Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nchi yetu inaitwa Tanganyika

[h=1]Wautakao Muungano ni Smz na sio wananchi wa Zanzanzibar hili liko wazi na jawabu Wtanganyika munalijuwa hamutaki jikateni kivyenu.[/h]Written by Hassan10 // 15/11/2011 // Habari // No comments

76821_174363709245339_143295315685512_664500_7625962_n-554x272.jpg

DAMU MZITO KULIKO MAJI, ZANZIBAR NIKWA WAZANZIBAR WOTE , SIASA ZINA PITA LAKINI ZANZIBAR IWEPO NA KIZAZI CHAKE.


JEE TUNDU LISU TAREHE 9 DECEMBER 1961 NIUHURU WA TANZANIA AU TANGANYIKA?
Maswala yanayo husu Muungano hayana nchi kubwa wala ndogo Tundu Lisu,kama hamutaki hivyo basi jikateni kwetu sisi ni sherehe tu.nikatu wazanzibar kusherehekea uhuru wetu wa Zanzibar na kusema uhuru wa Tanzania no way mzarau kwao mtumbwa.Kama hakuna usawa ktk maswala yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi smz jitoweni ktk utata huu , bila ya kutokufanya hivyo basi mutakinakamiza kizazi cha Wzanzibar na mujuwe huko twendako nikuipoteza Zanzibar ktk Makucha ya Tanganyika ijitayo Tanzania.
Hivi sasa ishara na dalili zote ziko wazi kuwa ccm Bara na Upinzani Bara na tasisi zote za kidini wote kitu kimoja lijapo swala la kuimeza Zanzibar lao moja , mumemsikia Tundu Lisa wa Chadema ana tafauti gani na Maneno alosema Mizengwe Pinda kuwa Zanzibar sio nchi?.
Jee ccm/smz Jee wajumbe wetu wa wawakilishi nikwa nini Mugaganie Muungano haliyakuwa hawa watu wanana nia nchema ya kuungana bali Zamira yao nikuifuta Zanzibar na kuifanya powerless.
Kama sio huu Muungano fake Zanzibar ingekuwa mbali hivi sasa kiuchumi na kimaendeleo,angalia visiwa vidodo vidogo viloko pempezoni mwa indian ocean mfano Moritios,Ushelisheli na vyenginevyo vilivyopiga hatuwa ya mandeleo why Zanzibar?.
Kwa hio tunawaomba Smz kuwa huko twendako mbeleni wenzetu wa Tanganyika wametutayarishia shimo kubwa lakuiingiza Zanzibar izidi kupoteza nguvu na power yake tubakie kuwa sote ni wa Tanzania/Tanganyika watu wa mkoa wa Pwani.
Umeona lini wewe upinzani kushindwa kukisakama chama tawala kilichoko madarakani badae ikawa wanasakama upande moja wa Muungano eti tu wameshindwa kikisalimicha kisiwa chao na watu wao kutokana na udogo wa nchi yao na watu wake.
