Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,988
- 142,393
Pengine hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya wengi wao kufeli. System mzima ya mitihani ya NBAA/CPA imeundwa kwa watahiniwa ambao wana experience ya accounting field angalau ya mwaka mmoja. Sasa kutoka fresh-from-school mpaka ku-tackle hiyo mtihani kunaweza kuwa ni mlima mmoja mrefu sana kuupanda.
Pia tusisahau kuwa mitihani hiyo iko very intimidating. Unaweza kujiandaa vilivyo, lakini jinsi mazingira ya mtihani yalivyowekwa, ni rahisi 'kuwehuka.'
Nakumbuka nilivyo-sit for CPA exam (U.S. system), nilipata headache moja ya nguvu sana. Tena afadhali siku hizi, mitihani iko computerized na wanakuruhusu kufanya one part at a time. Mimi nili-sit mtihani wa mwisho wa paper-and-pencil (Nov. 2003). Yaani ilikuwa unafanya part zote nne kwa wakati mmoja (Sat and Sun: 8am - 5pm). Kamwe sitosahau weekend ile.
Kufuata watasha ni kansa kwetu ukiangalia mfumo wa elimu toka msingi mpaka chuo ni madudu ya wazungu tu.lakini basi tuwajue wazungu(CPA) kwanza ili nasi tujijue kama hatutajua hata kanuni za Debit na Credit za wazungu sidhani kama tutaweza kuwa na zetu..
Maswali yako sibishi kitu na yanahitaji thread nyingine ya mfumo wa elimu walitaka kuanza kufundsha vyuo vikuu kwa kiswahili...........sijui yaliishia wapi BTW mfumo wetu africa ni tegemezi.....
Hahahahaaaa...Mazee sasa hapo unataka ku impress watu au? Maana ni kama unasema wewe ni CPA (even though you didn't specifically say that)....sawa bana mi ngoja niendelee na janitorial work yangu hapa....
Ha ha haaa...ingefaa ungeniuliza kama nili pass kwanza kabla hujanipiga dongo....lol
Hapana NN, mimi sio CPA. Nilichemsha vibaya mno. Nilipass parts mbili na nikavutwa parts mbili. Sijui siku hizi system ikoje, lakini wakati huo, ili upass CPA ulitakiwa kupata at least 75% kwa kila part. Na kama umepata chini ya hapo kwa angalau part moja, utapaswa kurudia ile part uliyofeli ONLY, kama umepata angalau 50%. Chini ya hapo utapaswa kurudia parts zote (including zile ulizopata 75% au zaidi). Sasa mimi, moja ya parts nilizofeli nilipata 42% (ile nyingine nilipata just over 50%), basi nikapaswa kurudia parts zote. Nikaona upuuzi....kwani hata ukibeba boksi utapata paycheck vile vile.
Sina uhakika kama sasa hivi pia wana vitabu maalum.....Kwa harakaharaka matatizo ya CPA kwawakati huo ni kama ifuatavyo:
1- Kulikuwa hakuna vitabu maalum kwa mitaala ya CPA ukilinganisha na wenzao wa ACCA.
.
Muulize Shazulu faida za CPAHivi kwa nini watu wengine wanaona CPA kuwa big deal?
Hivi kwa nini watu wengine wanaona CPA kuwa big deal?
Hili tatizo solution yake nini?
CPA inafanywa kama tiketi ya kwenda Mbinguni ambayo vizee pale NBAA ndio vinatoa ruhusa......Shonge analysis yako nimekubali lakini pamoja na hayo yoote sidhani kama ndio haswa sababu ya kufeli more than 80%.....kwa taarifa yako ni kuwa wengi wanaofanya CPA siku hizi hawapo kazini ni vijana wenye Adv Diploma na Degree za accountancy ambao wengi wao hawan kazi so wako busy na kusoma tu tangu wamalize chuo....
Mbona Open Univer wanafunzi wake wengi ni wafanyakazi lakni hawafeli namna hii......ukweli ni kuwa vile vizee vina roho mbaya vikiona kijana under 30 anakula CPA uku wenyewe walisotea miaka zaidi ya 20......
Pia suala la kuchoshwa sio mkuu nasikia majuu watu wanabeba box masaa kibao an wanakula buku na wanafaulu iweje Tz isiwezekane?
Kijana ume spesholaizi kwenye fani gani?
Umewahi kusoma tz elimu ya juu?
kuna watu wamegraduate juzi but wakifanya CPA wanapass modole E wakija F lazima wakamatwe
Belo nadhani hapa hauko informed vya kutosha. In fact kwa CPA [T] (final stage) syllabus ya sasa [current] ni rahisi ku'clear' [kufaulu] module F kuliko kufaulu module E.
wabongo tunakariri na CPA hawataki kukariri wanataka kupata Mamenager ambao wataleta manufaa kwenye taasisi Mtu unaulizwa Function za Interna Auditor General ni nini? wewe unaanza kukariri badala ya kutoa self explanational za kitaaluma then wewe unaanza kukariri kwa Mfano MA maswali yanahitaji uelewa and assumtion zako na individual skills na conclution jitu linatoa micalculation tu linaacha wazi so wewe ni manajor utakuwa unatengeneza cost control report then unaidistribute to kwa board of director bila kutoa ufafanuzi kamili sasa wakupe CPA ukavurunde na unajua ya kuwa CPA ndo mambo yote Tanzania Jamani Wabongo Acheni Taaluma na Siasa yasitukute ya shule za kata Jamani.