NCCR nao wakataa posho za vikao Bungeni

Ah! Unataka kususa kwa hilo tu! Kwani katumwa na uongozi wa JF kukutukana? Hiyo ni mbinu ya wengi humu kutaka kukuondoa kwenye hoja unayoisimamia na hasa inapokuwa na ukweli unaoumiza.
"'Hiyo ni mbinu ya wengi humu kutaka kukuondoa kwenye hoja unayoisimamia na hasa inapokuwa na ukweli unaoumiza"ASISUSE SAWA LAKINI AKIWEKA HOJA AMBAZO HAZINA MASHIKO ATEGEMEE RACTION KAMA HIZO,KWA SABABU HWEZI KUSEMA 70,000 HAISAIDII KITU WAKATI KUNA WABUNGE 300 MARA ELFU SABINI TSH NGAPI KWA SIKU MARA SIKU KUMI,HOSPITALI NGAPI HAZINA HATA PANADOL AACHE UJINGA HUO APELEKE FACEBOOK HUKO,CCM WANAWAPA WANANCHI FEDHA KIMYAKIMYA WAPI?WAKATI KUNAMFUKO WA MAENDELEO WA JIMBO,NDIO MAANA AKAPATA MAJIBU YA DHARAU
 
Usikurupuke best, mwalimu unayemzungumzia ni yupi? hivi unajua kuna walimu wenye mishahara mikubwa kuliko Wahasibu na Madaktari? be specific man

acha ukichaa, mwalimu anamzidi lini mhasibu?daktari? Kama unaongelea private sekta uko ni bargaining power wala mwenye akili timamu hawezi kulifikiria kwa kuwa hata sekretari wa kagoda ltd anamzidi msahara hata mtumishi wa hazina,ila ktk ngazi za govt.umechemka. Mwalimu kwa mapato hamfuati hata mhasibu msaidizi II. Na ukiongeza marupurupu ndo umewatenga kabisa,na overtime? We chunguza kwanza. Nakupa mfano mhasibu wa wilaya ana haki ya kuitumia gari ya STK ambayo hutumia DAS,yani district administrative secretary,mwl anapata usafiri huo?overtime?tuisheni au? Transport allowance kwenda na kurudi hazina hata ikiwa kila wiki? Je nauli kwenda na kurudi kutoka kwa mhasibu wa mkoa hata kama ni kila siku ktk majukumu? Hapa namuongelea mhasibu mdogo ktk ngazi za kiserikali,je mwl anaweza ayo? Sometimes we should call a spade a spade,mwl na mhasibu/daktari hawalinganishwi! Believe or reject!
 
Nimefurahi sasa Zito kuamua kutokuchukua kabisa posho maana kupeleka KDI haikuwa sahihi bado wangesema amechukua na kupeleka Kigoma. Sasa mnaweza kuona wabinafsi;;;;CCM wote, Mrema na TLP yake na CUF wote. NCCR nao wamebadilika wanaunga mkono mambo ya maana. Nawaomba pia watumishi wa serikali wakatae hizo posho maana wakipewa mshahara wao sitahili kama ulivyoombwa na TUCTA basi hawahitaji tena hizo posho zisizokuwa na uhalali
 
Kwa hili natofautiana na Chadema na NCCR-Mageuzi, hapa wanatafuta umaarufu kwa bei chee, hivi mnafahamu kiasi wanachokigomea? posho ya kikao kwa taarifa yenu ni Tshs70,000 kwa siku, kwanini wasigomee Milioni90 za magari? Tusishabikie upuuzi NCCR sasa wanaonyesha hawana mwelekeo hiyo hoja ya Zitto ni ya kitoto sana, kama ana machungu na wananchi kwananini asigomee M90 au angechukua awapelekee. au tatizo liko wapi angepokea posho za vikao na angezipeleka kwa wananchi? Kwa wabunge wakomavu(wengi wapo CCM). Wanapokea hizo posho na wanawapelekea wananchi kimyakimya bila kujitangaza magazetini. Hata hivyo simlaumu sana zito nasikia kiumri bado ni kijana mdogo sana hivyo watu wazima tunawajibika kumshauri

Mbona sikuelewiii.. kama ni kidogo kwa nini CCm waendelee kung'ang'ania walipwe....what are they loosing endapo wataachana nayo kama ni kidogo....kwa vp wakatae hoja hiyo kwa mijasho namna hiyo, fikiri ndugu yangu usikimbilie figures usizokuwa na uhakika nazo, wenzio wanachota zaidi ya hicho,ndio maana wanaofahamu wanapinga
 
Mkuu kutofautiana na CDM & NCCR si tatizo kwa kuwa nin haki yako ku express your views, lakini hawa wanajaribu kutushawishi kwa hili.CCM ni lini wamethubutu kufanya kitu kama hiki? most of them they are hypocrites wanajifanya kuwa ni wokomavu, ndio niwakomavu wa kuwaibia na kuwadhulumu masikini cake yao.GRAZZIE CDM&NCCR.
 
Nia ya Zitto Kabwe siyo mbaya, ninapomuona ni mtoto ni pale anapotaka pesa zake ziwekwe kwenye account ya KDI ndipo anakosea kwani kwani kwa kufanya hivyo analiongezea majukumu bunge, kwanini asichukue hiyo pesa na aipeleke yeye? unapomuomba mtu akusaidie kazi fulani tegemea yes or no maana hilo ni jukumu jipya kwa wahasibu wa bunge

Ujue hapo MwanaCCM (Magamba) dogo alivyo na akili ... Ngoja nikupe darasa. Zitto anacheza na kanuni kuhusu mahudhurio. Yeye ataendelea kuwepo kwenye vikao lakini kumbukumbu zitaonyesha hajahudhuria. Kwa kanuni watapaswa kumwajibisha; hapo ndipo zege litakapokuwa limetulia. Upo hapo Mwanamagamba? Wewe na chama chako cha magamba mtasoma namba tu hapo!!!
 
Wana JF suala la posho ni janga la kitaifa kwani sio wabunge tu wamekuwa wanapata posho peke yao. Katika halmashauri na manispaa na oficisi za za serikali wilayani na mkoani madiwani ambao wanalipwa mshahara kwa kazi ya udiwani hupata posho kwa kila kikao cha kamati wakihudhuri vikao. Kwa siku diwani anaweza kuhudhuria vikao hata vitatu vya kamati tofauti na kupata posho "stahili" mara tatu. Na kama haitoshi ofisa, hata karani wa serikali/halmashauri nae hupata posho. Wizi mtupu kwa maoni yangu kwani wote hao hupata mshahara kila mwezi.

Akitokea mtaalamu akakokotoa posho japo za manispaa kubwa tatu nchini utaona ni kwa jinsi gani nchi inahujumiwa. Kubwa zaidi utaona ni pesa kiasi gani itapatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta mbali mbali kwa kusitisha posho hizo ambazo naona ni wizi mtupu.

Naunga mkono hoja ya ZITTO na CHADEMA.
 
Big up nccr inapofikia wakati upinzani wanaungana kwa mambo ya msingi kama haya inatia moyo.Magamba chalii
 
Kwa hili natofautiana na Chadema na NCCR-Mageuzi, hapa wanatafuta umaarufu kwa bei chee, hivi mnafahamu kiasi wanachokigomea? posho ya kikao kwa taarifa yenu ni Tshs70,000 kwa siku, kwanini wasigomee Milioni90 za magari? Tusishabikie upuuzi NCCR sasa wanaonyesha hawana mwelekeo hiyo hoja ya Zitto ni ya kitoto sana, kama ana machungu na wananchi kwananini asigomee M90 au angechukua awapelekee. au tatizo liko wapi angepokea posho za vikao na angezipeleka kwa wananchi? Kwa wabunge wakomavu(wengi wapo CCM). Wanapokea hizo posho na wanawapelekea wananchi kimyakimya bila kujitangaza magazetini. Hata hivyo simlaumu sana zito nasikia kiumri bado ni kijana mdogo sana hivyo watu wazima tunawajibika kumshauri
nimetoka kusema punde tu mambo wanayofanya wana CCM yanashangaza sana wanaongea utazani vibogoyo unafananishaje mkopo na posho.jamaa wanahitaji maombi
 
