Creative Monster
Member
- Jul 22, 2019
- 10
- 27
Kwa taarifa zilizoonekana wazi, wananchi ndio walikuwa mstari wa mbele kwenye uokoaji wa ndege pale Bukoba hasa kwenye hatua za mwanzo za uokoaji hawa ni watu wa kupongezwa sana.
Mara kadhaa kumekuwa na majaribio ya kujiandaa na dharura viwanja vya ndege natumaini mengi wanajifunza, matukio mbali mbali yanayotokea nchini yanatosha pia kuleta changamoto na mafundisho ya kukabili changamoto za usoni.
Kwa hali ilivyokuwa kwenye ajali, uokoaji wa kisasa ulihitajika sana ili kuwapa msaada abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo. kuvuta kamba hakuwezi kufanikisha uokozi wa abiria kwa asilimia kubwa.
Ashukuriwe Mungu watu 26 wameokolewa, poleni sana waliopatwa na msiba kutokana na raia wengine 19 kufariki wakiwa ni abiria na rubani katika ajali hiyo.
Ifike mahali kama nchi, tuweke jitihada kwenye miundombinu ya tahadhari na dharura ili kukabili matatizo ya ajali za vyombo vya moto na moto wenyewe.