Ndugu zangu Wzanzibar kama hatukujipapatuwa katika jindamizi hili la Muungano fake basi smz nchi wataipeleka pabaya kutokana na matamanio yao pempeni ya ubinafsi,
Ikiwa Tundu Lisu anasema vipi Zanzibar ipewe nafasi kubwa ktk Katiba ya Muungano haliyakuwa sio nchi kama vile Tanganyika sio nchi? Wewe balahau Tundu nazani mkonjwa wewe? Kwa nini ukiulizwa nani aloiuwa Tanganyika? Tanganyika ni kifo chakujitakia wenyewe wala Wzanzibar hawaku chirikishwa walo kushauriwa ktk kifo cha Tanganyika.
Ispokuwa ni nyiyi wenyewe kwa tama zenu zakijambazi na utapeli muliona tubadilishe jina la Tanganyika badae tuite Tanzania lakini harakati zote za Tanganyikika na nembo zote za Tanganyika ziwe zile zile nisawa na Zaire kuita Kongo hivi sasa.
Kwa hio waswahili wanasema muelekeza china ncha humpata yeye, Wzanzibar kike kiume mkubwa mdogo wote Muun gano hawautaki na hio sio siri wanaomba kila leo Muungano uvunjike na hii blab la ife.
Wanao utaka Muungano ni nyiyi majambazi na kutuletea jeshi mukatuwekea viongozi kwa nguvu wasio chaguwa la Wzanzibar wenyewe, hamujuwi nyiyi kuwa kila uchaguzi Zanzibar huvamiwa kijeshi na Wakuria ili lengo lenu liwe.
Sisi jawabu ni lile lile Muungano ni batli na n i fake na mukitaka kupima kuwa Wzanzibar hawautaki huu Muungano tokea awali ni smz kupigija kura ya maoni utaona kuwa unatakiwa au laa, sisi tumebanwa tu navibaraka wenu munao wachaguwa Dodoma lakini Ishaallah iko siku tutajigomboa Zanzibar kutoka ktk mkoloni Mweusi, na hivi sasa tayari hata viongozi wetu wa smz wanaanza kushtuka jana Wajumbe wa Baraza la Uwakilishi wamesha towa cheche zao kuwa Muungano huu ni Batli na haukushirikishwa Bunge la Zanzibar wakati huo memba Baraza la mapinduzi (ASP) .
Kwa hio inazihirika wazi kuwa mulituvamia tu kiubabe vipi uskie muungano huu ulikuwa wa watu wawili wapi na wapi?.
Nyiyi mumetukalia kimabavu na ndio ukaona mambo mingi huwa hawashirikishwi Wazanzibar na hata wakishirikiswa basi niwale wasio Wzanzibar ni Wzazibara na tena hutumika mizengwe yahali ya juu.
Jeshi na vifaa vyote vizito vizito vyakijeshi humiminwa Zanzibar mwezi kabla ili kujakufosi mambo yenu yapite, kama sio hivyo basi munatoka kau kwa sababu ridhaa ya Wzanzibar hawataki Muungano huu fake.
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote.
 
