Ndege ivutwe na wananchi utegemee watu kupona?

Hii nchi hovyo sana angalia baada ya miaka 50 ya uhuru Maji tu matatizo,sembuse kuokoa wahanga wa ajali ya Ndege.
 
Juzi eti wanatumika kuzima eti motooo!!kwenye mlima!!kuna mwananchi mmoja alikuwa anasema bnana jamaa ni hatari moto ulipowaona tu ukaanza kupungua!!!jamaa anatumia buti tu zusigina kisiki chenye moto kinazimika!!!HII NCHI RAHA SANA WALA HUTAKIWI KUHAMA.
Tatizo ni elimu,

Wengi wana elimu ndogo ajabu wamepewa madaraka.

Na raia ndio kabisa.
 
Juzi eti wanatumika kuzima eti motooo!!kwenye mlima!!kuna mwananchi mmoja alikuwa anasema bnana jamaa ni hatari moto ulipowaona tu ukaanza kupungua!!!jamaa anatumia buti tu zusigina kisiki chenye moto kinazimika!!!HII NCHI RAHA SANA WALA HUTAKIWI KUHAMA.
elimu kaka ... hata uelewa tu ....
 
Kwa taarifa zilizoonekana wazi, wananchi ndio walikuwa mstari wa mbele kwenye uokoaji wa ndege pale Bukoba hasa kwenye hatua za mwanzo za uokoaji hawa ni watu wa kupongezwa sana.

Mara kadhaa kumekuwa na majaribio ya kujiandaa na dharura viwanja vya ndege natumaini mengi wanajifunza, matukio mbali mbali yanayotokea nchini yanatosha pia kuleta changamoto na mafundisho ya kukabili changamoto za usoni.

Kwa hali ilivyokuwa kwenye ajali, uokoaji wa kisasa ulihitajika sana ili kuwapa msaada abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo. kuvuta kamba hakuwezi kufanikisha uokozi wa abiria kwa asilimia kubwa.

Ashukuriwe Mungu watu 26 wameokolewa, poleni sana waliopatwa na msiba kutokana na raia wengine 19 kufariki wakiwa ni abiria na rubani katika ajali hiyo.

Ifike mahali kama nchi, tuweke jitihada kwenye miundombinu ya tahadhari na dharura ili kukabili matatizo ya ajali za vyombo vya moto na moto wenyewe.
Kuvuta ndege ilikuwa ni hatua ya baadae sana, kipaumbele ilikuwa ni kuwatoa watu kwanza. Hao hao wavuvi na mitumbwi yao isiyo na mashine ndio waliowaokoa wote ambao walikuwa hawajasakamwa na maji, hasa waliokuwa sehemu ya nyuma ya ndege.

Mv Spice
Mv Sarender sijui sirenda pale Mwanza
Mv Bukoba
Ajali ya Ndege
Na ajali za magari...

Tz Bado sana
MV Spice ilizama usiku taratibu. Abiria walipigia simu ndugu zao. Wengine walipiga Redio kuomba msaada wa watawala.
Waliokuwa wakiokowa ni wavuvi. Serikali walifika asubuhi kuokota maiti.
 
MV Spice ilizama usiku taratibu. Abiria walipigia simu ndugu zao. Wengine walipiga Redio kuomba msaada wa watawala.
Waliokuwa wakiokowa ni wavuvi. Serikali walifika asubuhi kuokota maiti.
Dah inauma Sana hii
 
Back
Top Bottom