Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Kama umepita shule hizi hapa tanzania,basi we tayari uko kwenye jeshi la akiba,maana maisha ya huko na jeshni hayana tofauti.
lyamungo
umbwe
old moshi
mara sec
musoma tech
iyunga tech
magamba
ndanda
tosamaganga
kilimanjaro boys
same
kibiti
pugu
minaki
mirambo
songea boys
Ongeza na Kwiro boys
 
Maputo ukitoka huko lazima uvue nguo kwanza na kukaa nje kidogo lasivyo ukiingia class kila mtu anajua umetoka toilet.

watu kuoga na kupendeza siku ya Soko la Kombo

Sijui kama mliikuta hii Advance waliandika barua umbwe kuomba Vita na Uwanja wa Vita uwe Mlama desert hii ni baada ya Umbwe kuanza kututangazia shule mbalimbali za Wasichana kama Machame,Mawenzi,Weruweru kuwa Sisi hatupendi kuoga ni wachafu ila umbwe walikataa hii vita.

kuvua samaki wa shule fishpond na neti siku za jumamosi walimu hawapo shuleni.

kuna sehemu iliitwa makaburini sijui chanzo cha jina hili ni nn

Siku za graduation Machame shule nzima inahamia machame kisa kuna umoja unaitwa Lyamacha.

Kiongozi wa chakula kuchukua nyama kwenye kindoo na kuenda kuuzia wenzake kinyango shs 200 nani lazima ununue na sio ombi.

Lyamungo ile ilikua ni kama Guantanamo bay au chuo cha kijeshi ukipita pale hata jangwan utaishi.
Hahaha kweli Kwiro kulikuwa na fujo sana ila nahisi lyamungo ni zaid
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Mwaka gani mkuu hii?
Hiyo ilikua 2004 mwanzoni kabisa, Hm Bureta alikua nje ya nchi akaja akaikuta skendo hiyo na shule alikua amemwachia second master Mr. Marenge na kina mugogo. Nooomaa sana kipindi hcho
 
Mimi nilifundisha hesabu Lyamungo 1975 hadi 1977 (Enzi za Mtui na Livigha). Shule ilikuwa yakistaarabu sana. Ila nikiri swimming pool ilionekana na kuanza kutelekezwa. Shughuli au elimu ya kilimo ilikuwa inakwenda vizuri kwa hiyo msosi fresh ilikuwepo.

Suala la ubabe na mateso nakubaliana na wewe kwa sababu utaratibu wa nidhamu ulipewa maana tofauti si mashuleni (sector ya elimu) pekee bali serikalini kote.

Samahani lakini ukweli nitausema 1977 kilizaliwa chama cha mapinduzi kipindi hicho hicho jumuia ya Africa ya Mashariki ilikufa. Kulikuwa na vuguvugu la vita na Uganda. Kisiasa chama kilishika hatamu. Kwa hiyo kulikuwa na mambo na changamoto nyingi sana.

Ikafuatia kufunga mikanda kwa maana ya changamoto za uchumi. Unaweza kujiuliza haya yana uhusiano gani na hoja yako. Kifupi yana uhusiano

1. Yako siyo isolated case ni hali ya taifa zima hususan kielimu kwa kukosekana kusustain ideals za matakwa ya kielimu.

2 Kushindwa kuhimili changamoto za nabadiriko . Kitaalam tunasema failure ya kumanage transition. Hili linatuathiri hadi leo.

3. Ile shule ilikuwa ya KNCU mchepuo wa Kilimo. Lakini ilipinduliwa kusudio la awali na kurundikiwa jukumu lisilofanana na mazingira. Kwa hiyo kulihitajika usimamizi madhubuti ambao haukuwepo na hautakuwepo.

Faida uliyopata moja ni ukomavu unaweza kukabiliana na mazingira yo yote magumu.

Hata hivyo nakupongeza maana umepikwa na tanuru la changamoto. Natumaini huna kinyongo maana umevuka ukiwa ngangari. Ila kwenye maisha kuna changamoto zaidi ya hizo za Lyamungo.

