Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,784
4,097
Amani iwe nanyi ndugu zangu.

Leo nimeona niwaelezee japo kwa ufupi mateso nliyokumbana nayo ktk shule ya wavulana Lyamungo iliyopo wilaya ya hai mkoa wa Kilimanjaro.

Enzi za utawala:-
-Gervas.
-Wandiba.
-Mtera.

Nilipojiunga kidato cha kwanza nilipokelewa na waalimu na kupangiwa bweni la Agrey, wakati napelekwa bwenini nlisikia sauti zikiuliza kama nimebeba Mbuzi (mkate) na wengine kuulizia nimebeba dekio (kumbe kazi ya kidato cha kwanza ni kudeki shule nzima).

Usafi: Bweni letu (yote manne: Aggrey, Shaban robert, Lumumba na Amri Abedi) yalikuwa ni ghorofa moja lenye vyumba ishirini (kumi juu na kumi chini). Kazi ya kudeki bweni ilikua ni form one hivyo tulipangiwa vyumba viwili, kimoja juu na cha pili chini kudeki kila siku saa nne usiku baada ya prep.

Kulikuwa na utaratibu wa kumwagwa maji bweni zima na kikundi kilichoitwa "mwaga-maji" kisha ndo tuanze kudeki wakati mwingine bila taa na ukidek juu ukienda chini, juu maji yashaingia kweny chumba tena.

Mara nyingi tuliamshwa saa nane usiku na kulazwa sakafuni kisha kumwagiwa maji na kupigwa mikanda kisa hatujadeki vizuri. Tulikata tamaa na shule.

Jukumu la kudeki kordo za shule nzima lilikua la kwetu pia, hivyo tulikua kama watumishi wa shule na ikipita siku bila kupigwa vibaya unashukuru Mungu.

Kuna wakati tulipigwa marungu ya migongo mpaka kuvimba huku wengine wakiingizwa kwenye masink yenye utelezi wa kijani (fangasi), mabaki ya chakula na kufunguliwa bomba za maji.

Nilipochoka mateso hayo niliamua kuomba kazi kweny mradi wa Ng'ombe ambapo tulikua tukizoa mbolea na kuchunga ng'ombe siku ya Jumamosi, wengine walikua kwenye mradi wa nguruwe.

Chakula: Shule ilikuwa na Wanafunzi zaidi ya 3000 na utaratibu wa kula ilikua ni kwa mstari, tulipigwa sana mikanda kutokana na vurugu za mstari na tulikua wa mwisho kula. Mara nyingi tulikosa chakula au tulipata ugali na kukosa mboga.

Mzee Manase (Zizu) alikua mpishi katili sana, akiwa kwenye foleni kabla hujafika kwenye sufuria ashakurushia ugali uudake sasa ole wako uanguke chini. Huyu mpishi akigawa haangalii sura ila ole wako urudie chakula lazima akudake mkono na kichapo kizito. Alipenda kutukana sana. Wengine ni mzee Urasa na Mzee mwingine wa kijiji cha Narum.

Vijana toka kanda ya ziwa walikua vinara wa kula sana, walikua wakiitana "tuigonge" maana watatu wanaweza gonga dish zima la msosi. Tuliwaheshimu sana kwa kula yao japo hawakua smart.

Viongozi Miungu: Viongozi wa serikali ya wanafunzi walikua miungu watu.
Head boy alikuwa Isaya na makamu wake Lema. Waziri wa chakula Saika na wengine. Hawa walikua wakifanya kila walichotaka na walipiga hata kwa nondo bila kuhojiwa na mtu. Mpaka walimu waliwaogopa tokana na karate uchwara zao.

Viongozi walikuwa wakiagiza vitu mgahawani bila kukupa hata cent na ole usilete utatafuta pa kulala.
Wengi walipata majeraha na kugeuka kama majangili.

Wizi: Hii ilikua ni sehemu ya maisha, vijana walevi walikua wanakupora huku unaona. Mtu akilewa anakuja saa saba usiku anabeba tranka lako huku unamwangalia anaelekea nalo msituni kulivunja. Ukimfwata anaweza kuchoma kisu, lilinipata hilo japo hawakufanikiwa kuiba simu walodhani ipo ktk sanduku.
Simu, discman na vifaa vingine vya thamani vilikua vikiibiwa kupita kiasi na viliuzwa Moshi mjini.

Nidhamu: Kulikua na makundi mengi sana ya kihuni yaliyojihusisha na uvutaji bangi, wizi, ubabe nk. Vikundi kama Ragamafi, jumba la dhahabu nk. Kila kikundi kilikua na viongozi na hakikutaka kuonewa hali iliyopelekea baadae shule kufukuza kidato cha tatu na nne wote tokana na machafuko ya mara kwa mara.

Uhasama na Umbwe sekondari: Hizi zilikuwa ni shule mbili za wavulana zilizokuwa zikioneshana ubabe na wakati mwingine kuvamiana na kutwangana. Baadhi ya wanafunzi waliuwawa ktk uvamizi uliokua unafanywa.

Pia wezi kutoka uraiani kuuwawa ilikuwa ni jambo la kawaida sana. Hali hii ilitunyima hata uhuru wa kutembea kijijini.

Maandamano: Kuna siku alifariki mwanafunzi mwenzetu kwa uzembe wa kimatibabu, tuliamshwa saa kumi asubuhi tukaanza maandamano 25 km mpaka Moshi mjini. Tuliziba upande mzima wa barabara na ilibidi wakati wa kurudi tukodishiwe fuso za kuturudisha maana idadi yetu ilikuwa kubwa mno.

Vita kati ya Advance na O-level: Hakika tulikua hatupendani hata kidogo, mara kwa mara yalizuka mapigano kati yetu na tulitumia silaha kama mawe, mafyekeo, majembe nk.

