Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

hapa inazungumziwa TISS kuegemea chama kimoja, ww unaleta mambo ya CIA kupanga nani aongoze nchi, democratic na republican wanabadilishana uongozi bila matatizo nyie mnakumbatia chama kimoja. maendeleo mtasubir miaka 1000
Maturity ya chama kwenye kuongoza nchi ndio vinasababisha watu wapokezane ofisi kubwa bila shida . .. . . Tutafika huko ila kuna kazi kubwa sana ya kufanyika
 
Kama hii ilikuwa kazi ya kitengo mi naiunga mkono. Kazi yao wanaijua,

Ifikie mahali watu au idara zijue kazi zake. Na magufuli mwenyewe akija pewa ikulu aje awe anafanya kazi kitaalamu. Na wengine pia chini yake hivo hvo - tusipotoka tutakuwa na gundu

Yule jamaa mwingine angechukua nchi angekuwa haambiliki wala hashikiki - kutwa kucha kujaribu kurudisha hela zake alizotumia kwenye kampeni na kuwakomesha wenzie. Na wa kuwakomesha ilikuwa wawe wengi. Tanzania isingekuwa salama tena kwa weng wao

We umeona wapi mtu anakomalia na kushupalia jimboni kwa mbunge mwenzie eti asichaguliwe muhula ujao? Hii ni laana. Na kwakuwa vitu hivi viko wazi vitakuwa vime mgharimu. Ni mtu wa vurugu, fitina. Sasa akiwa rais anaweza fanya nini?
 

Hivi wewe haujapata soma kwenye biblia takatifu ile aya isemayo" jiwe walilolikataa waashi ndilo limekua jiwe kuu la pembeni". Unajua maana yake!
 
Kitengo hawakutaka JK awe rais 2005 lakini Mkapa baada ya kuona hawezi kuzima Moto wa JK wa 2005 hakukubaliana na kitengo.

JK baada ya kuingia madarakani 2005 aliwashiti kiaina kitengo ushauri wao mwingi aliupuuza, baada ya CCM kupitia kwenye mapito ya kujivua gamba kitengo wakamshauri JK amteue Kinana kuwa Katibu mkuu na Mangula kuwa makamu mwenyekiti , Kikwete alikubali alishindwa kuwakatalia baada ya kuona Chama kinakwenda mrama.

2015 kitengo hawakumtaka EL , Kikwete hakuwa na jinsi, kitengo walimpa taarifa ambayo hata ungekuwa wewe mleta Mada ndio JK ungelikata tu jina la EL.
 

Hakuna lolote, kitengo kilitaka kumuweka mwenzao, mjomba mbona vetting yao imeshindwa, na hiyo quality yao imeshindwa hata kwenye chama tu? Ni ujinga kufikiri usalama ndo wanatakiwa wachagulie watu rais. Obama alichaguliwa na CIA? nijibu wewe..! Toa pumba hapa
 
Na hakuna anaetaka kujadili hili
huu ni mwiko mkubwa demokrasia

Hakuna demokrasia kwa vi nchi kama hivi, wananchi hawako informed kina lowasa wanawanunua kwa sh elfu kumikumi unategemea waachiwe wafanye maamuzi magumu. Waacheni usalama wafanye kazi zao, hatuwezi kuyaachia nchi magenge ya kifamilia!
 
Hakuna demokrasia kwa vi nchi kama hivi, wananchi hawako informed kina lowasa wanawanunua kwa sh elfu kumikumi unategemea waachiwe wafanye maamuzi magumu. Waacheni usalama wafanye kazi zao, hatuwezi kuyaachia nchi magenge ya kifamilia!
​Nawe upo KITENGO eenh?
 
We unafikiri edo ni mjinga kama wewe? Wewe unafikiri apson ambae ni mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa mstaafu alikuwa ana kazi gani? Watu wapo extra smart..
 
Je Kitengo kipo kikatiba?Kama jibu ni hapana mbona kina nguvu sana hadi Mzee Kingunge anakihofia?Labda Kitengo ni baadhi ya vyombo vya usalama wa Taifa ambavyo vipo very invisible but very powerful and untouchable.Mh Lowassa amekuwa Waziri Mkuu,na amekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Bungeni,hivi hakujua nguvu ya kitengo kabla ya kutangaza nia?
Uchaguzi Mkuu ujao Ngazi ya raisi na wabunge hauna maana kwa wananchi ni kupoteza pesa za walipa kodi kwani kitengo kimeisha maliza kazi yake.
 
Nakubaliana na mtoa mada, Tanzania usalama wa taifa unahusika sana kupanga mbinu mkakati nyingi sana katika kuongoza nchi, lakini tunajua pia hata kusambaratisha upinzani wanahusika pia.

Na hii sio kwa Tanzania tu bali hata Marekani, tunajua kilichotokea kwa JF Kennedy na nduguye Andrew Kennedy, pia hapa bongo tunajua kilichomkuta Sokoine, kolimba, Gnl Imran Kumbe na wengineo.

Ninashuku hata Mwang'onda kwenye team Lowassa alikuwa pale kwa mkakati maalumu lakini sio kumsaidia Lowassa.

Tukirudi kwenye mchakato wa kumpata mgombea kwa ticket ya CCM, kwa kweli mchezo walioucheza hawa jamaa kumpata John Joseph Pombe Magufuli nawapa credit kubwa sana, maana laiti kama angechaguliwa Lowassa basi nchi ingewekwa rehani, na kama angechaguliwa Membe basi tungeshuhudia makundi, mpasuko, ukanda na visasi, unakumbuka wale maadui zake 11 aliyosema akishinda watakimbilia Kenya?!

Kumchagua Magufuli imekuja kama suprise na kwa kweli pamoja na mambo yote kwa record yake nzuri na ya kutukuka ya nyuma nivigumu sana kumchafua Magufuli, pili hana makundi wala ukanda kama Membe na Lowassa!

Hapa nawapa HEKO kitengo!
 

Yameanza leo??!!
Waliokuwa viongozi mbona hakuna aliyewahi kuhoji uteuzi wake??!!!
 
Badirisha title umenikera mambo ya ccm kuyahusisha na taifa/nchi mojakwamoja, we sema ccm inaendeshwa na KITENGO
 
Huu mzimu wa maneno ya mkosaji tu kwani palipo ushindan lazima mshindi apatikane sasa kama yule upendae mtu hajapitishwa hakuna haja haja ya kuanzisha maneno ya mbaazi kukosa maua na kuanza maneno mara ooh kitengo tuache maneno kama hayo nadhan ya dodoma yamekwisha kama watanzania tugange yajayo na pia kama mgombea wako hakushinda usizushe,kitengo hicho inamaana kijan yote ya wapiga kura dodoma ilikuwa kitengo,tuache utoto kama mgombea wako alikuwa mhimu sana awe kiranja wa nyumba yako,tusianzishe mambo ya uongo na ukweli ila nafurah watanzania wako macho sana maneno ya kichochez si tz bwana
 

Well said!
Hapa tatizo ni mfumo huu ulioasisiwa na chama 1!.
Lkn watu hawaelewi
Ooh magufuli jembe sijui nn!
Hakuna jipya chini ya huu mfumo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…