Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Africa sijui tutakuja kuamka lini aisee
Unaona viongozi wanapambana sana na Internet linapofika suala la mambo ya msingi mustakabali wa maisha yetu na kutaka haki na utawala bora. Ukweli ni kwamba aidha watake au wasitake hawawezi kupambana na teknolojia. Mwanzo walianzaga hivihivi, wakaanza kusema hayo ni mambo ya kwenye mitandao, walipoona wanafeli wakaanza kuanzisha sheria ngumungumu ili tu kuwabana wananchi, mara huwezi kupublish kitu bila leseni.
Juzi Makonda kasema huruhusiwi kupost kuhusu Serikali, au kushare chochote kwenye mitandao kuisema Serikali pasipo na kibali akidhani ya kwamba wanaweza kupambana na teknolojia. Haya wenzetu majirani zetu Waganda, leo wamezima internet for reason kuwa inapisha uchaguzi, swali jepesi ni kuwa Je Internet inazuia vipi uchaguzi? au inasaidia kufanyika vitu kwa uwazi na uhakika?
Hii vita ni bora ile ya wakoloni ila sio hii ya wenyewe kwa wenyewe. Ngoja iendelee kunyesha, tutajua tu panapovuja.