hakuna cha kuwabananisha eti wanataka cheap popularity....msiotaka cheap popularity mmeifanyia nchi hii nini hadi sasa? hebu waacheni wazalendo wawazw kizalendo,watende kizalendo katika nchi isiyo na uzalendo matunda yake tutayaona soon
gooo chadema goooo...goooo nccr goooo! si lazima uwe mwanachama au mshabiki wa vyama hivi ili uweze kuelewa dhana nzima ya hili tendo.......

mix with yours
 
acha ukichaa, mwalimu anamzidi lini mhasibu?daktari? Kama unaongelea private sekta uko ni bargaining power wala mwenye akili timamu hawezi kulifikiria kwa kuwa hata sekretari wa kagoda ltd anamzidi msahara hata mtumishi wa hazina,ila ktk ngazi za govt.umechemka. Mwalimu kwa mapato hamfuati hata mhasibu msaidizi II. Na ukiongeza marupurupu ndo umewatenga kabisa,na overtime? We chunguza kwanza. Nakupa mfano mhasibu wa wilaya ana haki ya kuitumia gari ya STK ambayo hutumia DAS,yani district administrative secretary,mwl anapata usafiri huo?overtime?tuisheni au? Transport allowance kwenda na kurudi hazina hata ikiwa kila wiki? Je nauli kwenda na kurudi kutoka kwa mhasibu wa mkoa hata kama ni kila siku ktk majukumu? Hapa namuongelea mhasibu mdogo ktk ngazi za kiserikali,je mwl anaweza ayo? Sometimes we should call a spade a spade,mwl na mhasibu/daktari hawalinganishwi! Believe or reject!

Mimi nilimaanisha waalimu wa serikali. Nina data za baadhi ya waalimu, wahasibu, na madaktari. Tatizo lenu nyie ndo watu mnaowadharau waalimu kwamba hali yao ni ngumu huku mkiwa hamna data kamili. Mimi ninawafahamu wahasibu wa halmashauri za wilaya ambao maisha yao ni magumu kuliko baadhi ya waalimu wa shule za msingi. Fanya utafiti ujue watumishi wa serikali wanatofautiana vipi
 
kilichoanzwa kuonyeshwa na wabunge wa upinzani ni feedback ya nini walichokua wanamaanisha kuhusiana na serikali kupunguza matumizi yasiyokuwa ya ulazima na atleast kuokoa fedha ambazo zingetumika kusaidia kwenye sekta nyingine kama sekta ya afya, elimu na hata nishati ambazo kwa sasa zaonekana zahitaji kutizamwa kwa ukaribu wa hali ya juu. wanaopinga swala hilo la wabunge wa upinzani kutaka posho za wabunge zifutwe/kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, eti kwa kujinasibu kuwa hela inayookolewa ni kiasi kidogo sana ambacho kwa upeo wao eti hazina impact yoyote mimi nawaona ni kama viziwi wasioona!!!
watanzania tumeshazoea kuona/kusikia mamilioni ya shilingi yakitajwa basi ndio tujue kuwa ndio kiwango kikubwa kinachoweza kuleta maendeleo.!No,!hivi sh. 70,000/= kwa kila mbunge zaweza kutengeneza madawati mangapi kwa shule zetu za kata??? hizo posho posho zao haziwezi kununua vifaa vya uzazi kwa ajili ya akina mama na dada zetu at least kuboresha hali ya huduma za uzazi kwenye zahanati zetu???
hebu tuwe wazalendo wa-tz sisi, maana kama mtu anapewa posho kwa kazi ambayo ni ndani ya majukumu yake ya kikazi, swali ni je, tunamhujumu nani?
MUNGU IBARIKI TANZANIA...AMEN!!!!!
 
bora mgawane na jirani zako hata kikiwa kidogo,uchoyo ni dhambi.
 
