Nchi imeuzwa!

Hawa jamaa wasituzingue wameviua viwanda kibao ngoja nitaje vichache tu ninavyovijua tuanzie pale ubungo kulikuwa na kiwanda cha UFI, Fishnet,Maziwa,Urafiki. Mbeya kulikuwa na kiwanda cha ZZK-MBEYA. Haya twende kwenye usafirishaji kulikuwa na ma kampuni kila mkoa yaliyokwenda kwa jina la RETCO hapo ikitanguliwa na prefix zenye jina linalotambulisha mkoa fulani. Twende Ugawaji,SUKITA,RTC hawa jamaa wasitake kutuchanganya AISCO imefia wapi na kulikuwa na kiwanda kizuri tu hapa Tanzania cha ku assemble matekta ya VALMET. Twende STAMICO jamaa waeua kila kitu tulikuwa na TANCUT Almasi pale Iringa. Wa kulaumiwa nani? Nyerere hakuwa na hiyana kila sekta aliipatia japo chuo mfano chuo cha kilimo Sokoine. Mimi siongei zaidi.
 
Kama kawaida imekuwa kama mtindo kuwa hivi sasa tutegemee kauli kama hizi kutoka kwa wabunge....2010 sio mbali wajameni tuweni macho!

kwani ni linia lijua hayo wakati ni habari ya muda mrefu? kwa nini aseme sasa na sio wakati mwingine?
 
Umaskini wa Tz UNALETWA NA WATU WACHACHE AT THE EXPENSE OF THE MAJORITY.
Nawaambia ipo siku Tz zitakuja pigwa apa zaidi ya ulivyoona kenya.
Hatuwezi daily watu wanatufanyia mambo ya kipumbavu alafu bado wanapeta na kupiga bit wananchi?
 
Hivi hii nchi iliuzwa kabla ya kutekwa nyara, au walioiteka nyara ndio walioiuza au iliuzwa walioiteka nyara na walioinunua ni hao hao?
 
Huwa naupenda sana ule msemo maarufu hapa jf...Aseme huyo kiazi kwani miye muhogo nikisema naambiwa nina mzizi.
 
ccm lazima iwepo ili uwepo upinzani tanzania.
waache wana ccm wachukue hatua za kufanya mabadiliko ndani ya chama......kwa sababu najua hiyo ndio faida kwa mwananchi, na sio upinzani ambao utagonga ukuta kwa ccm na kumzidishia dhuluma mwananchi wa chini.
 

Gaijin CCM imegawanyika na ndio maana MAFISADI hawajakamtwa mpaka leo licha ya ushahidi kibao.

Na ndio maana hata huko bungeni migawanyiko yao imeendelea na issues hazikatwi tena kwani ndani ya CHAMA chenu kuna tunaotaka si tu wafukuzwe...Bali pia wawekwe ndani kwasababu ripoti zote zinaonyesha kuwa hao watu ni watuhumiwa.

Kwenye maswala yenu ya chama muwafukuze..Ya kitaifa ni WAKAMATWE MARA MOJA PERIOD.
 
Na inaonyesha hata jeshi nalo limenunuliwa ,haiwezekani kila eneo panapohitajika kufukuzwa raia wanatumika FFU ,hivi hawa nao mishahara yao ni mikubwa kiasi wanakuwa wapo mstari wa mbele katika kutekeleza ibara za ufisadi ?
 

Asha,
I hope you don't mean that Zitto is now part of their (Mtandao) team.
 
I am positive that Sinclair is just one of many, mostly white, indians, persians and arabs, who have easy access to our president and even our government documents, that even the influencial Tanzanians, like Mengi, don't have. Shame to you Kikwete and your fellas for making us, Tanzanians, slaves in our own soil.
 

Afadhali umesema wewe kiazi.
Nilimuonya Mh Zitto...Watu wakadhani ni chuki binafsi..Kumbe hata humo ndani ya Chama mlimwambia?
Nadhani na yeye keshagundua hayo sasa...Ndio siasa hiyo..Ajikusanye aombe msamaha halafu aendelee na mapambano
Ni ushauri wangu tu.
 
