Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Heparin

JF-Expert Member
Sep 24, 2021
203
880
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba radhi wananchi na wapenda demokrasia nchini kutokana na kauli aliyoitoa kuwa si lazima CCM ishinde kura kwenye boksi, bali kuna njia nyingine zikiwemo alizosema za haramu.

Akizungumza kupitia video aliyorekodi, leo Jumatano Julai 17, 2024 Nape ameomba radhi wote walikerwa na kauli yake.

“Nimeuona mjadala kwenye mitandao, lakini kama nilivyosema kauli ile ilikuwa utani lakini naona umekuwa mjadala mrefu wakati huu kwa sababu tunaelekea katikia uchaguzi. Nawapa pole ambao wamesumbuliwa na kuteseka na huu mjadala, nawapa pole na naomba radhi, nasisitiza haikuwa serious,”amesema Nape.

Nape aliyewahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, alitoa kauli hiyo iliyoibua mjadala juzi Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi.

Muktadha wa kauli hiyo ilikuwa ni kuwahakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025, Nape ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema:

“Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi tu mkishamaliza, unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea,” alisema.

Kauli hiyo ya Nape, ilipingwa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ambaye alisema kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.

“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” alisema Makalla.

Hii si mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli tata zenye kuzua mjadala katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, hata Juni 2015, akiwa ziarani Sengerema alisema “CCM ingeshinda uchaguzi mwaka huo hata kwa bao la mkono.”

Pia soma
  1. Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
  2. Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
  3. Kauli ya January Makamba ''hata kama hatumkubali Samia ni wetu'', ina maana gani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
 
Mods namba Moja mngeanza kutukumbusha thread ya bao la mkono
 
Back
Top Bottom