MwanaCCM,
Mkuu wangu unapotoa hoja jaribu kuijenga kwa umakini na kuonyesha sababu ambazo wewe unapinga kutoka hoja iliyotangulia.

Kwa nini wananchi, Chadema na NCCR wanapinga posho hizi?.. ni kwa sababu Tunatumia karibu trillioni 1 kwa mwaka kulipia posho toka bajeti ya trillioni 13 hizi fedha ni zaidi ya asilimia 7, kwa hiyo ukitumia sijui Tsh 70,000 kwa kikao haina maana yeyote kama hutazingatia kwamba serikali imetenga kiasi gani kitumike.

Kisha hao hao viongozi wana vikao zaidi ya kimoja usidhani kwamba wanalipwa Tsh 70,000 tu, kiongozi anaweza kuwa na vikao vitatu hadi vinne toka taasisi tofauti za kiserikali tena akiwa mji anaoishi, sasa huu usafiri na malazi ktk hesabu ya Tsh 70,000 inatoka wapi?. Tunajua michezo yote ambayo huchezwa na viongozi kiasi kwamba baadhi yao posho pekee inazidi hata mishahara yao kwa mwaka.

Pengine unaweza kufikiria kwamba asilimia 7 ni ndogo sana lakini jaribu kuperuzi utazame serikali ya Mwalimu, Mwinyi na hata Mkapa walikuwa wakitumia asilimia ngapi ya bajeti kwa elimu au Afya, kisha utapata picha kamili kwa nini wananchi wanapiga kelele na hizi Posho.
 
Pia sisi wananchi tunapinga vikali posho za aina yoyote ile pamoja na ruzuku kwa vyama vya siasa. Ruzuku inayokwenda kwenye vyama vya siasa ni kubwa mno kwa nchi masikini kama Tz, nayo inapaswa kusitishwa mara moja.
 
Katika swala la ruzuku za vyama mkuu wangu hapa naomba unipe mahesabu yake kwa sababu lazima ukubali kwamba nia na lengo la ruzuku hizi ni kujenga demokrasia. Sasa sijui ni gharama gani inayopaswa kutumiwa ktk ujenzi wa demokrasia kwani pasipo fedha hizi vyama vitaanguka kirahisi. Binafsi siamini NCCR ilianguka kwa sababu ya kuondoka kwa viongozi wake pekee kuwa sababu ila waliangukia pua pale fedha za uendeshaji chama zilipopungua na wakashindwa kuwalipa hata wabunge walioshindwa. CUF pia ingekuwa ktk matatizo kama haya sema tu wabunge wa Zanzibar ndio wameokoa jahazi laa sivyo ndio ilikuwa imetoka.

Sema tu kwamba kuwepo na kiwango maalum cha ruzuku kwa vyama vyote nchini na CCM irudishe mali za Umma ili nguvu ya chama itokane na michango ya wanachama pamoja na wananchi sio CCM kutumia mali za Umma kufanya biashara haramu. Na hakika kama chama wapigwe marufuku kabisa kujihusisha na biashara.
 