[h=1][/h]Written by amini // 17/11/2011 // Habari // No comments

Event_Schedule_Flyer-494x272.jpg
Kanisa lapotowa kwa makusudi historia ,jee lina lengo gani?

Evaristy Masuha
LEO katika kona hii ya Upembuzi wa Kihistoria nimeamua kuandika vile ambavyo wasomaji wamekuwa wakiniuliza.
Kwa hakika maswali hayo ndiyo yameibua hoja hii ya kutaka kujua kama kweli Watanzania wameelimishwa juu ya tukio hili ambalo kwa hivi sasa zinafanya kuwe na shamrashamra kila sehemu.
Wingi wa maswali hayo ndio umenifikisha katika kufanya utafiti wangu wa kienyeji kabisa kupitia vyombo ya habari ikiwa ni pamoja na wataaluma wa vyombo hivi.
Wapo wanaotambulisha tukio hili kama miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, wakati wengine wakiliita miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, wakati wengine wakisema miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Kituko cha mwisho kabisa katika mkanganyo huu ni Pauline Kazana, mmoja wa wafuatiliaji wa kona hii akiwa huko kisiwani Nyamguma, Kibara Bunda aliyewahi kujadiri nami mada hii kwa simu huku akisimama katika kupingana na wale wanaouita uhuru wa Tanzania, wakati yeye anaamini uhuru huu ni wa Tanganyika.
Msimamo wa awali wa Kazana ulisimama katika ukweli kwamba, Tanzania ni zao la muungano wa nchi mbili kati ya iliyokuwa ikiitwa Tanganyika na ile ile ya Zanzibar, tukio lililofanyika Aprili 26 1964.
Kwake yeye kwa vile Tanganyika ndiyo ilipata Uhuru mwaka 1961, basi haikuwa sahihi kusema Uhuru wa Tanzania ambayo ina miaka 47 leo hii tangu mwaka 1964 zilipoungana Tanganyika na Zanzibar.
Ni wazi kwamba kwa muda wote huo Kazana anaamini mawazo na fikra zake, alikuwa hajafuatilia vizuri vyombo vya habari vinavyoripoti tukio hilo.
Hivi karibuni ndio akachanganyikiwa kabisa baada ya kuchunguza vizuri moja ya vipindi vya runinga ambapo bendera moja inaonekana ndani yake kuna neno 50 kuashiria tukio lenyewe.
Kwa mujibu wa maelezo yake ambayo amelazimika kupiga simu akinijulisha juu ya kufuta kauli yake, huku akibaki kinywa wazi pasipo kujua tukio lipi ambalo amekuwa akilishadidia kwa muda mrefu ni pale alipogundua kwamba bendera ile inayoonekana si bendera ya Tanganyika ilipoyapata uhuru mwaka 1961, bali ni bendera ya nchi ya Tanzania iliyoanzishwa baada ya muungano wa nchi mbili.
Anasema kwa uelewa wake, kama tukio lingekuwa ni kumbukumbu ya miaka 50 ya Tanganyika, alitegemea kuiona bendera ya Tanganyika ambayo rangi yake ni kijani kwa juu ikifuatiwa na njano wakati rangi nyeusi inakuwa kubwa zaidi katikati.
Chini yake inafuatia rangi ya njano wakati kijani tena inamalizia kwa chini.
“Bwana mpembuzi, mbona hii bendera ni ya Tanzania na si Tanganyika ambayo nimekuwa nikiamini kwamba ndiyo inabeba tukio lenyewe?” anahoji.
Hilo lilikuwa swali la Kazana huku akiwa amekwama kuelewa kipi ni kipi?
Kwa tathimini hiyo fupi ni kweli kwamba Watanzania hawajui uhalisia wa tukio hili. Wapo wanaoamini kwamba tukio hili ni kumbukumbu ya watu wa bara wakati wengine wakiamini ni tukio la Watanzania wote.
Kwa upande wa historia Watanzania wanaelewa kabisa historia kwamba Tanganyika ilikuwepo siku nyingi hadi Desemba 9, 1961 ilipopata uhuru kutoka kwa Mwingereza.
Baada ya tukio hilo, jirani yake ambao ndiyo iliyokuwa Zanzibar nao wakaendesha mapambano yaliyowafikisha katika uhuru kwa njia ya mapinduzi.
Tukio hili likiwa limefanyika Januari 1964, miezi mitatu baadaye ndipo wakaunganisha nchi hizi na kuipata Tanzania.
Kwa kuitambua historia hiyo ndipo wanapotumia elimu yao hiyo kupiga mahesabu yanayowafikisha katika umri wa miaka 47 tu kwa ile inayoitwa Tanzania, wakati kwa Zanzibar ni miaka hiyohiyo wakati Tanganyika ambayo kwa sasa haipo ndio inakuwa na miaka 50.
Kuna haja ya kuwaelemisha Watanzania kabla ya kilele cha tukio lenyewe.
Tanzania daima
 
Wana JF naomba kuelewa vizuri kwa nini matangazo yasiwe miaka 50 ya iliyokuwa Tanganyika? Mwaka 1961 hakukuwa na nchi inayoitwa Tanzania.
Nawasilisha hoja.
 
Hata ivyo ni tanganyika,TANZANIA aikuwepo mwaka uwo1961 wajinga ndio waliwao
 
[h=1]Zanzibar katu kuwa Dubai au Hongonk kama hatuja jinasuwa na Muungano na wimbi kubwa llingialo Zanzibar .[/h]Written by Hassan10 // 17/11/2011 // Habari // No comments

IMG_25122-564x272.jpg

Hatma ya Z,bar iko mikononi kwenu na ni jukumu na zima mbele ya M/mungu.

