Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,767
Inasikitisha Sana kwamba vijana wetu wanajitahidi kimasomo katika mazingira magumu Sana. Wakati mwingine fedha za mikopo ya kujikimu inachelewa, na hata wengine hawapati kabisa. Licha ya magumu yote hayo, unakuta kijana amejitahidi Hadi kufikia hatua ya juu ya ufaulu.
Wengine katika madaraja yanayofikia hadi GPA 4.2 na zaidi kwenye fani mbali mbali. Cha kushangaza ni kuwa serikali ambayo ndiye mwajiri na mlezi mkuu wa watu wake, Haina utaratibu wowote wa kuhakikisha hawa WALIOFANYA VIZURI wanaendelea na MASOMO ya juu zaidi kwa kuwapatia scholarship, au kuwaingiza katika programu inyowawezesha kujiendeleza zaidi. Hapa nawazungumzia vijana wanaohitimu Stashahada na Shahada ya kwanza.
Nchi yenye uwezo wa kununua midege kwa fedha taslimu, inashindwaje kuwawekea vijana wake utaratibu wa ajira au kuwandeleza kielimu wale WALIOFANYA VIZURI kwa viwango vya juu!? Tunawatelekeza bila kujali kwamba vijana hawa walikuwa wakikesha kuhakikisha wanapata ALAMA za juu wakiamini taifa lao litaziona juhudi zao.
Nimejaribu kuwasiliana na wakufunzi wa vyuo vikuu kadhaa ambao kwa masikitiko wamelalamika kuwa siku hizi wamefungwa mikono kwa kutoruhusiwa kuwachukua baadhi ya vijana wanaofanya vizuri ili wajiendeleze vyuoni kuja kujaza nafasi za kufundisha katika vyuo hivyo. Kwamba serikali haina mpango wa kujenga think tank ya Tanzania ni jambo la kusikitisha sana.
Ni wito wangu kwa wahusika, Mhe. Rais pamoja na wizara ya elimu ya juu, wizara ya utumishi, na tamisemi kukaa chini na kuliangalia jambo hili kwa jicho la pili.
"Mcheza kwao hutuzwa" ni msemo wa kiswahili wenye maana ya kuwazawadia mema wale wanaofanya mambo kwa uzuri. Sisi Tanzania tunajenga jamii ya aina gani ambayo hata yule anayefanya jitihada na kufanikiwa anakuwa hatambuliwi!
Serikali ifikirie kujenga watu zaidi kwa kuwajali hasa wale wanaofanya vizuri kwenye MASOMO. Haiwezekani vilaza na vipanga wote wawe "maji ga nyanza" eti kwa vile serikali inajali ndege na magorofa kuliko watu.
A concerned citizen.