The Whistleblower
Senior Member
- Dec 9, 2022
- 137
- 224
JF ina moderator mwislamu,anafuta makala zote zinazoisifia Israel na makala zote za kidini kutukuza Uislamu ndo zimejaa humu,huyu moderator afukuzwe Kazi mara mojaViongozi wa nchi za kiislamu wasijitumbukize katika ujinga utakaowagharimu dunia na akhera yao.Kama ni maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu Palestina yapo makumi kadhaa na hayajatekelezwa hata moja.Kinyume chake maazimio hayo yanavunjwa mbele ya macho yao.
Anthony Blinken ameitembelea Israel kuipa pole kutokana na mashambulizi ya Hamas kwenye ardhi zao.Sambamba na yeye ndege za mizigo zimekuwa zikipeleka shehena kubwa za silaha nchini Israel ambayo tangu hapo haina upungufu wa vifaa hivyo.
Sambamba na hilo tena meli kubwa ya kivita na ya kisasa kuliko zote imeshapelekwa jirani kabisa na Gaza na karibu na Israel.Meli hiyo kwa ukubwa wake na vifaa vilivyomo na idadi ya askari wanaokuwemo humo ni sawa na kusema kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani imesogezwa karibu kuisaidia Israel kuimaliza Palestina.
Wakati wa press conference hapo jana kati ya Blinken na Netanyahu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani alitaja udugu alionao na Israel.Katika kuomboleza vifo vya raia wa Israel alitokwa na machozi katikati ya hotuba yake.
Baada ya kuondoka hapo imeelezwa ratiba inaonesha ataendelea na ziara kuzitembelea Jordan,Misri na Saudi Arabia.
Nini anakwenda kuwaambia nchi hizo.Huku muda huo huo Israel inaongeza ukatili wake kwa wapalestina ikitaka watu milioni moja na ushei wahame makazi yao katika kipindi cha masaa 24.Pamoja na kwamba haiwezekani kwa muda huo watu idadi hiyo kuhama pia huko wanakoelezwa waende hakuna mazingira ya kuwapokea.Kote ni kifo tu.Watakaoshindwa kuhama watakapouliwa itatolewa sababu kuwa waliambiwa wahame.Kule wanakotakiwa kwenda hakuna nyumba,maji ,chakula na umeme na bado hakuna uhakika kuwa hawatadondoshewa mabomu
Kama ni udugu uliomliza Blinken kwa ndugu zake Israel,jee waislamu na waarabu hawana udugu ulio bora zaidi na wenzao wa Palestina.Waislamu wakizidi kuwa wajinga watamalizwa kabisa.