Hakuna njia yoyote yakujinasua Z,bar kiuchumi na kimaendeleo kama hatukuondowa utata huu wa Muungano na kuwa taifa huru tukawawacha wenyewe wakashikana machati.
Wazanzibar tusijidanganye kuwa Zanzibar inaweza kuwa Hongong au Dubai ktk harakati za kujinasua ktk kukuza uchumi.
Madamu tumetawaliwa na mamuzi yote tunayo amua nilazima ya ridhiwe na yakubaliwe na upande wa pili ambao Serekali yetu ya smz imejukubalisha kuwa zalili na kupiga magoti na imewapa nguvu zakutuamulia mambo yetu yasio na mipaka , yani yanayo husu Muungano na yasio husu Muungano basi nikazi ya bure Zanzibar kupiga hatuwa za maendeleo.
Tukiangalia jografiki ya visiwa vyetu vya Zanzibar ni visiwa vyenye watu kidogo ukilinganicha na mkoa moja tu wa Bara, sasa kutokana na wimbi la ingia toka na mfumo wa viongozi wetu wa smz wasio ona mbali asari za uingiaji wakiholela eti wanasema Tanzania ni moja unaweza kuishi popote?.
Hii ni hatari na wenzetu wa Bara wana taget zao wanaisabu zao wanapiga na zikitimia basi yale wasio yataka hivi sasa ndio watakayo kuja kuyataka na kuyasimamia badae, yapi ? hivi sasa kupiga kura ya maoni kuwauliza wzanzibar kuhusu Muungano hilo nikosa la jina kwa Serekali ya Muungano nah ii yetu ya smz.
Lakini pindipo wimbi la Watanganyika likisha kuwa jingi Zanzibar na wzanzibar kufunikwa hapo ndipo Watapiga watakapo jikaza kuwa kuwe na kura ya maoni Zanzibar tukitanabahi wapi toolate, itakuwa tumeshafunikwa na tayari tumeshaitupa turuvu yetu (VETO) ya Wzanzibar na wabeba lawama itakuwa ni nani? Ni Serekali yetu ya Smz na Baraza lake la Blw.
Smz muda wakujinasuwa Zanzibar ni huu na uwezo wakufanya hivyo tunao na silaha ipo nikupigiswa kura ya maoni kulizwa wzanzibar kuhusu hatma ya nchi yao ktk Muungano, mukija mukitupa fursa hii viongozi wetu wa smz na Baraza lake Blw basi ndio mutakao kuja kubebe zima ya kizazi cha Wazanzibar .
Viongozi wekeni pembeni maslahi yenu binafsi nay a vyama muekwamue Zanzibar ambayo kila leo inazidi kunamiwa na Jindamizi la Muungano kwa kutumia vitanzi vyake vya katiba, hivi sasa Zanzibar imepoteza nguvu zake na wenzetu wa upande wa pili wanajizihirisha hazarani kuwa lengo lao wote moja kuifuta Zanzibar kuwa nchi.
Na hili linapata Baraka kwa badhi ya viongozi wetu wa smz kujigandisha wenyewe kwa kuwa na unafiki na kutafautiana kwa mitazamo ya uzalendo wengi huchangia kuwa na ubabaishaji mara husema nchi mara sio nchi nchi ni Tanzania.
Mimi hushangazwa na Serekali yetu ya Smz ponapo tokezea jambo kubwa linalo wahusu wzanzibar wote ktk hatma ya nchi yao na kutaka kuonyecha hisia zao zakukerwa basi serekali hii hii yetu ya smz huwakingia kifua na badae kutokana na unafiki hukaa pembeni na kunugunika kuwa Zanzibar haitendewi haki .
Sasa tuwafahamu vipi hawa ? nikwa nini mambo yanayo husu nchi hayaamuliwi na wananchi wenyewe kujuwa hatma ya nchi yao na badae huyavunganyia smz na huku hawayawezi na huku wakinugunika pembeni? Huu ndiwo unafiki walio nao viongozi wetu kujibebesha lawama kwa maslahi yao binafsi.
 
Wana jf naomba tuwekane sawa juu ya hili.Nijuavyo mimi TANZANIA HAIKUWAHI KUPATA UHURU isipokuwa ni zao la Muungano hivyo kwa umri huu TANGANYIKA ndio iliyopata uhuru 1961 sasa ni kwa nini tusiadhimishe miaka ya 50 ya uhuru wa tanganyika?Nahisi ukweli unapotoshwa hapa juu ya historia ya nchi yetu.NAWASILISHA
 
Watanganyika!!!!! mbona hamjibu? au hamjijui au hamlipendi Hilo jina la nchi yenu?.
 
Hapo ndio maana tunahitaji katiba mpya ambayo itatuweka huru na wazi na huu upuuzi wa viongozi wetu kukumbatia mambo yasiyo ya msingi kwa taifa letu.
 
ni mambo ya ajabu sana mkuu historia yetu sijui inapotoshwa kwa maslahi ya nani kuna haja ya kufanya utafiti mpya na kuiandika upya kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo
 
Navyojua 1961 zanzibar haikuwa bado huru na pia Tanzania haikuwepo. Sasa hii ni njia ya kutuibia kupitia maadhimisho ya Mnazi mmoja. Mpaka hawa jamaa waondoke nchi hii itakuwa mabua tu!!. Tunachoadhimisha mimi sikijui kabisa. Kilichopata uhuru ni TAnganyika au TAnzania? Tunaburutwa kila mahala pila mitazamo halisi. Tumekwisha chini ya Mzee wa sherehe na ngoma!!
 
