A
Anonymous
Guest
Naandika kwa masikitiko makubwa juu ya utaratibu wa kusajili kampuni ndogo za kutoa huduma ya Uhasibu kwa Umma hususani kwa watoa huduma wadogo (Small firms).
Pamoja na viambatisho vingi vinavyotakiwa kuwasilishwa NBAA muombaji anatakiwa pia kuwasilisha cheti cha usajili kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambacho kinatolewa na Mamlaka ya Mapato, lakini ikumbukwe kwamba ili uweze kupata cheti cha VAT lazima upeleke ushahidi wa kwamba umesajiliwa kutoa huduma za kitaalam yaani (professional service)
Eneo la pili ni lazima uwasilishe mkataba wa mashirikiano na firm ambayo imekwishasajiliwa (Affiliated firm) na hakuna utaratibu mzuri uliowekwa hivyo kulazimika kutoa fedha nyingi au wakati mwingine kukata tamaa binafsi nimetakiwa kutoa Milioni mbili kupata hiyo barua
Eneo la tatu usiwe umeajiriwa popote na wakati huo huo wanataka ushahidi wa kuwa umeajiri watu si chini ya wawili kabla hata hujasajiliwa sasa unajiuliza hawa watu wana kazi gani? Je kufungua biashara ni kwa wasio na ajira pekee?
Nadhani kuna fikra tunahitaji kuzibadilisha kama kweli tunataka fani hii ipige hatua