Gharama za matumizi yakonwewe ndio yanaondoa tafsiri kuwa mshahara unaolipwa ni mkubwa/mzuri?mlete na gharama za matumiz maan unawez ukalipw mshahar uwo ila gharam za matumiz zikaw kubw
Kama unalipwa milioni 30 alafu gharama za chakula na malazi zinafika milion 15.wakati mwenzako analipwa milioni 25 ila gharama za chakula na malazi ni milion 5.ipi itakuwa nchi bora hapo?Gharama za matumizi yakonwewe ndio yanaondoa tafsiri kuwa mshahara unaolipwa ni mkubwa/mzuri?
China?NCHI 10 ZINAZOLIPA VIZURI MISHAHARA DUNIANI
![]()
Je, ulishawai kujiuliza nchi ambazo wafanyakazi wanalipwa mishahara ya juu? Hebu tuangalie nchi kumi ambazo wafanyakazi wanapata malipo makubwa ya kazi zao wanazofanya
#10 Ufaransa
Ufaransa ni nchi ya 7 yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, Wafanyao kazi Ufaransa wanafanya kazi kwa mda mchache ni kama masaa 35 kwa wiki. Kwa wastani kipato cha mfanyakazi wa Ufaransa ni $28,799 kwa mwaka baada ya kulipa kodi zote.
![]()
#9 Sweden
Kutokana na data za Bank kuu ya dunia,hii nchi nzuri ya kiscandinavia ni ya sita kwa uchumi wa ndani duniani. Sweden ni wazalishaji wakubwa wa mbao. Kwa wastani kipato chao ni $29,185 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi
![]()
#8 Canada
Canada majirani wa Marekani,ni nchi ya tatu yenye uhifadhi mkubwa wa mafuta duniani ikipitwa na
Venezuela na Saudi Arabia. Nchi hii pia ina utajiri mkubwa wa zinc, uranium, dhahabu na aluminium.
Kwa wastani kipato chao ni $29,356 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi
![]()
#7 Austria
Austria ni nchi ambayo ipo katikati ya Ulaya, Imeendelea sana kiviwanda na sekta ya utalii
inachangia asilimia 9 ya pato la ndani la taifa. Kwa wastani kipato chao ni $31,173 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi
![]()
#6 Germany
Germany ni nchi ya kwanza yenye uchumi mkubwa zaidi ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $31,252 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi
![]()
#5 Australia
Australia ni moja kati ya nchi zenye uchumi imara zaidi duniani,ni wasafirishaji wakubwa wa madini na wanaagiza bidhaa chache sana kutoka nje.Katika swala la wastani wa utajiri, Australia ilishika nafasi ya pili duniani baada ya Switzerland mwaka 2013. Kwa wastani kipato chao ni $31,588 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi
![]()
#4 Switzerland
Uswisi inashika nafasi za juu katika utendaji bora wa serikali yao, ikiwa ni pamoja na uwazi wa serikali yao, uhuru wa raia, ubora wa maisha, ushindani wa kiuchumi na maendeleo ya binadamu. Kwa wastani kipato chao ni $33,491 kwa mwaka na wanafanya kazi masaa 35 tu kwa wiki.
![]()
#3 Norway
Norway ina utajiri mkubwa wa maliasili ikiwa pamoja na mafuta,umeme wa maji,uvuvi na madini.Kwa wastani kipato chao ni $33,492 kwa mwaka
![]()
#2 Luxembourg
Luxembourg ni wasambazaji wakubwa wa chuma ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $38,951 kwa mwaka
![]()
#1 USA
Pato la ndani kwa mwaka ni $55,000 na makato ya taxi ni asilimia 23.Wafanyakazi wa Marekani wanafanya kazi masaa 44 kwa wiki.
![]()
chanzo.Nchi 10 zinazolipa vizuri mishahara Duniani | Kwetustar
... na kuna vibarua wanalipwa elfu 3 kwa wahindi; baa "medi" wanalipwa 80K to 100K kwa mwezi; house girls 30K to 60K kwa mwezi. Kwa ujumla the "masses" mishahara kwa mwezi ni under 800K kabla ya kodi; zaidi ya hapo ni "elites" walio wachache.Tanzania vipi? Kuna watu wanachota M40+ kwa mwezi.
