Nchimbi adanganya bunge kuhusu Mtwara

Nchimbi adanganya bunge kuhusu Mtwara

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
3,575
Reaction score
528
Jamani walioko mtwara tunaomba mtupe ukweli maana Emmanuel Nchimbi kakanusha kuwa hakuna mtu aliyekufa Mtwara kuna majeruhi wa 2 na waliokamatwa na polisi 91 na kuna JWTZ walikuwa wameombwa kwenda kusaidia walipinduka 20 walijeruhiwa, 4 walikuwa na jumla yao ilikuwa 30. Je, nani mkweli jamani
 
akitoa taarifa kwa niabaya ya waziri mkuu amesema hayo maneno cha ajabu zaidi kuna vyombo kama ITV, Wapo radio na hata magazeti mengi yameripoti kuna watu walio umizwa na kuuawa. Sasa waziri anadanganya ili iweje?
 
ndio tunachokitaka hasa sisi amabo hatupo Mtwara tunahitaji habari za uhakika
 
kama kweli kandanganya tumuchukulie hatua gani? na anajua alichokiongea kmatokeo yake yatakuwaje?
 
kila siku huwa nasema kauli za serikali ndio chanzo cha vurungu jana waziri wanishati na madini ndiye alianzisha hii vurungu kulikuwa na haja gani yakuongea kauli "bomba la gesi lijengwe"
 
kama hujui kilichotokea utasemaje kadanganya. hatuwezi kuwaruhusu wahuni kama wewe mvuruge nchi yetu kwa uchochezi usio na maana. somalia wanapata faida gani? kongo wanapata faida gani? burundi walipata nini. tunataka fikra za kugeuza uchumi wetu twende mbele sio kuwasikiliza wavurugaji turudi nyuma
 
Mi nimesikiliza TBC radio mkuu wa jeshi flani wa huko Nachingwea nadhani alisema wanajeshi 4 wamefariki na hawakuombwa kwenda.

Nchimbi kasema waliomba usaidizi.
 
nimeona anatangaza vifaa vilivyoteketea ni za viongozi wa ccm na watendaji wa serikali sijasiki hata kama kuna vitu vya wananchi vimeharibiwa ina maana mtwara binadamu ni ccm tu?
 
Mi nimesikiliza tbc radio mkuu wa jeshi flani wa huko Nachingwea nadhani alisema wanajeshi 4 wamefariki na hawakuombwa kwenda.

Nchimbi kasema waliomba usaidizi.
hapo ndio kwenye mkanganyiko mkuu yaani kwa kauli hii hakika serikali na ccm itaingali damu
 
...mkuu usipate shida sana, mpe siku mbili tu atakuja kuweka sawa na atasema hakusema hivyo amenukuliwa vibaya, only in DRT...
 
nimeona anatangaza vifaa vilivyoteketea ni za viongozi wa ccm na watendaji wa serikali sijasiki hata kama kuna vitu vya wananchi vimeharibiwa ina maana mtwara binadamu ni ccm tu?

Jana tulitaarifiwa kuwa Polisi kwa kutumia mgongo wa "msako" walikuwa wanapora mali za wananchi hasa madukani!
 
kama hujui kilichotokea utasemaje kadanganya. hatuwezi kuwaruhusu wahuni kama wewe mvuruge nchi yetu kwa uchochezi usio na maana. somalia wanapata faida gani? kongo wanapata faida gani? burundi walipata nini. tunataka fikra za kugeuza uchumi wetu twende mbele sio kuwasikiliza wavurugaji turudi nyuma

wewe akili yako inamatatizo tumwamini nani vyombo vya habari vimetangaza na tumeona kwenye ITV inamaana walikuwa wanadanganya? wewe ndiye mhuni na na usiwe mtumwa wa mawazo ndugu yangu hakika mifano unayoitoa haina faida yoyote kama unajificha hapo kwenye ujinga kama huo subiri mtandanganya mpaka lini?
 
