WISDOM SEEDS
JF-Expert Member
- Jun 1, 2011
- 841
- 282
Kwanza tujiulize, mawaziri wa wizara zisizo za muungano huwa wanawakilisha
serikali ya nchi gani?
Katiba ya Tanganyika iliyounda muungano imeendelea kulindwa na Serikali yake bado ipo,
pamoja na viongozi wake kuwepo na kusimamia mambo yasiyo ya Muungano.
Katiba na sheria za Tanganyika ndizo zinazotumika katika eneo la Tanganyika kwa yale mambo
yasiyo ya Muungano kama ambavyo Katiba na sheria za Zanzibar zinavyotumika katika eneo
la Zanzibar kwa yale mambo ambayo si ya Muungano.
Kimtazamo, malalamiko ya wanancchi kudai uwepo wa serikali ya Tanganyika yana mantiki
kwa kuwa pamoja na hatua ya kuifuta Katiba ya Tanganyika, lakini kule kuendelea kutambua
kuwepo kwa sheria zisizo za muungano ni kutambua kuwepo kwa mamlaka ya Tanganyika
ambako sheria hizo kwa mambo yote yasiyo ya Muungano zinaendelea kutumika hadi leo.
Kwa maana hiyo sioni sababu ya watawala wa nchi hii kukataa serikali tatu...