... Japan yenyewe haimo ndio iwe Afrika?Afrika hakuna hata nchi moja[emoji134] [emoji134]
... chukua mishahara yote inayolipwa nchini then ijumlishe kwa pamoja then gawanya kwa idadi hiyo ndio maana ya wastani! Hiyo $55,000 ni wastani which means kwenye hiyo nchi wanaolipwa mishahara ya juu ni kufuru na wa chini ya kiwango hicho pia wapo!Hivi hiyo $ 55000 kwa mwaka si ni Tsh 10M kwa mwezi? Bongo wa hivyo mbona wako wengi tu; au wana maana hiyo ni kima cha chini cha mshahara? Anyway, ukiangalia purchasing power yao utaona huyu wa huku bongo ana unafuu sana; Ni sawa kwamba ukiwa Ksh 50,000 ni sawa na Tsh 1000,000; now ni bora niwe na hiyo milioni hapa bongo kuliko kua na hiyo 50 uwe nayo Kenya, ukiwa bongo na hiyo milioni unaweza kununua vitu vingi zaidi kuliko ukiwa na hiyo 50 Kenya. Maisha ni fumbo kubwa
Well understood brother... chukua mishahara yote inayolipwa nchini then ijumlishe kwa pamoja then gawanya kwa idadi hiyo ndio maana ya wastani! Hiyo $55,000 ni wastani which means kwenye hiyo nchi wanaolipwa mishahara ya juu ni kufuru na wa chini ya kiwango hicho pia wapo!
... kwa ufafanuzi huu, asiyekuelewa ana lake jambo!Nilichogundua katika huu uzi ni either watu wengi hamjui hesabu au hamjasoma uzi vizuri. Mleta mada ameleta pato la wastani katika nchi kadhaa.
Wengine mkasema mbona kuna watu Tanzania wanavuta hadi millions 40+ kwa mwezi na hoja nyingine nyingi.
Lakini mmesahau hapa kinachozungumziwa ni WASTANI (AVERAGE). Maana yake tukichukua idadi ya watu wenye ajira rasmi (wanaopokea mshahara) tukajumlisha mishahara yao kwa pamoja kisha tukagawanya hicho kiasi kwa idadi ya hao watu ndio tunapata WASTANI.
Mfano hapa mmeongelea Tanzania kuna watu wanalipwa 40m+. Ni kweli lakini katika idadi ya watu wote Tanzania wenye ajira rasmi (wanaopokea mshahara) hao watu wanaopokea aina hiyo ya mshahara hawazidi asilimia moja (1%) ya waajiriwa wote.
Tufanye hesabu kidogo.
Tuchukue sample ya waajiriwa 100. Kati ya hao ni wawili (2) tu wanaolipwa milions 40, hao tisini na nane (98) tuseme kila mmoja analipwa laki tisa (900,000) kwa mwezi. Sasa hapa tukitaka kupate mshahara wa wastani kwa idadi hiyo ya watu kwa mwezi tutafanya hivi.
40,000,000 ×2 = 80, 000, 000
900, 000 × 98 = 88, 200, 000
Tukijumlisha 80, 000, 000 na 88, 200, 000 tunapata 168, 200, 000.
Hii 168, 200, 000 ndio idadi ya mshahara wa watu wote 100. So tukiigawanya kwa idadi ya watu.
168, 200, 000÷100 = 1,682, 000.
Maana yake mshahara wa wastani kwa mwezi ni hiyo 1,682, 000.
Kinacho determine kama wastani utakuwa mdogo au mkubwa ni gap kati ya wanaolipwa mshahara mkubwa na wanaolipwa mshahara mdogo.
Huwezi kupata wastani mkubwa katika population yenye chini ya asilimia moja ya wanaolipwa executive salaries na zaidi ya asilimia tisini (90%) ya wanaolipwa chini ya million moja.
wenzetu kule wame induce mentality ya ulipaji kodi toka mtu akiwa mdogo. imefika mahali mtu asipolipa kodi anaona aibu, yaani jamii inamuona kama si wa kwao. ana feel guilty.Nilimsikia Kitila akisema Wananchi wa Sweden wanapenda kulipa kodi, naona anatamani tuige Sweden.....sasa sijui na sisi tupo namba ngapi.
We boya huwa upo bado?Usiwe kichwa ngumu!umeambiwa baada ya makato yote ya kodi hicho ndicho kinachobaki kama take home.