Nchi Kwanza, Chama baadae - Nape Nnauye

Nchi Kwanza, Chama baadae - Nape Nnauye

Nape aache unafiki. Posho ni sera ya CCM, ilitetewa na Pinda, inasainiwa na JK-mwenyekiti wa CCM, inajadiliwa na kupigiwa kura na wabunge wa CCM, ni mpango mzima wa chama kuwaongezea wabunge wa CCM mapato kwani ruzuku imepungua. Ni rushwa kwa wabunge ili kuwapumbaza. Ni ulafi na kukosa busara.
 
Kwa kweli hii sio kweli kwa yeye kuwa na iyo nafasi aliyonayo ingetosha kabisa kuelimisha na kushauri wabunge wa chama chake wawe na kauli moja ya kukataa au kuzikubali hizo posho ila wamekuwa kila mmoja anaongea lake.ok kwangu mimi naona hayo ni matukio yanayotufanya tuwe bize kwa muda kuyajadili illi cku ziende.

Tatizo sisi watanzania/wazanzibar/watanganyika huwa tunapiga kelele ila hatuna focus, ilikuja ishu ya mishahara ya wabunge kutokatwa kodi tukapiga kelele,ikaja issue ya kupewa millioni 90 tunapiga kelele,ikaja isssue ya dowans, ikaja ya nishati na madini, ikaja ya wanyamapori kelele zikapigwa na hili la posho kelele zitapigwa then maisha yataendelea kila cku

my take. ifike sehemu tutafute suluhisho la haya matatizo na sio kupiga kelele mara kwa mara

Duu! Kiukweli umenigusa mkuu, ndio maana saa nyingine huwa nasoma watu wanavyobwabwaja tuu bila conclusion.
 
Kauli ya 'nchi kwanza chama baadaye' itapendeza sana ikitumika ktk swala la mswada wa katiba mpya,
Hii namaanisha kuwa, yale madaraka makubwa ya rais wanayoyalilia wabunge wa CCM yapingwe kwenye katiba mpya na wazalendo wote kwa kuongozwa na na iyo kauli ya 'nchi kwanza, chama baadaye'.
Tofauti na hapo, hizi copy and paste za hoja mnazofanya(nape na wengine wengi) kwa nia ya kutafuta publicity zinawachoresha sana na mwisho wa siku inajidhihirisha mvuto wa kisiasa umepotea.
 
NAPE: NCHI KWANZA CHAMA BAADAYE (HABARI NDANI YA GAZETI LA RAIA MWEMA)

MADA: EDUCATION IN TANZANIA , NAPE NNAUYE , RAIA MWEMA , UFISADI , UVCCM

Chama cha siasa huzaliwa,hukua na kinaweza kufa pengine hata kabla hakijakua.Tofauti nachama nchi ikishazaliwa ni lazima iishi milele,tena kwa gharama yoyote ile.Lakini kuna wenzetu wengine hawataki kuelewa ukweli huo.

Kwao,chama cha siasa ni kila kitu hata kama kinaipeleka nchi ahera. Angalia mfano huu mwepesi: chama kinapewa dhamana ya kuongoza nchi, lakini kinaendesha mambo yake kihuni na kupeleka nchi mrama.Ni dhahiri kwamba chama cha aina hiyo kinaamsha vurugu ambazo zitalekea mmomonyoko wa amani katika nchi husika.

Kwa bahati mbaya au makusudi,kuna wenzetu hawataki kuamini kwamba ni vigumu kujenga na kudumisha amani kuliko kuivunja.Sote tunawajibika kuhakikisha nchi yetu haipelekwi kusikofaa badala ya kunyoosheana vidole tunapotofautiana namna ya kuboresha ustawi wa Tanzania yetu.

Katika toleo la wiki hii la gazeti mahiri la Raia Mwema,pamoja na mkusanyiko wa habari na makala motomoto,kuna hababari kuhusu the man of the moment,Nape Nnauye.Kuna wanaodai kuwa huyu jamaa aanashupalia ishu za ufisadi ndani ya UVCCM kwa minajili ya kutafuta umaarufu utakaopelekea apate nafasi ya juu kwenye jumuiya hiyo.

Sina uhakika kuhusu hilo lakini binafsi naamini kwamba hata kama malengo yake ya ni kupata umaarufu au uongozi,jitihada zake kuushikia bango ufisadi ndilo lililo muhimu zaidi kuliko motives zake.