Naipenda Lyamungo ya KNCU
Unamkumbuka Mwalimu George Mushi Kimboka
Alipotelea lyamungo mpaka Leo atujawai kumuona
Ni baba yangu mkubwa
Pia kaka zangu mabinamu Zangu walikuwa wanasoma umbwe miaka hiyo waliniadisia Kuwa lyamungu walikuwa wakicheza Mpira na kibohehe
Pakatokea ogomvi mkubwa
Kibohehe walipoondoka wanafunzi waliyamungo walipokwenda kuoga
Kibohehe wakarudi Kimya Kimya wakawavamia wapishi Jikoni wakabeba masufuria ya nyama yote
Unaikumbuka hii
Sisi kwetu mango
 
Nimesoma maeneo ya jirani na Lyamungo,hakika mtoa mada umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa tunakuja sana kila jumamosi kupata da'awa kutoka kwa maustaadh wa Lyamungo,walikuwa wanatupikia vizuriiiiii wali maharage
Hahahaaaaaa

Yote uliyoyasema ni kweli kabisa.
I miss those days
Safi Sana kumbe wakwetu jamani
 
hivi wale machalii waliopandishwa kwenye mando ya Burieta(mkuu wa shule enzi hizo) wapo hapa? walepelekwa pale Lyasikika kisa wasichana wa Lyasikika walienda kuwasemea vijana wa lyamungo wanawatongoza kwa nguvu. iligongwa kengele wale mabinti wa shule jirani wakaambiwa wapite kukagua sura moja baada ya nyingne....
bureta kwasasa n kamishna wa elimu
 
VURUGU KUBWA SHULE YA SECONDARI LYAMUNGO LEO HII TAREHE 1 MARCH 2018 HALI SII SHWARI

Hali sio shwari hata kidogo katika shule ya sekondari Lyamungo iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kilichopelekea mkuu wilaya ya Hai kufunga shule hiyo kwa muda kukwepa hasara zaidi, huku ofisini ya mwalimu wa nidhamu na ofisini ya mkuu wa shule vikiharibika vibaya sana.

Vurugu hizi zilianza katika uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo mwanafunzi mmoja mtukutu aliwatukana waalimu na wanafunzi wa shule katika kura alizopiga. Uongozi wa shule pamoja na walimu walishirikiana kubaini mwandiko wa mwanafunzi huyo, ndipo ugomvi ulipoanzia Kitendo cha uongozi wa shule kumfukuza shule mwanafunzi huyo ndio chanzo cha vurugu zote hizo.



C $ P GROUP LINGINE LA POLISI [emoji121][emoji121]
 
Umenikumbusha mbali nimesoma hapo o-level 2007-2010 . Kweli ile shule imenipa ukakamavu sana ilikua ni zaidi ya jeshi.Ila nimemkumbuka mzee Manase na Massawe wale wazee walitulea sana. Ila vita ya Lyamungo na Umbwe ndo sitakaa niisahau mkuu ndo siku niliyoshuhudia mtu akikata moto live.Ila zile changamoto za pale viongozi walipewa Madaraka makubwa mno na waalimu mpaka kuunda (JV) , Jeshi la Viranja.Daaa sitasahau aisee ni balaa.
Amani iwe nanyi ndugu zangu.

Leo nimeona niwaelezee japo kwa ufupi mateso nliyokumbana nayo ktk shule ya wavulana Lyamungo iliyopo wilaya ya hai mkoa wa Kilimanjaro.

Enzi za utawala:-
-Gervas.
-Wandiba.
-Mtera.

Nilipojiunga kidato cha kwanza nilipokelewa na waalimu na kupangiwa bweni la Agrey, wakati napelekwa bwenini nlisikia sauti zikiuliza kama nimebeba Mbuzi (mkate) na wengine kuulizia nimebeba dekio (kumbe kazi ya kidato cha kwanza ni kudeki shule nzima).

Usafi: Bweni letu (yote manne: Aggrey, Shaban robert, Lumumba na Amri Abedi) yalikuwa ni ghorofa moja lenye vyumba ishirini (kumi juu na kumi chini). Kazi ya kudeki bweni ilikua ni form one hivyo tulipangiwa vyumba viwili, kimoja juu na cha pili chini kudeki kila siku saa nne usiku baada ya prep.

Kulikuwa na utaratibu wa kumwagwa maji bweni zima na kikundi kilichoitwa "mwaga-maji" kisha ndo tuanze kudeki wakati mwingine bila taa na ukidek juu ukienda chini, juu maji yashaingia kweny chumba tena.

Mara nyingi tuliamshwa saa nane usiku na kulazwa sakafuni kisha kumwagiwa maji na kupigwa mikanda kisa hatujadeki vizuri. Tulikata tamaa na shule.

Jukumu la kudeki kordo za shule nzima lilikua la kwetu pia, hivyo tulikua kama watumishi wa shule na ikipita siku bila kupigwa vibaya unashukuru Mungu.