J.J Mnyika.
Eeeh bwana weee! sasa picha wazi kabisa ktk kila nachokiita siku zote Bongo connection!...
Hivi nani vile Mbunge wa nzega?...

Wanabodi,
Maneno haya ya Sinclair ni mazito sana na kama nchi huru nadhani Kikwete kwa mara ya kwanza ametoa mwanga wa kuwa impeached..

''I've had the privilege of reviewing the (Bomani) committee's recommendations - along with comments from the (Tanzania) Chamber of Mines - and have no serious issues with them. What's important to know, however, is that the man who will make the final decision on the recommendations is the president - not the committee.''

He continues: ''President Kikwete is an extremely knowledgeable and capable man who will do nothing to disturb the balanced fiscal policies that have produced enormous growth in Tanzania's economic base, most of it fuelled by international investors.''

Yaani JK kisha mpelekea salaam shetani kabla hata ya kuongea mapendekezo hayo na wananchi?...

sasa atasema nini kipya kwa wananchi kama sio yale alokubaliana na Sinclair! kipi atawakilisha kwa wawekeshaji ikiwa tayari wameisha jua kinachokuja!..
 
JK anaugonjwa sawa na wa Mkapa ingawa kakwake kamezidi.Anawaachia wengine watawale yeye yuko 'honeymoon'.Kuna haja gani ya kuwa na Rais mwenye rekodi ya kusafiri nchi za nje kama waziri wa mambo ya nje!au pengine anafikiri bado yuko foreign affairs?.Naona wizara ya membe haina kazi bora rais a-assume kazi za waziri wa mambo ya nje.

Reputation ya Kikwete kwa watu wa nje ni excellent.Hata Andrew Young aliwaambia wamarekani wenzake kuwa 'if you didnt happen to meet mwalimu nyerere here (meaning JK) is a man of his like'.Wapi bwana, kikwete na Nyerere wanashahabiana nini? tangu lini? labda alichanganywa na herufi za mwanzo za majina yao tu J na K.

Serikali inaongozwa kisanii kama kununuliana bia kwa raundi bar (wanwaji wanajua hilo).Kikwete kashajua kachemsha ila kuwakana wenzake inakuwa ngumu.Wanafunikafunika siku ziende.Kazi yetu ni kufunuafunua siku ziende tuwaduwaze kwa masanduku ya kura.Big up wanamtandao!
 
Last edited:
Nchi immeuzwa siku nyingi hata watu walishatuhesabu na kutuuza. Tatizo ni kwamba wengi wetuna njaa au tuko usingiizini au walalahoi.
 
Nilishasema hii nchi imeuzwa twangoja resiti tuu kieleweke!
 
Watanzania wanaojua ukweli kuhusu "utawala" wa Tanzania ni wengi sana lakini hawana ujasiri wala mtu wa kuwaongoza kwenye kupigania nchi yao.

Hiyo ndiyo turufu ya JK na chama chake. Mbaya zaidi majeshi yetu yote hayana agenda ya nchi wana mkakati mmoja tu wa "Ndiyo Mzee". Sasa kama akina Sinclair ndio wanayoiweka serikali madarakani ni wazi nchi imeuzwa. Cha kufanya ni kuvunja huu mduara wa umasikini na ujinga watu waelimishwe vizuri kwa lugha nyepesi.

Wabadilishe utamaduni wa kusaidiwa wajisaidie wenyewe.

Takwimu za wanachama wa forum hii wenye uchungu wa nchi kuuzwa naamini zinatosha kutoa elimu kwa watanzania kuhusu uuzwaji wa nchi.
 
2010 ikaja...

Haya,tusikate tamaa, hata hivyo kumbe tukisema nchi imeuzwa hatuko wrong?
 
Reactions: BAK
Haoni wala hasikii,hajui atakuja kuwajibika?Shauri yake...Kumbe hii mikataba ote mibovu ni yeye alisaini akiwa waziri halafu sisi tunalalamika ni washauri?

Halafu eti wanalalamika kuhusu suti?

Mkandara said:
Wanabodi,
Maneno haya ya Sinclair ni mazito sana na kama nchi huru nadhani Kikwete kwa mara ya kwanza ametoa mwanga wa kuwa impeached..

 
Mama alisema ukweli mtupu,je tumejifunza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…