Kuna mtoto wa jirani yangu nilimkuta akijisomea huku akijibu homework zake na kwa mbali niliona swali alilokuwa ameulizwa likiwa hivi,

ni cnhi gani iliyopata uhuru mwaka 1961 kati ya hizi:
(a) zambia
(b) tanzania
(c) uganda ( )
(d) ghana


jambo la ajabu dogo aliweka jibu la ''b'' kwenye mabano na mwalimu akamuwekea tiki. Kizazi kinapotoshwa.
 
Watanganyika!!!!! mbona hamjibu? au hamjijui au hamlipendi Hilo jina la nchi yenu?.

Ndio Mkuu. Naona hili jina hawalitaki, au sijui wanaliogopa. Duh Watanganyika mpoooooo!!!
 
kiukweli maadhmisho ni miaka 50 ya tanganyka na c tz.ndio hapo huo namkumbuka jamaa anaitwa c.mtikila na sela zake za utanganyka na kisha nakumbuka mhe. njelu k.na G55 ndani ya bunge la j ya muungno tz.YAANI WEE ACHA TU!!
 
HODI HODI wanajamvini.....
Nadhan sisi si wageni wa msemo wa taifa hili hasa katika ule wa miaka 50 ya tanzania..napata waswas kulingana na historia ya nchi hii kama nlivyofundishwa yaaani:
Tanzania ni zao la tanganyika na zanzibar..tanganyika ilikua huru mwaka 1961 na zanzibar 1963..tanzania ikafata mwaka uliofata yaan 1964,katka hesabu rahisi ni kua toka 1964 mpaka 2011 yaan mwaka huu kuna miaka 47 ya tanzania na miaka 50 ya tanganyika ambayo inafika kilele disemba 09..tatizo linakuja hiyo miaka 50 ambayo inaelezwa na serikali hii kama miak 50 ya tanzania inakuja vp?mbona zanzibar cjawackia wakisema hiki kitu..NADHAN SERIKALI IWEKE WAZI HILI SWALA KUA NI MIAKA 50 YA KIFO CHA TANZANIA
 
Daima ukijidharau usitegemee mwingine akuheshimu, na ukisema ukweli unaonekana mbaya kisa umeenda kinyume na mwalimu malimu hakuwa munguna hii dunia inabadilika, wakati wanaungana Zanzibar hata bendera iliwekwa kapuni, kama sisi tulivyoeka ya Tanganyika, hivi majuzi wamedai na wamepewa bendera yao! sasa kule inapepea bendera ya Zanzibar na ya Muungano, wakafikiri wakasema hapana hii bendera ya muungano sio ya kwetu ni ya watanganyika na sisi tumgeuzwa koloni hatutaki, choko choko zikaanza mbya zaidi walipoona mgombea wa urais Zanziba kupitia CCM anachaguliwa Dodoma, kuna kerokero nyingi lakini zote zinakuja baada ya sisi wa bara kuifuta Tanganyika, USA zimeungana nchi hamsini na mbili lakini kila nchi ina haki yake na kila nchi ina utambulisho wake japo kuwa sio kimataifa, hivyo USA kuna serikari 52 + Serikali ya Umoja = 53
 
Kwa muda sasa mie Mkweche najiuliza bila majawabu!Hivi kwanini Tanganyika na mipaka yake ilizama kabisa!
Mbona wenzetu Tulioungana nao likija swala la Zanzibar si Nchi wanang'aka sana!Nakumbuka yaliyomkuta Mh.pinda siku zile na alikosa mtetezi!Wao wakakomelea msumari kwa kurekebisha Katiba yao!
Lakini likija swala la Tanganyika ni Nchi sisi watanganyika tunang'aka Muungano utakufa!
Hivi ni kweli Sumu ya Muungano ni kuwa na serikali ya Tanganyika!
Kichwa kimepata Moto waungwana mnisaidieeee!
Mkweche nimepotea kabisa!
Ila Napenda Tanganyika pia kama Zanzibar ni Nchi!Hapo dhana ya TZ bara na TZ visiwani itakuwa Hai!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom