Nchi Kwanza, Chama baadae - Nape Nnauye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi Kwanza, Chama baadae - Nape Nnauye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Dec 14, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  "Nchi Kwanza, Chama Baadae"- Nalipelile 'Nape' Moses Nnauye. Jumatano, Novemba 14, 2011.

  Ndugu yangu Nape,

  Nadhani jina lako ni kifupi cha Nalipelile, utanisahihisha kama nimekosea. Hakika, kauli yako hiyo ni nzito sana. Kauli uliyoitoa leo kwenye ukumbi wa facebook. Yumkini kauli hiyo itakutoa kutoka kwenye tope ulilonasa, if you will walk your talk. Maana, mwanadamu anayeyejaribu kumtoa mwanadamu mwenzie kwenye tope alilonasa, naye yumo kwenye hatari ya kunasa topeni. Juhudi ya kwanza ya kujinasua kwenye tope yapaswa ifanywe na aliyenasa topeni.

  Maggid Mjengwa, Iringa.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hili namuunga mkono,
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Maggid, kwani kuongeza posho ni maamuzi ya chama? tuwe makini kidogo wabunge wale wa tume ya bunge ni watu huru wenyewe, sio hata kamati ya bunge ya chama, at least hapo ungeunganisha na chama.

  Hivyo mimi naona Kauli ya Nape ni ya Chama na ya wabunge ni ya wabunge.
   
 4. m

  mob JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hii sio kweli kwa yeye kuwa na iyo nafasi aliyonayo ingetosha kabisa kuelimisha na kushauri wabunge wa chama chake wawe na kauli moja ya kukataa au kuzikubali hizo posho ila wamekuwa kila mmoja anaongea lake.ok kwangu mimi naona hayo ni matukio yanayotufanya tuwe bize kwa muda kuyajadili illi cku ziende.

  Tatizo sisi watanzania/wazanzibar/watanganyika huwa tunapiga kelele ila hatuna focus, ilikuja ishu ya mishahara ya wabunge kutokatwa kodi tukapiga kelele,ikaja issue ya kupewa millioni 90 tunapiga kelele,ikaja isssue ya dowans, ikaja ya nishati na madini, ikaja ya wanyamapori kelele zikapigwa na hili la posho kelele zitapigwa then maisha yataendelea kila cku

  my take. ifike sehemu tutafute suluhisho la haya matatizo na sio kupiga kelele mara kwa mara
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kama huzifahamu siasa za CCM na viongozi wake ndio utasifia matamko ya akina Nape na wenzake.....siasa za Tanzania hazijatoa mipaka ya utendaji wa chama na serikali...kwasababu ya hili tatizo,mara nyingi chama kina msukumo mkubwa sana kwa maamuzi ya serikali....mfano juzi NEC ilimpa agizo JK akutane na vyama vya siasa kuhusu kujadili mswada wa marekebisho ya katiba.

  Kwa hali hii uwezi niambi kuwa posho za wabunge CCM walikuwa hawajui,wakati kwa hakika mambo mengi yanayoendesha nchi hii CCM wanayajua......
   
 6. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kauli YES...Nape NOOOOOoooooo, Kwa sababu ni walewale hawaishi kubadilika rangi
   
 7. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  safi!!!!na ndio maana nikasema ndugu mwenyekiti kafulia!!!yeye kazi yake siku hizi ni kukurupuka tu!!!!!!aende vacation Sweden atakuja na mawazo onyevu!!!
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hivi mnaelewa maana ya neno PROPAGANDA? Lilianzia wapi na nani walikuwa wanalitumia sana?

  Asanteni
   
 9. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wether haya maneno yanatoka moyoni au la, nchi yetu imeshagawanyika na mgawanyiko huu hautokani na hoja. Kuna watu wapo tayari kumkashifu mtu anayepinga posho, simply because wabunge wao wamekuwa wakipokea posho.
  Mwanasiasa yeyote aki reach out for support, watu wanamtukana.

  Lakini Nape, inabidi ujifunze kuheshimu tofauti kati yetu na wana CDM, umewatukana matusi ya nguoni Mwanza na unapenda kutumia kebehi kama signature yako unapofanya kazi yako ya uenezi. Sasa chochote utakachosema sidhani kama utapata support kutoka upinzani hasa CDM.

  Kuhusu Zitto, nakuonea huruma sana ndugu yangu.Kwa namna moja au nyingine huko ulipo hawakupi support unayotaka, na wala hakuna kiongozi aliye balance intelligence/diplomacy na militancy/radicalism.

  Vyama vyote vikuu sasa hivi vimeoza, havina points. Wezi watupu wamejazana.
   
 10. N

  Nipe tano Senior Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAPE: NCHI KWANZA CHAMA BAADAYE (HABARI NDANI YA GAZETI LA RAIA MWEMA)

  MADA: EDUCATION IN TANZANIA , NAPE NNAUYE , RAIA MWEMA , UFISADI , UVCCM

  Chama cha siasa huzaliwa,hukua na kinaweza kufa pengine hata kabla hakijakua.Tofauti nachama nchi ikishazaliwa ni lazima iishi milele,tena kwa gharama yoyote ile.Lakini kuna wenzetu wengine hawataki kuelewa ukweli huo.

  Kwao,chama cha siasa ni kila kitu hata kama kinaipeleka nchi ahera. Angalia mfano huu mwepesi: chama kinapewa dhamana ya kuongoza nchi, lakini kinaendesha mambo yake kihuni na kupeleka nchi mrama.Ni dhahiri kwamba chama cha aina hiyo kinaamsha vurugu ambazo zitalekea mmomonyoko wa amani katika nchi husika.

  Kwa bahati mbaya au makusudi,kuna wenzetu hawataki kuamini kwamba ni vigumu kujenga na kudumisha amani kuliko kuivunja.Sote tunawajibika kuhakikisha nchi yetu haipelekwi kusikofaa badala ya kunyoosheana vidole tunapotofautiana namna ya kuboresha ustawi wa Tanzania yetu.

  Katika toleo la wiki hii la gazeti mahiri la Raia Mwema,pamoja na mkusanyiko wa habari na makala motomoto,kuna hababari kuhusu the man of the moment,Nape Nnauye.Kuna wanaodai kuwa huyu jamaa aanashupalia ishu za ufisadi ndani ya UVCCM kwa minajili ya kutafuta umaarufu utakaopelekea apate nafasi ya juu kwenye jumuiya hiyo.

  Sina uhakika kuhusu hilo lakini binafsi naamini kwamba hata kama malengo yake ya ni kupata umaarufu au uongozi,jitihada zake kuushikia bango ufisadi ndilo lililo muhimu zaidi kuliko motives zake.

  Na wanaokemea ufisadi,hata kama kwa njia zisizo sahihi,wanapaswa kuungwa mkono badala ya kunyanyaswa.Enewei,habari ya Nape ni hii HAPA na mambo mengine motomoto yanapatikana ndani ya gazeti hili la RAIA MWEMA.

  HUU NI UTHIBITISHO HAJAANZA LEO NAPE, WANAOPINGA WANA YAO!!!!!
   
 11. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo zitto atoke huko alipo aende Red Cross???
  Si umesema vyama vyote vimeoza!!!
  Yale yale ya ushabiki wa watu. Unajua swala la posho lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya cdm?? Unajua kwamba sio ajenda binafsi ya Zitto??

  Nafikiri wewe unahitaji kutoka huko ulipo uende cuf ya akina mnyaa, sio ya mtatiro.
   
 12. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  karibu sana Nipe tano...........i mean Nape.
   
 13. N

  Nipe tano Senior Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soby,
  Katika watu wanasikitisha wewe unaongoza. Hivi hata kwa mambo ya msingi we akili zako ki masaburi tu??? Hivi katika wazelondo wa nchi hawa vijana wawili hawamo?? Iko kazi na tatzo la wengi nchini ni kuunga mkono watu kwasababu ya makundi yao a wanapata mkate basi,kuna jema gani wangefanya hawa kwako lingekufur,ahisaha?? Shame na sitaarabika
   
 14. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kitendawili..........Tegaaaaa..........
   
 15. N

  Nipe tano Senior Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ooooh, HIVU ULISHACHKUA LILE TOY LAKO AU BADO, MAANA HIZO AKILI ZAKO NI ZAKUYUMIA KICHWA CHA CHINI AMBACHO CHAKO HUFANYA KAZI VIZURI UKIKISAFISHA NA TOY, PLS KASAFISHE KWANZA
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ilani?.... mbona wabunge wenu wanachukua posho? Au hawachukui?

  Mbna mshahara wa Dr. Slaa ulikuwa haukatwi kodi?

  Hebu niondolee upuuzi wako hapa!!
   
 17. Mwamikili

  Mwamikili JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35  Anatafuta pa kutokea, ukiangalia watu wote kwenye facebook wamejaribu kumweleza na kumpa points, ndio maana nae akacomment hivyo bali alikuwa akimpongeza zitto so ni propaganda tu hizo na nafananisha na wimbo wa bwana misosi nitoke vipi!!
   
 18. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuwa mzalendo peke yake hakutoshi. Mmmoja wao amezidi kebehi na matusi.

  Mwingne anapendwa anapoanza kususa na kuacha kuongea na mtu yeyote kutoka CCM, na anaona watanzania ni wajinga kwa kutokusaini EAC inayompa ardhi raia yeyote wa nc yewyote iliyo kwenye jumuia, pamoja na suala la ulinzi.

  Kwa kifupi wote ni wapayukaji tu hawana maana yeyote.
   
 19. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Watu wengine hapa sijui wanafikiri je. Eti hii ni kauli nzito .Is it? Si kila mtu anasimamia hilo au NAPE ndio icon ya uzalendo. Even a fool can say that. So long as his is another gamba , he can go to hell .
   
 20. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Nape sialikuwa anasema Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM. Yeye ndio alikuwa anajua leo nchi kwanza vyama baadaye? Aende akwaambie wachumia tumbo wa ccm kule Dodoma. [​IMG]
   
Loading...