Mimi nilikuwa ni mwanachama na mpenzi wa dhati wa Chama Cha Mapinduzi nilikuwa silipwi nilikuwa nimejitolea kukiunga mkono Chama changu cha awali.
Ila nimeamua kukihama Chama cha Mapinduzi baada ya kushuhudia mambo ambayo nimeona hayako sawa ilani inapuuzwa katiba inapuuzwa,na mambo mengi ya kutisha dhidi ya wananchi.
Nilipokuwa ndani ya CCM nimeshuhudia haswa katika (awamu hii ya tano)mambo ya "kinazi" wanayofanyiwa wapinzani (ambao wapo kikatiba) ukiukwaji wa haki za binadamu.
Nimeamua kukihama Chama cha Mapinduzi kwa ridhaa yangu bila ya kulazimishwa na nimejiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
Wapinzani sio maadui kama tulivyoaminishwa huko nyuma wapinzani ndio wakosoaji na wachokonozi wakubwa tokea nihamie Chadema nimeanza kuufahamu upinzani vyema kabisa hakuna Udini wala Ukabila.