Nchi imekauka, mambo hayaendi...

Huyu jamaa ni kiboko alisemaga lakini tusitupe suruali za zamani baadaye zitatutosha leo nimevaa suruali niliofanya date ya kwanza kwa mke wangu pale Blue palm kwa nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi unaijua DAR vizuri???

ulishatembelea shule zote uone watoto wanavyokaa chini?? walimu je?? mmeajiri lini baada ya kutumbua??

kule mahospitalin wajawzito wanapoambiwa wakajinunulie vifaa na bado wanalala 3 kitanda kimoja hujaona??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hivi mtu maskini unamnyang'anya nini hadi alie? Maskini anakosa nini? maskini anachotamani ni kwenda juu.. watu wa chini wanalalamika nini wakati walikuwa tayari chini; wao matumaini yao ni kwenda juu. Angalia maelfu ya vijana walioajiriwa kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi... watu ambao walikuwa hawajui wataishi vipi leo wanaweza kufanya kamradi kao kakalipa..na hapa ndio watu wanakosea.. wanafikiria kulalamika "maisha magumu" kunatosha kubadilisha tu serikali.. watu wakiona mahitaji yao mbalimbali yanaanza kutimizwa wataona tofauti...

Hakuna maisha magumu ambayo watu wanalalamika sasa hivi ambayo yameanza juzi tu; uwe mwangalifu kudhania kuwa watu wote Tanzania hasa walio wengi wanaonalalamika na kuwa kwao maisha yamekuwa magumu zaidi sasa hivi kuliko wakati wa JK. Hili si kweli...
 

Hapa sasa ndio unatakiwa useme na kutoa ushahidi wa hili ili watu washughulikie... usilalamike pembeni. Hospitali gani wa kina mama Dar wanalala watatu watatu kitanda kimoja.. embu tutajie ili kina Ndungulile wapate taarifa hapa hapa...
 

Inawezekana kabisa hukujua ni kwa kiasi gani ufisadi ulikuwa unaendesha uchumi; hivi mnafikiri tulikuwa tunapinga ufisadi ili ili kila mtu aishi tu kwa raha.. au mlidhani ukiushambulia ufisadi nini kitatokea. Tanzania haijafika mahali bado kabisa pa kuweza kuwa pepo ya wengi... ufisadi uliharibu siyo tu watu wa serikali; uliathiri hadi wakulima na watoto ambao hawajazaliwa bado. Madhara ya ufisadi yalikuwa ni mapana mno na hata sasa bado hazijachukuliwa hatua zote sahihi na stahiki kusahihisha mfumo wetu. Kwamba hali ni ngumu ili lilitarajiwa.
 

Kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya Watanzania milioni mbili wameingia katika umasikini wa kutupwa tangu mwaka 2015-2018 (Kwa mujibu wa kauli ya mbunge Zitto Kabwe bungeni, serikali haikukanusha)

Wakati wa J.K uchumi ulikuwa unakuwa kwa wastani wa 7% sasa hivi tunaambiwa ni 6 point something percent, hiyo reduction japo ni ya points kadhaa inawakilisha nini interms of kipato cha watu?

Kipindi cha JK kulikuwa na watu masikini, lakini kipindi cha huyu mheshimiwa Umasikini wao umezidi zaidi, na wale waliokuwa na nafuu kipindi cha JK sasa wengi wao wamegeuka masikini.

Biashara zinakufa kwa kasi ya kutisha!
 
Wanaoibeza Serikali iliyoko madarakani hawana hoja dhabiti ni kulalamika tu. Isitoshe hawatoi sera/mikakati mbadala ya maendeleo au kukuza uchumi. Wanaamini mchawi wa matatizo yao ni Rais Magufuli badala ya kuchambua kwa kina ubora na udhaifu wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi, 2015 na kwa kiwango gani imetekelezwa na Serikali yake.

Upinzani ungetanabahi kuwa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, 2020, CCM inatathmini kiwango cha utekelezaji wa Ilani yake, nao wangejipanga ipasavyo kutathmini kiwango cha kutimiza ahadi zao katika majimbo na halmashauri wanazongoza. Badala yake wanahangaika kuikosoa Serikali kwa maneno ya ulalamishi, kebehi na matusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…