Kuna wakati tulipigwa marungu ya migongo mpaka kuvimba huku wengine wakiingizwa kwenye masink yenye utelezi wa kijani (fangasi), mabaki ya chakula na kufunguliwa bomba za maji.

Nilipochoka mateso hayo niliamua kuomba kazi kweny mradi wa Ng'ombe ambapo tulikua tukizoa mbolea na kuchunga ng'ombe siku ya Jumamosi, wengine walikua kwenye mradi wa nguruwe.

Chakula: Shule ilikuwa na Wanafunzi zaidi ya 3000 na utaratibu wa kula ilikua ni kwa mstari, tulipigwa sana mikanda kutokana na vurugu za mstari na tulikua wa mwisho kula. Mara nyingi tulikosa chakula au tulipata ugali na kukosa mboga.

Mzee Manase (Zizu) alikua mpishi katili sana, akiwa kwenye foleni kabla hujafika kwenye sufuria ashakurushia ugali uudake sasa ole wako uanguke chini. Huyu mpishi akigawa haangalii sura ila ole wako urudie chakula lazima akudake mkono na kichapo kizito. Alipenda kutukana sana. Wengine ni mzee Urasa na Mzee mwingine wa kijiji cha Narum.

Vijana toka kanda ya ziwa walikua vinara wa kula sana, walikua wakiitana "tuigonge" maana watatu wanaweza gonga dish zima la msosi. Tuliwaheshimu sana kwa kula yao japo hawakua smart.

Viongozi Miungu: Viongozi wa serikali ya wanafunzi walikua miungu watu.
Head boy alikuwa Isaya na makamu wake Lema. Waziri wa chakula Saika na wengine. Hawa walikua wakifanya kila walichotaka na walipiga hata kwa nondo bila kuhojiwa na mtu. Mpaka walimu waliwaogopa tokana na karate uchwara zao.

Viongozi walikuwa wakiagiza vitu mgahawani bila kukupa hata cent na ole usilete utatafuta pa kulala.
Wengi walipata majeraha na kugeuka kama majangili.

Wizi: Hii ilikua ni sehemu ya maisha, vijana walevi walikua wanakupora huku unaona. Mtu akilewa anakuja saa saba usiku anabeba tranka lako huku unamwangalia anaelekea nalo msituni kulivunja. Ukimfwata anaweza kuchoma kisu, lilinipata hilo japo hawakufanikiwa kuiba simu walodhani ipo ktk sanduku.
Simu, discman na vifaa vingine vya thamani vilikua vikiibiwa kupita kiasi na viliuzwa Moshi mjini.

Nidhamu: Kulikua na makundi mengi sana ya kihuni yaliyojihusisha na uvutaji bangi, wizi, ubabe nk. Vikundi kama Ragamafi, jumba la dhahabu nk. Kila kikundi kilikua na viongozi na hakikutaka kuonewa hali iliyopelekea baadae shule kufukuza kidato cha tatu na nne wote tokana na machafuko ya mara kwa mara.

Uhasama na Umbwe sekondari: Hizi zilikuwa ni shule mbili za wavulana zilizokuwa zikioneshana ubabe na wakati mwingine kuvamiana na kutwangana. Baadhi ya wanafunzi waliuwawa ktk uvamizi uliokua unafanywa.

Pia wezi kutoka uraiani kuuwawa ilikuwa ni jambo la kawaida sana. Hali hii ilitunyima hata uhuru wa kutembea kijijini.

Maandamano: Kuna siku alifariki mwanafunzi mwenzetu kwa uzembe wa kimatibabu, tuliamshwa saa kumi asubuhi tukaanza maandamano 25 km mpaka Moshi mjini. Tuliziba upande mzima wa barabara na ilibidi wakati wa kurudi tukodishiwe fuso za kuturudisha maana idadi yetu ilikuwa kubwa mno.

Vita kati ya Advance na O-level: Hakika tulikua hatupendani hata kidogo, mara kwa mara yalizuka mapigano kati yetu na tulitumia silaha kama mawe, mafyekeo, majembe nk.

Polisi wa Boma ng'ombe walikua na wakati mgumu kutuliza fujo zilizokua zikitokea usiku wa manane. Wengi tulilala mashambani kuokoa maisha yetu.

Mahudhurio darasani: Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi mahudhurio hayakuwa mazuri. Nakumbuka kidato cha pili tulikuwa 500 na tuliwekwa ktk mikondo mitano (J,K,T,U, na V). Niliwahi kuandikishwa barua na mkuu wa shule kwa kutoonekana darasani miezi mitano kwani hata mwalimu wa darasa alisema hanifahamu na hajawahi kuniona.

