Mamzalendo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 1,670
- 558
Jamani ndugu zangu kwa nini tunategemea nchi iendelee kwa staili hii, mimi mwaka jana niliomba kufungiwa maji kwenye plot yangu mwezi wa tisa mpaka sasa hamna kitu na nimelipia kila kitu nikifuatilia napigwa tarehe tu, januari wakaniambia chimba mtaro nimechimba mpaka sasa mtaro umeziba hawajaja, hivi niwafanyaje? Naongelea Kilimanjaro ambayo watu tunategemea iwe na maendeleo. Hatuwezi kuendelea kwa sababu toka mwezi wa tisa ningekuwa nimetumia maji na likawa pato kwa taifa kwa ulipaji wa bili zangu, pili ningeweza kufanya biashara zangu na kuiingizia nchi hela lakini hawa watu hawafikiri wanabaki kusema mishahara inachelewa itaendelea kuchelewa kwa sababu ya ujinga na kutotaka kufikiri. Jamani kila mtu kwa nafasi yake atoe huduma kwa wakati. Ningekuwa na uwezo ningeishtaki idara ya maji kwa hasara yote niliyopata kwa kutopata maji. Sasa hivi nimeamua kutofuatilia maana ufuatiliaji wangu hauzai matunda au mnanishauri nifanyaje jamani? Nimechoka kabisa kila siku nasikia watu wanafungiwa lakini mimi nikiuliza vipi tarehe tu! Na rushwa sitatoa hata shilingi kama ndo wanachosubiria.