Kwa hili natofautiana na Chadema na NCCR-Mageuzi, hapa wanatafuta umaarufu kwa bei chee, hivi mnafahamu kiasi wanachokigomea? posho ya kikao kwa taarifa yenu ni Tshs70,000 kwa siku, kwanini wasigomee Milioni90 za magari? Tusishabikie upuuzi NCCR sasa wanaonyesha hawana mwelekeo hiyo hoja ya Zitto ni ya kitoto sana, kama ana machungu na wananchi kwananini asigomee M90 au angechukua awapelekee. au tatizo liko wapi angepokea posho za vikao na angezipeleka kwa wananchi? Kwa wabunge wakomavu(wengi wapo CCM). Wanapokea hizo posho na wanawapelekea wananchi kimyakimya bila kujitangaza magazetini. Hata hivyo simlaumu sana zito nasikia kiumri bado ni kijana mdogo sana hivyo watu wazima tunawajibika kumshauri
Safari ni hatua...wakati hawa wameanza na jambo hilo, wengine hawakatazwi kuanza na jingine..kwani lengo si lile lile la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza kidogo tulichonacho katika sekta muhimu...Hata hivyo my take: Wabunge wetu wangekuwa waungwana na wangejijengea heshma duniani na akhera km wangeshinikiza walipe kodi (PAY AS YOU EARN) kutokana na mishahara yao kama ilivyo kwa waajiriwa wote nchini. Pia Mashangingi wanayokopeshwa wasikubali kulipia nusu ya mikopo yao, bali waonyeshe uzalendo wa kulipia kwa asilimia 100%, kwani wao si sawa na watanzania wengine??
 
Katika swala la ruzuku za vyama mkuu wangu hapa naomba unipe mahesabu yake kwa sababu lazima ukubali kwamba nia na lengo la ruzuku hizi ni kujenga demokrasia. Sasa sijui ni gharama gani inayopaswa kutumiwa ktk ujenzi wa demokrasia kwani pasipo fedha hizi vyama vitaanguka kirahisi. Binafsi siamini NCCR ilianguka kwa sababu ya kuondoka kwa viongozi wake pekee kuwa sababu ila waliangukia pua pale fedha za uendeshaji chama zilipopungua na wakashindwa kuwalipa hata wabunge walioshindwa. CUF pia ingekuwa ktk matatizo kama haya sema tu wabunge wa Zanzibar ndio wameokoa jahazi laa sivyo ndio ilikuwa imetoka.

Sema tu kwamba kuwepo na kiwango maalum cha ruzuku kwa vyama vyote nchini na CCM irudishe mali za Umma ili nguvu ya chama itokane na michango ya wanachama pamoja na wananchi sio CCM kutumia mali za Umma kufanya biashara haramu. Na hakika kama chama wapigwe marufuku kabisa kujihusisha na biashara.

CCM watakwambia wanafanya biashara ili kujenga demokrasia, pia wanaopokea posho watakwambia bila hiyo kitu hawatafanya kazi zao vizuri kwa masilahi ya Taifa.

Serikali inatakiwa kufumba macho, tunachotaka kujenga ni uchumi, na uchumi ukijengeka domokrasia by default itaji set yenyewe. Huwezi jenga domokrasia kwa watu walio masikini na wenye njaa kali, mtu mwenye njaa siku zote sio mstaarabu. Huwezi mhubiria mtu asichukue rushwa ya sh 500 wakati familia na watoto wanalia nyumbani kwa sababu hawajapata chakula siku kadhaa.
Domokrasia kwa watu walio ktk lindi la umasikini ni demokrasia kichaa. Serikali tunawaomba wafute ruzuku na posho zote na wazielekeze ktk masuala ya kujenga nchi kiuchumi.
Hizi pesa kwa pamoja zinatosha kutengeneza shamba moja kila mwezi lenye irrigation system ya kisasa na kuzalisha chakula kwa mwaka mzima ktk life span yake na kuondokana na njaa na bei ya chakula juu isiyo na sababu. Kwa mwaka tutakuwa na mashamba 12 na tena kwayo tutazalisha chakula ambacho tuta export kwa majirani zetu.

Posho na ruzuku zinapaswa kufutwa na zielekezwe ktk miradi ya maendeleo zaidi, badala ya kutupa hizo fedha kwenye miba wakati udongo mzuri upo.
 
Back
Top Bottom