Nchi za Afrika zina haki ya kuamua kuunga mkono au kupinga upande wowote kwenye migogoro

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
下载.jpg


Fadhili Mpunji

Hivi karibuni mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania walikutana na waandishi wa habari kwenye makazi ya balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, na kutoa mwito wa nchi za Afrika kuunga mkono msimamo wa Umoja wa Ulaya kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine. Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bibi Leberata Mulamula, alizungumzia uamuzi wa Tanzania kupiga kura ya kutopendelea upande wowote, akisema uamuzi huo wa Tanzania unaendelea na sera ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote.

Wakati dunia ikiendelea kupaza sauti kutaka mgogoro kati ya Russia na Ukraine utatuliwe, wachambuzi pia wameanza kufuatilia mambo ya kisiasa yaliyotokea kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo nchi mbalimbali zilipiga kura kuhusu azimio la kuilaani Russia kwa hatua iliyoichukua dhidi ya Ukraine. Matokeo ya upigaji kura kwenye baraza hilo yalitarajiwa na wengi, kwani nchi zote za magharibi zilikuwa na sauti moja ya kuilaani Russia na kupiga kura kuunga mkono azimio hilo, lakini haikutarajiwa kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kwa nchi za Afrika.

Kati ya nchi 54 za Afrika, nchi 28 ziliunga mkono azimio hilo, nchi 17 hazikuwa na maoni yoyote (abstained), nchi 8 hazikupiga kura kabisa, na nchi moja ilipinga azimio hilo. Baadhi ya wachambuzi wa nchi za magharibi wamezikosoa nchi za Afrika ambazo hazikuunga mkono azimio hilo kwa madai kwamba zinafumbia macho kitendo cha Russia, na kwamba kufanya hivyo kunaonesha kutojali taabu zinazowakabili watu wa Ukraine. Lakini ukosoaji huo pia unatokana na imani kwamba nchi za Afrika zinatakiwa kufuata mtazamo wa nchi za magharibi kuhusu mgogoro wa Ukraine, au kwenye mambo ya kimataifa kwa ujumla.

Upigaji kura wa nchi za Afrika kuhusu azimio hilo, umeonyesha kuwa Afrika ni bara linalothamini kujiamulia mambo yake, na kwamba kila nchi imepiga kura kwa mujibu wa mazingira yake, maslahi yake na historia yake. Pamoja na kuwa karibu nchi zote za Afrika zimeonyesha kuwa hazifurahii kuona taabu na vifo vya watu vinavyotokea Ukraine, na nyingine zimekosoa vikali matumizi ya mabavu kwenye kutatua mgogoro kati ya Russia na Ukraine, lakini pia zimeonyesha kuwa kila nchi ina mtazamo na msimamo wake kuhusu suala hilo.

Ikilinganishwa na nchi za magharibi, uhusiano kati ya nchi za Afrika na Russia ni mdogo. Lakini pia nchi za Afrika hazijasahau mchango mkubwa iliotoa Russia katika harakati za ukombozi wa nchi Afrika. Historia hiyo imeonekana kwenye msimamo wa nchi zilizoitwa nchi za mstari wa mbele kwenye ukombozi wa eneo la kusini mwa Afrika (Frontline states) ambazo zote hazikuunga mkono au kupinga azimio hilo.

Lakini pia nchi nyingine za Afrika zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo, na mjumbe wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kimani, alieleza sababu za kuunga mkono azimio hilo kutokana na sababu za kihistoria. Alikumbusha kuwa nchi za magharibi zilifanya uhalifu mwingi kwa kuvamia na kuzigawa nchi za Afrika, na kuweka mipaka ambayo haiendani na hali halisi na historia ya nchi za Afrika.

Katika historia ya upigaji kura kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, mara kadhaa China imekuwa haipigi kura ya kuunga mkono au kupinga. Safari hii China pia imefanya hivyo, kama zilivyofanya nchi 17 za Afrika. Lakini nchi kutopinga au kuunga mkono azimio hilo, hakumaanishi kuwa hazijali hali ya watu wanaokabiliwa na mgogoro huo, lakini ni kutokana na utatanishi wa kisiasa, kihistoria na kibinadamu kwenye suala linalopigiwa kura. Lakini pia kupiga kura hakutakuwa kuwe suala la mkumbo au suala la kulazimishwa bila kuzingatia maslahi ya nchi inayopiga.

China kwa mfano, licha ya kutounga mkono upande wowote imetangaza kutoa msaada wa kibinadamu wa dola za kimarekani milioni 1.57 kwa Ukraine ili kuwasaidia watu wanaokabiliwa na taabu. Afrika Kusini nayo, licha ya kuwa na msimamo kama China imesema imeomba kufanya juhudi kuwasiliana na Russia na kuishawishi ifanye mazungumzo na Russia ili kupata ufumbuzi wa amani wa mgogoro wa Ukraine.
 
Msimamo au ushauri wowote kutoka Africa hauna madhara yoyote kwa beberu, na huwa hauzingatiwi zaidi ni kupuuzwa tu.
 
Back
Top Bottom