Nchi iko salama na Haijayumba, mpuuzeni Mbowe - CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi iko salama na Haijayumba, mpuuzeni Mbowe - CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 25, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 25, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gloria Tesha
  Daily News; Saturday,October 25, 2008 @00:02

  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema nchi haijachafuka wala kuyumba kama wanavyosema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na kuwataka Watanzania wapuuze kauli hizo zenye kila dalili ya uchochezi.

  Aidha, CCM imemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuacha mara moja tabia ya kumsema vibaya Rais Jakaya Kikwete kwa kile kilichodai kuwa ni udhalilishaji wa kiongozi huyo wa nchi na kamwe CCM haitavumilia jambo hilo.

  Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati, alipokuwa akitoa tamko la CCM kuhusu hali ya kisiasa na kiusalama nchini kwa waandishi wa habari Dar es Salaam.

  Chiligati alisema taarifa hizo za baadhi ya wanasiasa zinasambaza hofu, woga na wasiwasi mkubwa si kwa wananchi tu, bali hata kwa wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza na ambao tayari wapo nchini.

  “CCM inasema nchi ipo salama na haijayumba kama wasemavyo hao wapinzani na mali za wananchi na wawekezaji zipo salama hivyo kauli hizo ni za watu walioishiwa sera,” alisema Chiligati.

  Alisema viongozi hao wamekuwa wakitumia matukio na matatizo yanayolikabili taifa hivi sasa kama vile mgomo wa walimu, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mafisadi wa EPA na Mwafaka wa CUF na CCM kwamba ndiyo ajenda kila wanapopanda majukwaani au kuzungumza katika mikutano na kusahau kwamba serikali imekwishasema inayafanyia kazi.

  Alisema CCM inatambua kuwa changamoto hizo zipo, lakini masuala yote yanashughulikiwa kwa wazi na kila mtu anafahamu hilo na kusema “kwa mfano suala la EPA mbona hata Novemba mosi haijafika watu wanaanza kusema, wasubiri waone ndipo waseme, maana Rais alishasema yote wanayoyasema bungeni Agosti mwaka huu.”

  Kuhusu madai ya walimu, aliiomba kamati ya pamoja ya kushughulikia madai hayo iliyoundwa kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili uhakiki ukamilike na walimu walipwe mapema kwani ni haki yao.

  Kuhusu mwafaka kati yao na CUF, Chiligati aliwataka CUF kurudi katika meza ya mazungumzo na kukanusha taarifa za chama hicho kwamba mwafaka tayari, akisema kilichokuwa tayari ni mapendekezo ambayo yamerekebishwa na vyama husika ili yajadiliwe tena na Kamati ya Mwafaka.

  Kuhusu habari zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku juzi zikimnukuu Mbowe kuhusu kumdhalilisha Rais Kikwete kwamba Watanzania walikosema kumchagua kuwa Rais kwa kuwa hana uwezo na ameshindwa kuongoza nchi, Chiligati alisema kauli hiyo ni ya uchochezi na anapaswa kuomba radhi.

  Alisema maneno hayo hayana heshima hasa ikizingatiwa kuwa Kikwete ni Rais wa nchi aliyeshinda kwa kura asilimia 80 mwaka 2005, jambo lililoonyesha kuwa Watanzania wanamfahamu na wana imani naye ndiyo sababu wakamchagua.

  “Mbowe ni nani kwanza mpaka amchafue Rais kiasi hiki, amepata wapi ujasiri wa kusema haya? Hana sifa yoyote hapa nchini. Historia na sifa zinaonyesha kwamba ni mchezeshaji disko na kamari katika majumba ya starehe anayomiliki na si chochote wala lolote,” alidai Chiligati.

  Alisema kila raia kwa mujibu wa Katiba ya nchi, ana haki ya kuzungumza na kumkosoa Rais, lakini si katika hali ya udhalilishaji, kejeli au dharau na kwamba CCM inatoa onyo kali ikimtaka Mbowe achunge mdomo wake kwa kauli zake na heshima yake. Alisema demokrasia ya kweli inahitaji heshima na uungwana na endapo ataendeleza kashfa dhidi ya Rais, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na kwa mwanasiasa ye yote atakayefanya hivyo.

