NCCR nao wakataa posho za vikao Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR nao wakataa posho za vikao Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, Jun 13, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  *Wabunge wake waandika barua nao wakatwe

  *Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema kuwa tayari kimeandaa barua ambazo kitaziwasilisha kwa waziri wa Fedha, Bw. Mustafa Mkulo kuelekeza posho za vikao kwa wabunge wanne wa chama hicho zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Kigoma.

  **Msimamo huo unaunga mkono hoja ya kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na Chadema ambayo tayari imeweka msimamo huo.

  *Pia wanapendekeza posho zote zikatwe kodi ili kuongeza mapato ya ndani kwa ajiri ya miradi ya maendeleo.


  Source: Majira Jumatatu juni 13 2011
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwa mtindo huu CCM hali itakuwa mbaya 2015
   
 3. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Magamba mpoooo
   
 4. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hili natofautiana na Chadema na NCCR-Mageuzi, hapa wanatafuta umaarufu kwa bei chee, hivi mnafahamu kiasi wanachokigomea? posho ya kikao kwa taarifa yenu ni Tshs70,000 kwa siku, kwanini wasigomee Milioni90 za magari? Tusishabikie upuuzi NCCR sasa wanaonyesha hawana mwelekeo hiyo hoja ya Zitto ni ya kitoto sana, kama ana machungu na wananchi kwananini asigomee M90 au angechukua awapelekee. au tatizo liko wapi angepokea posho za vikao na angezipeleka kwa wananchi? Kwa wabunge wakomavu(wengi wapo CCM). Wanapokea hizo posho na wanawapelekea wananchi kimyakimya bila kujitangaza magazetini. Hata hivyo simlaumu sana zito nasikia kiumri bado ni kijana mdogo sana hivyo watu wazima tunawajibika kumshauri
   
 5. P

  Pokola JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wewe jamaa bana!! But anyhow, vyovyote iwavyo, CCM jueni tu kuwa mshapigwa bao 2015!!
   
 6. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa kufikiria watu wenye mahitaji zaidi kadri mtu anapopanda juu na siyo kuwasahau.
  Ushauri wangu kuhusu posho hizi ni kwamba zikatwe ziwekwe halafu kwa muda maalumu ijulikane ni kiasi gani kimefikiwa na hapo wale waliokatwa waamue zitumikeje na wapi ili kuweka kumbukumbu ya shabaha yao na kuthibitisha kuwa kweli fedha hizi siyo negligible kama wengine wanavyodai na kama wabunge wote wangesamehe posho zao kikubwa zaidi kingeweza kufanyika kuleta maendeleo au kuboresha huduma kwa wananchi. Katika kuamua zitumike wapi kuna mtazamo wa kitaifa au kupelekwa katika majimbo wanakotoka wabunge husika. Baada ya hapo itakuwa rahisi zaidi mtu kuelewa tungrfaidikaje kama posho hii ingefutwa kote ndani na nje ya Bunge. Vinginevyo watu hawataona impact wazi wazi yenye kielelezo kutokana na wao kuacha kuchukua posho hii wakati wengine wanaendelea kuchukua.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mawazo ya kimakengeza sana haya
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SAKATA la kutaka kufutwa kwa posho za vikao nchi nzima zikiwamo za wabunge limezidi kupamba moto baada ya wabunge wa Chama cha NCCR-Mageuzi kutangaza kuliunga mkono.

  Aidha wabunge hao wamesema watamuandikia Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo na Spika wa Bunge Anne Makinda, wakitaka posho zao za vikao kuanzia sasa zipelekwe kwenye fungu la miradi ya maendeleo ya mkoa wa Kigoma.

  Pia wamesema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2011/2012 kipaumbele cha miundombinu hakina umuhimu sana kama ilivyo kwa elimu, nishati, afya na kilimo.

  Wamesisitiza kuwa pamoja na nishati kuwa moja ya vipaumbele vya kwanza katika bajeti hiyo bado fedha zilizotengwa katika kipaumbele hicho hazitoshelezi kufanikisha utekelezaji wa miradi ya nishati nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR) alisema wabunge wa chama hicho ambao wote wanatokea mkoa wa Kigoma wamekubaliana kutoa posho zao katika miradi ya maendeleo ya Kigoma ambapo kwa mujibu wake kila mwaka mkoa huo hutengewa kiasi kidogo cha fedha za ndani za maendeleo ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.

  Hivi karibuni akiwasilisha mwelekeo wa bajeti ya Kambi ya Upinzani kwa waandishi wa habari, Waziri Kivuli Zitto Kabwe(Chadema) alisema moja ya mkakati wa kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Serikali ni kufuta posho za vikao, jambo ambalo liliungwa mkono na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe (Chadema) pamoja na wabunge wa chama hicho.

  Alisema kwa upande wa wabunge wana malipo ya aina tatu ambayo ni mshahara, fedha za kujikimu wakiwa na majukumu ya kujikimu nje ya maeneo yao ya kazi na posho za vikao ambapo aliongeza kuwa katika fedha zote hizo fedha ya posho za vikao haina maana yoyote.

  “Kwa sababu mshahara upo, ukiwa Dodoma au Tanga ilimradi ni nje ya eneo lako la kazi unapewa fedha ya kujikimu, sasa tena posho ya vikao ya nini, ndio maana tunasema si halali,” alisema.

  Alisema kwa wabunge wanne wa chama hicho kwa siku hulipwa posho ya Sh 70,000 hivyo jumla ya fedha zote za wabunge hao kwa siku ni Sh 280,000 ambapo kwa siku 10 itakuwa ni Sh milioni 2.8 hivyo kwa muda wote watakaokaa bungeni watachangia kiasi kikubwa cha fedha katika miradi ya maendeleo ya Kigoma.

