Nchi ya Qatar yaishinikiza Tanzania kuitambua serikali mpya Libya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi ya Qatar yaishinikiza Tanzania kuitambua serikali mpya Libya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Nov 26, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katika pitapita zangu mitaani kwenye mitandao ya habari nimekutana na habari hii. Je kuna ukweli au ni suala linalowahusu wachache?

  Nchi ya Qatar imezuia visa kwa Watanzania,baada ya Serikali ya Tanzania kumsupport Muamar Gaddafi na Kutoitambua Serikali mpa ya Libya. Hii ilionyesha wazi wakati raia wa Watanzania wanaoishi nchini Qatar walipojaribu kuwaombea visa familiya zao walioko huko tanzania. Wananchi hao watanzania waliambiwa kua nchi yenu imezuiwa na haipewi visa. hii ni karibu ya miezi sita sasa toka nchi hio isimamishe viza hizo kwa tanzania lakini hakuna ishara au ufuatiliaji wowote ule uliochukuliwa na Serikali hio ya Tanzania kuweza kutatua tatizo hili.Qatar ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi na nchi ambayo inahitaji wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali duniani, Qatar tayari huko nyuma ilishakubaliana na Tanzania kuweza kuchukua wafanyakazi kutoka tanzania lakini kwa saga hili lililotokea inaonyesha Qatar itasimamisha kuchukua wafanyakazi kutoka huko na kuchukua wafanyakazi kutoka kenya na nchi nyengine dunini.  Mdau
  Sahim Khatib
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Siwapendi hao Qatar ni basi tu,siwapendi watu wanafiki!

  If it was my call hata uhusiano nao ningeuvunjilia mbali!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kumbe nao wana mizengwe utoaji wa visa?
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mbopo yuko wapi?

  website ya foreign inasemaje kuhusu
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  tanzania siwaelewi. wanaleta mambo ya kulipizana visasi?
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hao Qatar/na serikali mpya ya libya wanacheji? kama tulio kuwa tunapata toka kwa Ghadaffi
   
 7. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi ya Qatar ni ghali hata kuishinda USA kuishi. Je tukiwaamrisha wasivae kanzu na hijabu watatufanyaje kwani?
   
 8. S

  Sheba JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Taarifa hii haijakamilika. Nenda ukatafute vizuri sababu za ndugu zako kunyimwa viza. Kwanza unatakiwa kuweka wazi ni aina gani ya viza wameomba, je ni ya ukaazi na kufanya kazi au ya utalii. Haiingii akilini kwa Qatar kuzuia viza kwa watanzania kutokana na msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu Libya au Ghaddafi. Haiwezekani zaidi kuwa Kenya yenyewe ikubaliwe. Kenya kama Tanzania haijaitambua NTC. Lakini, nenda mbali zaidi ujiulize, mbona Qatar Air inakuja Tanzania tena mara mbili kwa siku? Je, viza kwa wasafiri hao wanatoa wapi? Maana sisi wenzako ambao tumewahi kwenda Qatar tunafahamu fika kuwa viza zao hutolewa kupitia airline yao. Utaratibu huo hutumika pia na UAE. Na kwa vyovyote vile uamuzi huo ungefanyika lazima Serikali yetu ingejulishwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na tamko la aina hiyo lingemaanisha kuwa ni tamko la kuvunja uhusiano wa kidiplomasia.
   
 9. S

  STIDE JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mr. Candid, nadhani ili litakuwa ni suala la wachache, maana hivi ninavoandika niko Qatar, binafsi nina zaidi ya mda ulotaja lakini pia kuna jamaa zangu watatu wamekuja hapa Qatar, mmoja ana miezi 3 na wawili wana wiki 2 na siku 4!!
  Na wakati nashughulikia Visa zao sikuona wala kuhisi tatizo lolote!! Sihafiki unachokiongelea mkuu.
  "MUNGU IBARIKI TANZANIA"
   
Loading...