Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,192
- 10,926
Mnamo Novemba 20 mwaka huu 2023 mawaziri wa nchi tano za kiarabu na kiislamu walifunga safari kwenda China ili kutoa malalamiko yao na kutafutwa kuungwa mkono na nchi hiyo kuhusiana na suala la vita vilivyokuwa vikiendelea katika namna ya kutisha huko Gaza.
Mawaziri hao walikuwa ni kutoka nchi za Saudi Arabia,Misri,Jordan,Mamlaka ya Palestina na Indonesia.Safari hiyo ilikuwa ni kutekeleza azimio la mkutano mkubwa uliofanyika tarehe 11 Novemba huko Riyadh nchini Saudi Arab na kuzikutanisha nchi zaidi ya 52 kujadili suala hilo la Gaza.
Safari hiyo ya mawaziri wa nchi hizo kwanza ilifanyika wakati vita vimeshika nguvu na wapalestina hasa akinamama,watoto na wazee wakiuliwa katika namna ya wazi ya kutisha.Walioumia zaidi na vita hivyo walionekana wakichukua hatua japo ndogo iliyokuwa katika uwezo wao.Mfano mzuri wa watu hao wenye huruma ni Hizbullah wa Lebanon na Houth wa Yemen.
Kwa upande mwengine kuonesha kutokuwepo na haja ya safari hiyo ni ukweli kwamba kwenda China kushtaki masuala yanayohusu waislamu ni kama tumbili kupeleleka kesi yake kwa ngedere.China kama ni kuuwa waislamu na kuwadhalilisha imefanya hivyo zaidi ya Israel japokuwa mtindo wa uuwaji na udhalilishaji unatafautiana kidogo.
Baada ya kuondoka China ujumbe huo uliondoka kuelekea mataifa mengine ya nchi za Ulaya kwa malengo hayo hayo ya kulalamika wanavyotendewa wapalestina kutoka Israel.
Hata China nayo haikuupa uzito mkubwa msafara huo kwani ulipokewa na maafisha wa chini ya serikali na kuishia kuonana na waziri wa mambo ya nchi za nje pekee.
Kwa ujumla mawaziri hao wa nchi za nje wameeleza udhaifu mkubwa wa kidiplomasia wa nchi za kiislamu na kiarabu ambao wana udugu na ukaribu sana na ndugu zao wa Palestina na wanaunganishwa na wito wa kiimani baina yao.
Maraisi na mawaziri wa nchi ambazo si za kiislamu akiwemo waziri mkuu wa Spain wameweza kufika ndani ya Israel na kuonana na waziri mkuu mhalidu wa Israel na kumpa maneno makali ana kwa ana juu ya unyama wake anaoufanya kwa watu wa Gaza.
Haijulikani ni kitu gani kinachowakosesha kujiamini kwa nchi za kiislamu na kiarabu kwend kuonana na kumpa maonyo waziri mkuu wa Israel na badala yake wanaishia kupita pembeni pembeni kama nyumbu na fisi wanaoshuhudia mwenzao akiliwa na wanyama wakali.