  My Take:

  Hivi demokrasia lazima iwe na heshima na uungwana?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Ayasemayo Mbowe yasingekuwa effective Chiligati asingepoteza pumzi yake kulalamika kuwa mambo ni bwerere Bongo. Wanaogopa jinamizi la Tarime lisisambaze mabawa yake katika mawingu ya Tanzania nzima. Na wapi ilipoandikwa kuwa mchezeshaji wa disco hana haki ya kuzungumzia hatima ya nchi yetu?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Ni wenye akili finyu ya kutafakari mambo ndiyo bado wanaamini kwamba nchi haijayumba. Aliyoyasema hayo ya nchi kuyumba si Mbowe pekee yake bali pia viongozi wa dini mbali mbali na hata Warioba ambaye ameshatoa kauli zinazoashiria nchi inayumba. Chiligati uwongo wako tumeuchoka, hebu muogope Mungu wako hata siku moja tu ili useme ukweli.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nadhani hayo ndiyo Chiligati anayoweza kusema na pia anayotakiwa kusema na Chama chake.

  Tatizo langu ni kutaka Rais asisemwe. Kwani yeye ni nani hadi asisemwe na mtu yeyote. Mimi nadhani kama Chiligati na CCM wanataka Rais asisemwe wamwambie kwanza atekeleze aliyowaahidi Watanzania na pia atekeleze wajibu wake kama Rais na si kama mtalii wa Ikulu!!!

  Na hili suala la Chiligati kusema kuwa Mbowe ni mchezesha kamari wa Casino ni upuuzi mtupu. Hata kama angekuwa hivyo, hiyo haimfanyi kuwa mbumbu kiasi cha kutoona upuuzi unaofanywa na Serikali ya wasanii! Kwani hajui kwamba kuna watu waliwahi kuwa wacheza sinema lakini wakawa viongozi wazuri!! Tatizo analotakiwa kujua ni kuwa Kiongozi mzuri hawezi kutoka mbiguni, atatokea humu humu kwenye jamii zetu. Ili mradi anaweza kutofautisha usanii na mambo halisi inapofikia suala la kuongoza jamii. Hapo ndipo naona waheshimiwa wetu wanapata taabu, wanadhani kila mahali ni sanaa na usanii tu!
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa kama wanataka kusema hivyo mbona CCM inakumbatia majambazi, mafisadi, wakwepa kodi na wehu wengu tu kama mtaji wao, sembuse Mbowe anayefanya biashara halali. Nadhani Bw. Mbowe angepatikana na kosa la kutolipa kodi saa hizi wangekuwa wameshamfilisi kabisa kwa sababu inavyoonekana anawindwa kweli kweli ila hawajampata tu.
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Amesema Askofu wa KKKT, CHADEMA, MBOWE, ZITTO,SLAA, WARIOBA, KICHWANGUMU, NA WANAJF na WATZ sasa tupuuzie Mbowe peeke!!! Hapana hii itakuwa 9 - 1.

  Mimi nakupuuza wewe Chiligati, nasita kwa CCM maana nataka Mwenyekiti wenu ajibu. Kama ndo Rais mimi sijui, hapa aliongea kama Mwenyekiti. Akiongea kama mmiliki wa Billicanas ndo Rais wa Tz nae aongee au wewe.

  Bla blah
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Chilingati et al 2008, ni wavivu wa kufikiria na kutafakali alama za nyakati, mbona hamsemi mwenyekiti wa sisiem kuwa ni msanii anayeishi Ikulu? Hajui nini cha kufanya zaidi ya kuuza meno?
   
 8. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi Muungwana pekee huongea mantiki, lakini hawa walio chini yake naona hawakawii kukurupuka na kutishia kutumia nguvu ya dola na ubabe kama vile hawajapata funzo toka Kenya,Zanzibar,Zimbabwe etc ni watu ambao wana kiburi cha hali ya juu katika kuongoza wanainchi na kushindwa kusoma alama za nyakati, nina imani sio mbali watapata majibu yao
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  ...tunajuwa kuwa novemba 1 ...mmepanga kuwatafuta mbuzi wachache wa kafara na kuwaacha the real culprits kwenye EPA wakitamba......kama kweli mtataka tuwapongeze..pelekeni mahakamani hiyo nov 1 the real mafia kamalowaasa ,kikwete, rostam,jeetu patel,noni,...et al..lakini sana sana mkijitahidi labda mtamtia kashi kashi johnson...na nawaonea huruma wale wafanyakazi wa BOT ...wanaoandaliwa kutolewa sadaka kama baba yao daud balalli.......
   
 10. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #10
  Oct 25, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasanii wa "Ze Comedy" aka chama cha mafisadi at its best. Kujibu hoja kwa vioja.
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu huwa inanikera when someone refers JK with the purported 80% win in 2005. That was then and was thru corrupt means involving hell lots of $$$$. Even the REDET polls suggested he had huge support but what about now????? Go ask the pple accross the spectrum, ask ur mama, ur dad, ur uncle, bro or sis, ur neighbor, REDET and even the Dogs, yes DOGS all know huyu mkulu uwezo ni mdogo kuliko kazi aliyopewa.
   