  Alisema, mkoa wa Kigoma umekuwa ukipata fungu dogo la miradi ya maendeleo kwani hupata asilimia 27 tu ya fedha za matumizi ya ndani wakati mkoa wa Dar es Salaam pekee hupatiwa asilimia 47.

  Kafulila alisema, katika kusisitiza juu ya mfumo mzuri wa matumizi ya fedha za Serikali, chama hicho kitapendekeza bungeni kufutwa kwa nafasi ya mkuu wa wilaya na makatibu tarafa nchini kwa kuwa nafasi hizo ni za kisiasa na zinaingilia wajibu wa wakurugenzi na wabunge.

  Akizungumzia bajeti alisema, imeelemewa na madeni makubwa, misaada na mikopo na hivyo kuifanya bajeti hiyo kuwa tegemezi.

  “Inasikitisha taifa lenye deni la Sh trilioni 11 bado tunazalisha umeme wa megawati 800 wakati robo ya deni hilo ingetosha kuzalisha megawati 3000 ambazo zimeingizwa kwenye mikakati ya Mpango wa Maendeleo ya miaka mitano.

  Alisema suala la kuendelea kulilia misaada kwa wahisani ni aibu kwa Tanzania kwa kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa nchi saba zinazopewa misaada kwa wingi duniani, baadhi ya nchi nyingine ni Ethiopia, Sudan, Iraq na Afghanistan ambazo hupatiwa misaada hiyo kwa wingi kutokana na vita na hali mbaya kiusalama. “Ndio maana nasema ni aibu Tanzania yenye amani kusaidiwa sawa na mataifa yenye hali tete ya kiusalama.

  Aidha alisema bajeti ya umeme haitoshi ikilinganishwa na bajeti za nyuma za umeme. Alisema mwaka 2006/2007 sekta ya umeme ilitengewa asilimia 24, 2007/2008 ilitengewa asilimia 13.9 na mwaka 2008/2009 asilimia 12 wakati katika mwaka huu wa fedha 2011/2012 miradi ya maendeleo imetengewa Sh bilioni 4.9 na umeme nishati na madini Sh bilioni 530 ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya fedha za miradi ya maendeleo.

  Kwa upande wake, mbunge wa Muhambwe Felix Mkosamali (NCCR) alisema baada ya kuwasilisha leo barua kwa Spika pia watawasilisha hoja ya kujadili kifungu cha Sheria kinachozungumzia posho za wabunge na kupendekeza kibadilishwe.
   
 9. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 10. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nimeona kwenye taarifa habari channel 10,Nimeipenda sana.
   
 11. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Something is far more better than nothing!!!! Hao wabunge wa CCM wamegomea Shilingi ngapi???? If you cant say something good about somebody.... Shut the hell up!!!
   
 12. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Nice move.
   
 13. m

  mwanza JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Acha kuchanganya mambo million 90 unazosema si posho bali ni mkopo ambao mbunge anakopeshwa nahuwa anakatwa kwenye mshahara wake na posho wanayokataa ni pesa ambayo mbunge analipwa kwa kazi ileile aliyotumwa na wananchi nakulipwa mshahara nandio Zitto ameikataa
   
 14. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mbaha, Heshima yako mkuu, ni kweli big things start with small things, kama wewe si muaminifu kwa mambo madogo, hakika makubwa huyawezi. Zitto and chadema have shown the way, you never know this may be just the beginning of equality in distribution of national cake. For long time national cake has been right of just few and advantaged Tanzanians while the majority wilt in absolute poverty. These are important milestones indicating that we are now starting heading in a right direction. I have a dream that this nation will rise again against the injustice done by our leaders.
  Go ZItto, go Chadema, go NCCR, go Tanzanians.
  God bless us all
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Elfu sabini ndogo? Unafahamu take home ya mshahara wa walimu?
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Kumbe mtu mzima!!!

  Sa mbona hoja unajenga za kidato cha pili?
   
 17. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wewe kweli kilaza. Kwa taarifa yako 70,000 X Idadi ya wabunge ni 357 =24,990,000 (sawa na Mil25) kwa siku. Hesabu hii haijumlishi idadi ya watumishi wa bunge ambao nao hulipwa posho pamoja na kuwa Dodoma ni mahali pao pa kazi.

  Unazungumzia Mil 90 za magari: Kwanza tuweke mambo sawasawa. Kuwa na usafiri kunmwezesha mbunge kuweza kuwafikia wapiga kura wake kwa urahisi. Hata hivyo wabunge wa upinzani walishasema kuwa haiihitajiki kununua magari ya gharama (landcruiser VX). Ila kwa kiburi cha serikali yetu wameendelea kununua magari hayo. Ikiwa Zitto kawaelekeza walipe pesa za posho kweye account ya KDI wamekataa, unafikiri wangesemaje kuhusu magari? Naomba kurudia: Usafiri si anasa - unamsaidia mbunge kuwafikia wananchi. Hoja tunayopaswa kuzungumza ni magari ya aina gani kwa bei nafuu kiasi gani.
   
 18. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  acha porojo zako wewe,hizo ni pumba zisizokuwa na msingi.fikiri kwanza.
   
 19. delabuta

  delabuta Senior Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha kuwa mjinga Tshs.70,000 x 350 =24,500,000.00 haziwezi kuleta mabadiliko hata kwenye wizara ya afya nadhani na wewe ni mmoja wa hayo magamba na ndio maana umekuwa kipofu na kiziwi. pole zako fisadi wewe.
   
 20. delabuta

  delabuta Senior Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hoja ya zitto ni ya kitoto toa yako ya kikubwa tuione na tuisikie.
   
Loading...