Jamani walioko mtwara tunaomba mtupe ukweli maana Emmanuel Nchimbi kakanusha kuwa hakuna mtu aliyekufa Mtwara kuna majeruhi wa 2 na waliokamatwa na polisi 91 na kuna JWTZ walikuwa wameombwa kwenda kusaidia walipinduka 20 walijeruhiwa, 4 walikuwa na jumla yao ilikuwa 30. Je, nani mkweli jamani

acha kupotosha wewe. unasikiliza kwa kutumia media gani maana sisi tuliosikiliza tbc tumemsikia akisema kuwa kuna mtu mmoja amekufa na askari wa jwtz.
 
Jana tulitaarifiwa kuwa Polisi kwa kutumia mgongo wa "msako" walikuwa wanapora mali za wananchi hasa madukani!

mkuu unajua ni bora serikali ingekaa kimya kuliko kutoa taarifa kama hizi tumesikilza hadi BBC wamesema kuna watu wamefariki na majeruhi kibao sasa mbona yeye kandanganya Bunge ili iweje
 
acha kupotosha wewe. unasikiliza kwa kutumia media gani maana sisi tuliosikiliza tbc tumemsikia akisema kuwa kuna mtu mmoja amekufa na askari wa jwtz.

ni mawzo yako mimi na unahaki ya kuongea na kutetea ujinga huo
 
acha kupotosha wewe. unasikiliza kwa kutumia media gani maana sisi tuliosikiliza tbc tumemsikia akisema kuwa kuna mtu mmoja amekufa na askari wa jwtz.

jana mkuu wa mkoa akihojiwa na wapo radio alikanusha kuwa hakuna vurungu je, hao JWTZ waliokufa walikuwa wanapelekwa wakafabye nini? Akili yako tu inatosha ukiwa wakufikiria nausifikirishwe
 
Jamani walioko mtwara tunaomba mtupe ukweli maana Emmanuel Nchimbi kakanusha kuwa hakuna mtu aliyekufa Mtwara kuna majeruhi wa 2 na waliokamatwa na polisi 91 na kuna JWTZ walikuwa wameombwa kwenda kusaidia walipinduka 20 walijeruhiwa, 4 walikuwa na jumla yao ilikuwa 30. Je, nani mkweli jamani

Ikigundulika na ww umedanganya JF tukufanyeje? Nchimbi kasema mtu mmoja ameuawa, soma Extracts hapa:

Anasema chanzo kikuu cha vurugu ni kupinga gesi kusafirishwa kutoka Mtwara hadi Dar. Vurugu zilianza kwa kusambazwa vipeperushi vya kuhamasishana kufanya vurugu

Athari
Nyumba ya Mbunge imechomwa, ofisi za CCM kata, Nyumba na ofisi mbalimbali, mtu mmoja ameuawa na wengine wamejeruhiwa.


watu 91 wamekatwa, hali hiyo imedhibitiwa jeshi la ulinzi limeenda kwa ombi la RC ambapo wakiwa njiani kuelekea huko askari 4 wamefariki kwa ajali ya gari

Nawapongeza askari waliofanya kazi katika mazingira magumu kurudisha hali ya amani
 
taarifa ya nchimbi na kilichotokea ni sahihi kabisa. Bado hajadanganya.
 
Jamani walioko mtwara tunaomba mtupe ukweli maana Emmanuel Nchimbi kakanusha kuwa hakuna mtu aliyekufa Mtwara kuna majeruhi wa 2 na waliokamatwa na polisi 91 na kuna JWTZ walikuwa wameombwa kwenda kusaidia walipinduka 20 walijeruhiwa, 4 walikuwa na jumla yao ilikuwa 30. Je, nani mkweli jamani

mkuu huoni aibu kusema uongo mbona nchimbi kasema wamekufa 5 askari 4 na raia 1
 
Back
Top Bottom