NCCR-Mageuzi yaishauri Bunge kubadilisha Tozo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Siku chache baada ya Serikali kutetea tozo zinazotozwa kwenye miamala ya kielektroniki, Chama cha NCCR-Mageuzi kimeitaka wizara ya fedha na mipango pamoja na kamati ya bajeti kupeleka mswada wa dharura bungeni ili jambo hilo liangaliwe upya.

Septemba 1, 2022, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akitoa ufafanuzi wa tozo hizo alisema maoni na ushauri uliotolewa na makundi mbalimbali wameupokea na wanauganyia kazi.

Alisema tozo hizo zilizoanzishwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/22, zimekuwa msaada mkubwa kwa taifa kwa sababu zimesaidia kuchochea maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.

Septemba 6, 2022, Mjumbe wa Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam amesema Serikali haina jinsi zaidi ya kusikiliza kilio cha wananchi.

"Kwakuwa waziri wa fedha alisema Rais Samia Suluhu Hassaan amesikia kilio cha wananchi na kuelekeza wizara kupititia upya tozo hizi, tunaiomba wizara katika vikao hivi vya Bunge jambo hili likatekekezwe," amesema Selasini.

Amesema Rais Samia ni lazima kufuata utaratibu kwamba kuwa jambo hilo ni la kisheria na ilitungwa na kupitishwa na Bunge ambalo linatarajia kuanza vikao vyake Septemba 13, 2022.

"Jambo hili ni jambo zuri tunampongeza Rais na tunashauri hati ya dharura kupelekwa bungeni ili jambo hili lirekebishwe," amesema.

Selasini ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Rombo mwaka 2015-2020 aliwataka Watanzania kujitokeza na kutoa maoni kuhusiana na tozo hizo badala ya kuendelea kulalamika kwenye mitandao.

"Pamoja na kuumiza Serikali ilibuni chanzo hicho cha mapato kwa kuangalia ni namna gani watapata fedha kwaajili ya mipango ya maendeleo," alisema.

"Dhamira ilikuwa hivyo lakini imeleta sintofahamuna sio mara ya kwanza kwa Serikali kutafuta vyanzo vya fedha," amesema.
 
Back
Top Bottom