Na wanaokemea ufisadi,hata kama kwa njia zisizo sahihi,wanapaswa kuungwa mkono badala ya kunyanyaswa.Enewei,habari ya Nape ni hii HAPA na mambo mengine motomoto yanapatikana ndani ya gazeti hili la RAIA MWEMA.

HUU NI UTHIBITISHO HAJAANZA LEO NAPE, WANAOPINGA WANA YAO!!!!!

"NAPE KIGEUGEU"

Ni kweli tunaopinga haya tuna yetu,kama yafuatayo..

1:Suala la posho lilipotolewa na CDM ,ilikuaje?Si ni CCM yote pamoja na wabunge wao na akina NAPE waliowaponda CDM na kuwapa maneno ya kejeli eti,wanazitaka,visebusebu ,mara hoo ni ndumiila kuwili,wao ndio waliojenga hiyo hali ya wabunge wao kujiongezea posho kila wanapotaka.sasa saa hizi wabunge wanataka zaidi,haohao wanajifanya mashujaa wa kuzipinga.Hili nafikiri ukweli waliujua ila wakaufumbia macho kwa sababu tu,ilitoka CDM.Na pia kwa CCM walivyo wajanja wanaweza kuwa wamelipika hili halafu baadae waibuke mashujaa kuwa wameazuia wabunge kuongeza posho,na wananchi tulivyo wapuuzi tutawaunga mkono.

2:NAPE aliwaambia wananchi wa mwanza atawashikisha "UKUTA".sasa sie tumkubali awe kiongozi wetu ili aje kutushikisha ukuta?Wengine hatukulelewa hivyo.Inaelekea hako kamchezo kako kwenye chama chao,Na ndio maana Cameroun alipowashtukia akasema wahalalishe vinginevyo hatatoa misaada ,eti wanakuja Public na kupinga uonevu wa waingereza,kumbe ndo kamchezo kao kwenye chama chao,kakushikishana UKUTA.

3.Lakini pia si alituambia anawavua watu magamba na kuwataja na majina,na alikomelea msumari kule mbeya na kina Sitta.Alipoona mafisadi wanakuja juu,kabla ya NEC akaanza kutuambia oooh,maazimio ya NEC yako mengi anashangaa kuona watu wanang'ang'ania kipengele kimoja sijui cha ishirini na ngapi vile/kama ndio hicho pekee kinachokwenda kujadiliwa.Alivyotoka NEC akatuambia tulimnukuu vibaya,ooh..sikusema hivyo.sasa unataka sisi tuwasikilize viongozi waongo?

4.Hivi kwa nini NAPE anajichubua,au ndio dalili za hako kamchezo kao ka kushikishana "UKUTA" Sasa mie nimchague awe kiongozi wangu, watoto wangu atawafundisha nini?kujichubua na kushikishana "UKUTA'?Hell no..

5.Nikweli nakubaliana nae anaposema "nchi kwanza" kwa asilimia 100 kwani yeye anachojali ni NCHI ambayo ina utajiri wa mkubwa.Ningekua mimi ningesema "wananchi kwanza".kwani ndio wanaoteseka na huu ufisadi unaowamaliza ilhali wakijaribu kulitumikia taifa hili.Ukitaka kulijua hili baada ya kupewa ukuu wa wilaya alitulia tuli,,sasa saa hizi alivyoona hakuna ulaji anatafuta pa kutokea apewe zaidi.

Kiufupi narudia na ntarudia NAPE ni "MNAFIKI" na mbaya zaidi ni sawa na kale ka wimbo ni"KIGEUGEU"
 
Tukumbushane jinsi Nape alivyoikana Jamii Forums baada ya uchaguzi wa Igunga. Mtu wa namna hiyo anaweza kuikana fesbuk wakati wowote. Kwa kifupi Nape haaminiki, yeye anafuata mambo yanayomfurahisha Baba Riziwani ili aendelee kuishi mjini
 
duh hii kali ya kuwashikisha watu "UKUTA" hahahhah nimecheka mpaka basi Bongo politics bana wee acha tu
 
Hapo ni baada ya kuona kumbe wenzie wanapiga ngoma hivi na kucheza vile....alidhani wanakwenda kwa bit!!
 
kama kakiuka miiko ya chama hivi mana CHAM KWANZA WANANCHI BAADAE
 
mlikuwa mnataka nape afanye nini? akubali hizi posho ili muendelee kumshambulia?
 
