Juzi Alhamisi nimeshuhudia mwenyewe. Mwanzoni nilikuwa siamini nikijua ni siasa tu, nikiwa katikati ya Jiji la Kampala wakati wa lunch time ktk mgahawa mmoja nilikutana na Wafanyabiashara watatu Watanzania. Nilikuwa nimekaa meza ya jirani na wao, niliposikia Kiswahili chao fasaha nikagundua hawa ni ndugu zangu wa Home, nikasogea tukakaa pamoja, hapo ndipo Mazungumzo yakaanza.
Ktk maongezi kila mmoja wetu alijitambulisha ni nani na amefata nini Kampala, wao walisema kuna bidhaa huwa wanazichukua Kampala na kuzipeleka Tanzania. Aina ya bidhaa sitazitaja. Lakini ni bidhaa hizi hizi za kawaida zinazotoka China na Zimepitia bandari ya Dar kuja Kampala. Nilijaribu kuwadadisi ya kwamba kwanini wasinunue Dar wakati pia zipo, walijibu bei ni kubwa sana na haiwezi kuwalipa.
Tuliongea mengi sana. Lakini nilichogundua ni kwamba, aidha kuna mkakati wa Makusudi wa baadhi ya watendaji wa TRA wa kuhakikisha kwamba hakuna mfanyabiashara wa Tanzania atakayefanikiwa kibiashara. Kwa sababu haiwezekani Bidhaa inayotoka China kupitia bandari yetu halafu iuzwe kwa bei ya chini Kampala kuliko Dar.halafu wafanyabiashara wetu waifate Kampala na kuirudisha Dar na waiuze Dar na kupata faida kuliko Yule Mtanzania aliyenunua bidhaa hiyo hiyo China na akaipitisha bandarini dar na akaiuza Dar.
Madhara yanayosababishwa na Hawa Majini TRA ni makubwa sana tofauti na wenye akili ndogo wanavyofikiria. Nitayataja baadhi.
1 Wafanyabiashara majirani zetu ambao hawana bandari wamekoma kuja Tanzania
1 Wafanyabiasha wetu haswa wa Soko letu kubwa la Kimataifa k,koo wako hoi kiuchumi
3 Wenye Mahotel ambao target Yao ilikuwa ni kuwapokea wageni kutoka Zaire, Malawi, Zambia,
Burundi, Rwanda, lazima watafilisika kwa kukosa wateja.
4 Wenye Restaurant wengi watafunga kwa kukosa wateja. Na hivyo wafanyakazi wengi
Watapoteza ajira.
5 Wabeba mizigo Ajira zao zitakufa rasmi hawa ni kuanzia wale Vibega, matoroli, bajaji, kirikuu, Canter
Fuso malori nk, hii cheni ni kubwa
6 Mama lishe biashara sitadoda.
7 TRA wenyewe hawatoweza kukusanya tena kodi kwa sababu biashara wameua wenyewe.
Maoni yangu,
Pamoja na Raisi kukaa na wafanyabiashara wachache, pia ni lazima TRA wenyewe wakae na Wafanyabiashara haswa wale wanao import bidhaa toka Nchi mbali mbali Duniani. Ili kupanga namna na viwango bora vya kulipa kodi.
TRA ni lazima iwe inawapeleka baadhi ya wafanyakazi wake nje kujifunza ktk Nchi Kama Dubai , Hong Kong, China Uganda South Africa, kuona wao wamewezaje kufanikiwa ktk Suala la kodi kwa kiasi hicho na Kufanya hizo Nchi Wafanyabiashara wakawa na furaha.