Polisi wa Boma ng'ombe walikua na wakati mgumu kutuliza fujo zilizokua zikitokea usiku wa manane. Wengi tulilala mashambani kuokoa maisha yetu.

Mahudhurio darasani: Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi mahudhurio hayakuwa mazuri. Nakumbuka kidato cha pili tulikuwa 500 na tuliwekwa ktk mikondo mitano (J,K,T,U, na V). Niliwahi kuandikishwa barua na mkuu wa shule kwa kutoonekana darasani miezi mitano kwani hata mwalimu wa darasa alisema hanifahamu na hajawahi kuniona.

Kidato cha 3 na 4 kufukuzwa shule: Kutokana na nidhamu mbovu kulitokea ugomvi mzito baina ya makundi ya wahuni na viongozi ambao ulipelekea hasara kubwa na shule kufungwa kwa muda. Kila mwanafunzi ililipa faini ya sh.9000/= na baada ya hapo kidato cha 3 na 4 tulifukuzwa wote na kupewa ofa ya kuhamia shule yeyote ya kata.

Tulipakana na shule kama: Lyaskika, Somsom, Narum nk ambapo tulikua tunapoozea mioyo kwa mabinti wa shule hizo.

Waweza ongeza lolote kwa uliyepitia mambo hayo:


1480583166738.jpg
 
Mimi nilifundisha hesabu Lyamungo 1975 hadi 1977 (Enzi za Mtui na Livigha). Shule ilikuwa ya kistaarabu sana. Ila nikiri swimming pool ilionekana na kuanza kutelekezwa. Shughuli au elimu ya kilimo ilikuwa inakwenda vizuri kwa hiyo msosi fresh ilikuwepo.

Suala la ubabe na mateso nakubaliana na wewe kwa sababu utaratibu wa nidhamu ulipewa maana tofauti si mashuleni (sector ya elimu) pekee bali serikalini kote.

Samahani lakini ukweli nitausema 1977 kilizaliwa chama cha mapinduzi kipindi hicho hicho jumuiya ya Africa ya Mashariki ilikufa. Kulikuwa na vuguvugu la vita na Uganda. Kisiasa chama kilishika hatamu. Kwa hiyo kulikuwa na mambo na changamoto nyingi sana.

Ikafuatia kufunga mikanda kwa maana ya changamoto za uchumi. Unaweza kujiuliza haya yana uhusiano gani na hoja yako. Kifupi yana uhusiano

1. Yako siyo isolated case ni hali ya taifa zima hususan kielimu kwa kukosekana kusustain ideals za matakwa ya kielimu.

2 Kushindwa kuhimili changamoto za mabadiriko . Kitaalam tunasema failure ya kumanage transition. Hili linatuathiri hadi leo.

3. Ile shule ilikuwa ya KNCU mchepuo wa Kilimo. Lakini ilipinduliwa kusudio la awali na kurundikiwa jukumu lisilofanana na mazingira. Kwa hiyo kulihitajika usimamizi madhubuti ambao haukuwepo na hautakuwepo.

Faida uliyopata moja ni ukomavu unaweza kukabiliana na mazingira yoyote magumu.

Hata hivyo nakupongeza maana umepikwa na tanuru la changamoto. Natumaini huna kinyongo maana umevuka ukiwa ngangari. Ila kwenye maisha kuna changamoto zaidi ya hizo za Lyamungo.

Naipenda Lyamungo ya KNCU
 
dah lybwax bwana..siku nafika hapo nilishangaa sana, yani paredi watu wanaenda kama sokoni, huyu kavaa sweta ndani na shati jeupe chafu juu..

dah vituko aisee..class watu hawaingii..yani wengine tupo class wengine wako social hall wanacheki tv...lkn watu wanafaulu balaa.....tumekula sana ugali na pilipili apo.
 
Dah.. lyamungo palinikomaza sana... nakumbuka mtaani nilikuwa naleta fujo then narudi shule kupandisha kikosi tukiwa na maslesha... siamini nlikuwa narudi home nakaa miezi kwa miezi nikirudi ni kwa mitiani tu... ila walionifata walipotea maana nlikuwa nasoma kama sina akili nzuri na ni moja kati ya watu walioshangaza kwenye matokeo... dah maisha ya lyamungo ni sawa na jeshi tu
 
Daaah..! Umenikumbusha mbali mkuu..! Nakumbuka vita ya mwaka 2009 tarehe 27/28 August, kati ya Umbwe na Lyamungo..!
Daah , kaka hata mimi nilikuwepo . Nikiwa nasoma umbwe form 5 wakati huo. Kwakweli sitasahau. Usiambiwe kabisa. Aiseee? Mungu atusamehe na amrehemu mwenzetu aliyeuawa. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amiin! Wadogo zetu waache kabisa ujinga huu, hauna faida
 
Kijana naona umenitaja eti nilikuwa na karate uchwara, usinijaribu( in ......voice). Nitakuchukua nikakuzamishe kwenye mfereji wa uwanja wa mpira. Dah! Lyamungo!
Acha tu mkuu, nliichukia shule na nisingefukuzwa ningefeli kabisa.

Tulikua tunapigwa kama wezi.
 
Nimesoma maeneo ya jirani na Lyamungo,hakika mtoa mada umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa tunakuja sana kila jumamosi kupata da'awa kutoka kwa maustaadh wa Lyamungo,walikuwa wanatupikia vizuriiiiii wali maharage
Hahahaaaaaa

Yote uliyoyasema ni kweli kabisa.
I miss those days
Hahaha wewe utakuwa wa Lyasikika au Somsom
 
Back
Top Bottom