Cheichei2010,
POLE SANA KAMANDA, NILIJUA UMESHASAHAU ALIKUSHIKISHA UKUTA PALE KWENU NYUMA YA NYUMBA, KUMBE BADO UNAKUMBUKAA DUH!!!.. SASA SIJUI ULINOGEWA NA MCHEZO AKAKUMWAGA NDO MAANA UNA HASIRA AU ALIKU OVERDOSE NDO MAANA UNAWEWESEKA... TUPASHE TAFADHALI, NA KALE KAWIMBO KA CHEICHEIIIIIIIIIIIIIII EEHH MAMA!
 
Nape ni mnafiki tu, hana lolote. Always maneno yake huwa hayaendani na matendo yake. Kama mtizamo wake ni nchi kwanza na si chama kwanza, mbona huwa hasimami kutetea interest za nchi na kupingana na mwenyekiti wake wa Chama ambaye anaonekana kuivuruga na kuiharibu nchi yetu? Magamba wote mtizamo na mawazo yao ni mamoja tu. Hatuweza kutarajia kuchuma zabibu kutoka kwenye miiba, wala hatutarajii matendo mema kutoka kwa mbwa mwitu. CCM wote ni mbwa mwitu tu, hatutarajii zuri na lenye maslahi ya taifa kutoka kwao. Wao wanawaza kujineemesha tu hawawezi kupoteza muda kuifikiria nchi.
 
Slogan ni nzuri tatizo haifuatwi na wabunge wake mf
  • Walikuwa wa kwanza kutetea Posho ilihali wanajua hali halisi ya nchi hii
  • Walimzuia Ris kukutana na ujumbe wa CDM ilihali walijua kuwa ziara lie ilikuwa kwa maslahi ya nchi kama si busara za Rais angewatii
  • waliacha kuujadili mswada Waka base kijadili CDM na LISSU huku wakitetea chama badala ya taifa letu
  • etc
 
Maggid, kwani kuongeza posho ni maamuzi ya chama? tuwe makini kidogo wabunge wale wa tume ya bunge ni watu huru wenyewe, sio hata kamati ya bunge ya chama, at least hapo ungeunganisha na chama.

Hivyo mimi naona Kauli ya Nape ni ya Chama na ya wabunge ni ya wabunge.

Msimamo wa CCM kwenye suala zima la posho (hata kabla ya uongezwa) unafahamika. Ukiacha mwanasheria mkuu na wakuu wa mikoa, wabunge wengine wameingia bungeni kwa ticket za vyama vyao.

Spika wa bunge ni mojawapo wa viongozi wa CCM kama mjumbe wa kamati kuu.

CCM sio one or two or three men party, bali misimamo na maamuzi ya CCM ni makubaliano halali ya vyombo vya uongozi vya CCM ambavyo members wengi ni wabunge.

Hakuna mbunge hata mmoja wa CCM asiyeunga mkono ongezeko la posho.

Conclude mwenyewe...

@Nape... Hivi sio wewe uliyesema hii nchi ina wenyewe, na wenyewe ni CCM? Inakuwaje unasema Nchi kwanza, chama baadae, wakati nchi hiyo ulishasema inamilikiwa na chama??!
 
Kauli ni nzuri sana kama akiishi ila kwa desturi za wanaccm ni wazuri wa kutoa kauli pasipo matendo hapo ndo nachelea kutokuamini alichokisema ndugu yetu Nape.
 
Cheichei2010,
POLE SANA KAMANDA, NILIJUA UMESHASAHAU ALIKUSHIKISHA UKUTA PALE KWENU NYUMA YA NYUMBA, KUMBE BADO UNAKUMBUKAA DUH!!!.. SASA SIJUI ULINOGEWA NA MCHEZO AKAKUMWAGA NDO MAANA UNA HASIRA AU ALIKU OVERDOSE NDO MAANA UNAWEWESEKA... TUPASHE TAFADHALI, NA KALE KAWIMBO KA CHEICHEIIIIIIIIIIIIIII EEHH MAMA!
Na kwa jinsi unavyoandika kwa capital letters inajidhihirisha wewe ni nani.

Unajua physics, chemistry, math . biology...... zote ni sayansi, na formulas huwa derived from principles. In short my brother, conclussions can be made from a trend (which make principles).

Ungeweka picha yako ile uliyovaa cheni na lipstick.
 
Back
Top Bottom