Kidato cha 3 na 4 kufukuzwa shule: Kutokana na nidhamu mbovu kulitokea ugomvi mzito baina ya makundi ya wahuni na viongozi ambao ulipelekea hasara kubwa na shule kufungwa kwa muda. Kila mwanafunzi ililipa faini ya sh.9000/= na baada ya hapo kidato cha 3 na 4 tulifukuzwa wote na kupewa ofa ya kuhamia shule yeyote ya kata.

Tulipakana na shule kama: Lyaskika, Somsom, Narum nk ambapo tulikua tunapoozea mioyo kwa mabinti wa shule hizo.

Waweza ongeza lolote kwa uliyepitia mambo hayo:


View attachment 441650
 
...keleeeuwiiii aisee mmekuta shule tamu namna hii mamamammamamamaaaaaa...enzi hizo Lyasesco tunavaa suruali za kaki papaa...ni mwendo wa kilimo mwanzo mwishoooo, unaeza kata tamaa ukaona elimu haina umuhimu aisee...kilichonikimbiza hapo ni pale nilipougua apendex bila msaada wowote asee..nikatemana nao hah hah kipindi hiko ilikubidi uwe na roho ngumu ili uweze ku-master mazingira la sivyo unarudi home papaa...si mchezo
Wewe mshkaji itakua tulikua class moja class of 2010
 
hivi wale machalii waliopandishwa kwenye mando ya Burieta(mkuu wa shule enzi hizo) wapo hapa? walepelekwa pale Lyasikika kisa wasichana wa Lyasikika walienda kuwasemea vijana wa lyamungo wanawatongoza kwa nguvu. iligongwa kengele wale mabinti wa shule jirani wakaambiwa wapite kukagua sura moja baada ya nyingne....
Buretta aliyekuja kuwa kamishina wa elimu au?
 
VURUGU KUBWA SHULE YA SECONDARI LYAMUNGO LEO HII TAREHE 1 MARCH 2018 HALI SII SHWARI

Hali sio shwari hata kidogo katika shule ya sekondari Lyamungo iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kilichopelekea mkuu wilaya ya Hai kufunga shule hiyo kwa muda kukwepa hasara zaidi, huku ofisini ya mwalimu wa nidhamu na ofisini ya mkuu wa shule vikiharibika vibaya sana.

Vurugu hizi zilianza katika uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo mwanafunzi mmoja mtukutu aliwatukana waalimu na wanafunzi wa shule katika kura alizopiga. Uongozi wa shule pamoja na walimu walishirikiana kubaini mwandiko wa mwanafunzi huyo, ndipo ugomvi ulipoanzia Kitendo cha uongozi wa shule kumfukuza shule mwanafunzi huyo ndio chanzo cha vurugu zote hizo.



C $ P GROUP LINGINE LA POLISI [emoji121][emoji121]

Ila mods wakati mwingine mnanisikitisha

Sasa hii post na mada ya huu uzi unaendeanaje?
Mtu akitaka kupata info latest mnafikiri atasema arudi hadi 2016? Or akiona mada ya huu uzi mnafikiro atafikiria kuna habari ingine ya hiyo shule ya mwaka huu kuwemo humu?

Mjue sio watu wote usoma hadi mwisho wa uzi.. first page ndio usomwa zaidi labda kitu kimvutie mtu ndio ataendelea pages zinazofata

Mnaipotezea sana hii forum na kuunganisha kwani inapunguza nini haswa.. maandishi si yale yale yamo bado kwa forum.. duh

Anyway huwa hamchukui ushauri wa hili jambo
 
Kama umepita shule hizi hapa tanzania,basi we tayari uko kwenye jeshi la akiba,maana maisha ya huko na jeshni hayana tofauti.
lyamungo
umbwe
old moshi
mara sec
musoma tech
iyunga tech
magamba
ndanda
tosamaganga
kilimanjaro boys
same
kibiti
pugu
minaki
mirambo
songea boys

Ongezea Chidya
 
Kijana naona umenitaja eti nilikuwa na karate uchwara, usinijaribu( in ......voice). Nitakuchukua nikakuzamishe kwenye mfereji wa uwanja wa mpira. Dah! Lyamungo!

Haha!, nasikia mkubwa Isaya ni head master siku hizi sipatii picha hao madogo labda kama kaacha ubabe yule jamaa sitamsahau japo kanisaidia sana mambo mengi
 
Back
Top Bottom