyama wote duniani likimsaidia kuweza kuona mbali na hasa maadui zake. Jicho la Mbuni ni Kubwa kuliko hata Ubongo wake

8b59d39db6cb77d1746efda9a7b01c27.jpg

7. Mbuni hawana meno hivyo hutegemea sana mawe kusagia vyakula vyao. Mbuni hakosi kutembea na mawe popote unapomkuta na yasemekana si chini ya Kg1

8. Dume la Mbuni Linangurumo kama za SIMBA
16-male-ostrich.jpg

9. Wanahistoria wengi wanaamini kuwa mbuni wamekua wakiwindwa tangu maelfu ya miaka ya zamani sio kwasasbabu ya nyama tu, bali pia kwa uzuri wa manyoya unaovutia sana. Tahadhari ni kwamba Usicheze kabisa na mbuni kwenye anga za yai lake

Top-20-most-funny-Angry-birds-memes-and-Jokes-.-.-.-Hilarious-Funny-Jokes-Funniest1.jpg

10. MBUNI ni ndege mwenye ushirikiano zaidi ya binadamu hasa katika kipindi cha kuatamia mayai mbuni hugawana majukumu ambako jike huatamia wakati wa mchana na dume huatamia wakati wa usiku

11. Mguu wa mbuni una vidole viwili vyenye kucha kwa mbele na kidole cha nje huwa hakina kucha wakati ndege wengine huwa na vidole vitatu hadi vine na uwepo wa vidole hivi humsaidia kuwa na mwendo kasi wa ajabu sana kuliko ndege wengine duniani.
 
Mbuni anayepatikana Africa na hasa Afrika Mashariki ndiye ndege mrefu na mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kufikia urefu wa futi 9 na uzito wa kilo 156.
ostrich-facts.jpg

U1. zito mkubwa wa mbuni upo kwenye miguu yake ambayo ndiyo silaha yake kubwa dhidi ya maadui zake. Yasemekana teke moja la Mbuni laweza kumuua hata Simba...
9de25fe2eb970d7bde439427f01cdf0c.jpg

2. Mbuni wana Matumbo matatu.........
hqdefault.jpg

3. Mbuni ndiye ndege mwenye kasi kuliko ndege wote ama hata wanyama wenye miguu miwili, Kasi ya Mbuni ni Km 70/saa na mruko mmoja wa umbani unaweza kufika hata m5. Mbuni ana Kasi Kuliko hata Farasi
Ostriches-fast-furious-run-faster-728.jpg

4. Yai la Mbuni ndilo kubwa kabisa kupita mayai ya ndege wote likiwa na urefu wa sm15. Uzito wa Yai moja la mbuni ni sawa na uzito wa dazani mbili za mayai ya kuku. Yai hili pia ni gumu kiasi kwamba unaweza kusimama juu yake
images

321322-18514-5.jpg

5. Manyonya ya Mbuni ni maarufu kote duniani kwa mapambo, nyama ya mbuni hutumika kama kitoweo kadhalika ngozi yake ni kwa ajili bidhaa za ngozi kama mikoba, mikanda na hata viatu

6. Jicho la mbuni kenye sm5 ndilo Jicho kubwa kuliko wanyama wote duniani likimsaidia kuweza kuona mbali na hasa maadui zake. Jicho la Mbuni ni Kubwa kuliko hata Ubongo wake

7. Mbuni hawana meno hivyo hutegemea sana mawe kusagia vyakula vyao. Mbuni hakosi kutembea na mawe popote unapomkuta na yasemekana si chini ya Kg1

8. Mbuni pia hutumika kwa ushirikika kwa baadhi ya nchi za Afrika kama Misri

8b59d39db6cb77d1746efda9a7b01c27.jpg

9. Dume la Mbuni Linangurumo kama za SIMBA
16-male-ostrich.jpg

10. Usicheze kabisa na mbuni kwenye anga za yai lake

Top-20-most-funny-Angry-birds-memes-and-Jokes-.-.-.-Hilarious-Funny-Jokes-Funniest1.jpg
ahsaante kwa kutujuza ..
 
hapa Mwanza maeneo ya kilimahewa na kona yabwiru kuna mwarabu mmoja anaitwa Mchimkenda aliwahi kufuga hawa mbuni ila walikuwa sio wakubwa sana,yaani walikuwa kivutio sana sema sasa yeye alikuwa anawaachia wanajichunga wao,mbuni hawa walikuwa wakipita kwako wakikuta sabuni ya kufulia wanakula na walikuwa wababe kweli,ila kunakingine nilicho gundua ukitaka kumchanganya mbuni muwekee au au vae mfuko katikakati ya shingo yake huwa anachanganyikwa kabisa atakimbia vibaya mno na kuchanganyikiwa kabisa
 
Apo kwenye kasi kuliko wanyama wote vipi kuhusu duma?

Back
Top Bottom