 12. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  “Mbowe ni nani kwanza mpaka amchafue Rais kiasi hiki, amepata wapi ujasiri wa kusema haya? Hana sifa yoyote hapa nchini. Historia na sifa zinaonyesha kwamba ni mchezeshaji disko na kamari katika majumba ya starehe anayomiliki na si chochote wala lolote,” alidai Chiligati.

  RONALD REGAN ALIKIWA MCHEZA CINEMA NA AILIIONGOZA AMERIKA VIZURI SANA!
   
 13. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #13
  Oct 25, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM Walisema KELELE ZA....... HAZIMKOSEHISHI MWENYE NYUMBA USINGIZI,Kumbe yanawakosesha usingizi???????????????
  NA BADO.
   
 14. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #14
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ahadi ilipotezwa na "serikali ya wasanii"...the man screwed up the political mileage he got in 2005.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Si kwamba wanajibu hoja kwa vioja, hawana la kusema. Kama wangekuwa nalo, duu hakuna mtu angelala wallah nakwambia!!! Ila kwa sababu hawana hoja, wanajikuta wanasema au kupayuka lolote kwa sababu ni wajibu wao kusema ili kutunza kazi zao! Ni ile dizaini ya "Commical Ali wa Iraq". Hata hivyo muda hauko mbali itabidi watupe majibu bila kuanza kung'ata midomo kama wanavyofanya sasa.
   
 16. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Chiligati ameishiwa hoja na kukosa shabaha kama kawaida yake!
  Hivyi mchezehsaji disko na kamari na yule ambaye anawaibia walalahoi wa nchi hii bila huruma na kuwanyanyaza yupi bora?Chiligati na CCM yake wanajua kabisa kwamba CHADEMA kwa sasa wameiteka nchi na wanajua watakiona cha moto 2010.Wasituletee upuuzi hapa washahulikie mafisadi kwanza then waanze kutema porojo zao.
   
 17. d

  defence JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2008
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 508
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 60
  Hi wana JF,
  Chillllingatii naye huyo kajitokeza wakukodi walikuwepo kule Tarime wakina Tabwe Hizza(wote idara moja) tulipata kuwasoma kwenye magazeti.
  Sasa huyu Chillingati kwanza akae akijielewa kuwa yeye kama yeye hatakiwi kujifananisha hata chembe na Mbowe kiuwezo kwani kwa kutumia ulinganifu wa pato la uchangiaji gharama za pato la Taifa Muh. Chillingati hamfikii hata kwa chembe kwa hizo hizo biashara anazozifanya Muh. Mbowe na sijajua kama angelikuwa alipi kodi ingelikuwaje?
  Achana na hayo hivi kweli kwa mtu makini anaweza kusimama na kuitisha waandishi kuzungumzia biashara ambazo zinachangia pato la taifa kwa muhusika kulipa kodi kama mapungufu ya mtu katika upeo wa uchangiaji wa mada muhimu kuhusu kuporomoka kwa UADILIFU WA VIONGOZI TULIO NAOM LEO NDANI YA NCHI Chilllingaatiiiiii AKIWEPO?

  Kwa taarifa ya wana JF kuna fununu kuwa Muheshimiwa huyu karibu na uchaguzi ujao atakuja na hoja ya kuuziana nyumba za NHC hili nimelisikia ni sera wanayoipanga kuja nayo, tusubiri tuone.

  Lakini yote ya yote nilikuwa namshauri Ndg Chiligati ajibu hoja sio vitisho nchi hii si yake ni yetu yeye ni mtumishi wetu tunayemlipa ni sisi awaulize wakina Lowasa kutoka kwenye vingora hadi kutembelea magari ya tinted kukwepa aibu.

  Natoa hoja
   
 18. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  The fundamentals of the economy are strong.... Everything is under control.
   
 19. H

  Herbert Member

  #19
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli mi naanza kwa kushangaa hizi takwimu za kupikwa. Kama walishinda kwa asilimia hizo zote ni wao wenyewe wanazijua.


  Kiboko ya Tembo Sisimizi .


  Nawapongeza Star TV kwa kipindi chao cha Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni kwa ukweli waliotuthihirishia kutoka kwa mwanakijiji wa kabila la Wahzabe kwa kutamka hadharani kwamba anakumbuka nchii hii iliwahi kuwa na Raisi Mmoja anaitwa Nyerere ila anasikia alishakufa anashangaa mpaka sasa nchi bado haijapata Raisi Ama Vipi??

  Haya ni Maneno makali sana na inabidi huu ushindi wa asilimia 80% uwe unawalakini.
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .....Precise words of the "Tanzania Economical Comical Ali" (TECA)
   
Loading...