Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Maputo ukitoka huko lazima uvue nguo kwanza na kukaa nje kidogo lasivyo ukiingia class kila mtu anajua umetoka toilet.

watu kuoga na kupendeza siku ya Soko la Kombo

Sijui kama mliikuta hii Advance waliandika barua umbwe kuomba Vita na Uwanja wa Vita uwe Mlama desert hii ni baada ya Umbwe kuanza kututangazia shule mbalimbali za Wasichana kama Machame,Mawenzi,Weruweru kuwa Sisi hatupendi kuoga ni wachafu ila umbwe walikataa hii vita.

kuvua samaki wa shule fishpond na neti siku za jumamosi walimu hawapo shuleni.

kuna sehemu iliitwa makaburini sijui chanzo cha jina hili ni nn

Siku za graduation Machame shule nzima inahamia machame kisa kuna umoja unaitwa Lyamacha.

Kiongozi wa chakula kuchukua nyama kwenye kindoo na kuenda kuuzia wenzake kinyango shs 200 nani lazima ununue na sio ombi.

Lyamungo ile ilikua ni kama Guantanamo bay au chuo cha kijeshi ukipita pale hata jangwan utaishi.
 
hivi wale machalii waliopandishwa kwenye mando ya Burieta(mkuu wa shule enzi hizo) wapo hapa? walepelekwa pale Lyasikika kisa wasichana wa Lyasikika walienda kuwasemea vijana wa lyamungo wanawatongoza kwa nguvu. iligongwa kengele wale mabinti wa shule jirani wakaambiwa wapite kukagua sura moja baada ya nyingne....
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] umenikumbusha mbali sana mkuu nakumbuka hiyo ilikua 2004 ambapo lyasikika ndo ilikua imeanzishwa. Bureta akidondoka na biti zake unaona hapa haponi mtu.
 
Vipi na wale waliofungwa taulo wacheze taarifa ya habari, hiyo ilikua Shaban Robert hiyo ya kina mustapha kama dom leader hiyo skendo nakumbuka mpk Stanislaus aliewahi kushinda isha ya East Africa alihusika.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Mwaka gani mkuu hii?
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] umenikumbusha mbali sana mkuu nakumbuka hiyo ilikua 2004 ambapo lyasikika ndo ilikua imeanzishwa. Bureta akidondoka na biti zake unaona hapa haponi mtu.
Dah jamaa alikuwa na bit balaa ila nadhani Ile shule iliharibika baada ya yeye kuondoka ndo kukawa na hadi mauaji
 
Maputo ukitoka huko lazima uvue nguo kwanza na kukaa nje kidogo lasivyo ukiingia class kila mtu anajua umetoka toilet.

watu kuoga na kupendeza siku ya Soko la Kombo

Sijui kama mliikuta hii Advance waliandika barua umbwe kuomba Vita na Uwanja wa Vita uwe Mlama desert hii ni baada ya Umbwe kuanza kututangazia shule mbalimbali za Wasichana kama Machame,Mawenzi,Weruweru kuwa Sisi hatupendi kuoga ni wachafu ila umbwe walikataa hii vita.

kuvua samaki wa shule fishpond na neti siku za jumamosi walimu hawapo shuleni.

kuna sehemu iliitwa makaburini sijui chanzo cha jina hili ni nn

Siku za graduation Machame shule nzima inahamia machame kisa kuna umoja unaitwa Lyamacha.

Kiongozi wa chakula kuchukua nyama kwenye kindoo na kuenda kuuzia wenzake kinyango shs 200 nani lazima ununue na sio ombi.

Lyamungo ile ilikua ni kama Guantanamo bay au chuo cha kijeshi ukipita pale hata jangwan utaishi.
Ale Palikuwa na milima milima midogo midogo nadhani ndo chanzo
 
Mimi nilifundisha hesabu Lyamungo 1975 hadi 1977 (Enzi za Mtui na Livigha). Shule ilikuwa yakistaarabu sana. Ila nikiri swimming pool ilionekana na kuanza kutelekezwa. Shughuli au elimu ya kilimo ilikuwa inakwenda vizuri kwa hiyo msosi fresh ilikuwepo.

Suala la ubabe na mateso nakubaliana na wewe kwa sababu utaratibu wa nidhamu ulipewa maana tofauti si mashuleni (sector ya elimu) pekee bali serikalini kote.

Samahani lakini ukweli nitausema 1977 kilizaliwa chama cha mapinduzi kipindi hicho hicho jumuia ya Africa ya Mashariki ilikufa. Kulikuwa na vuguvugu la vita na Uganda. Kisiasa chama kilishika hatamu. Kwa hiyo kulikuwa na mambo na changamoto nyingi sana.

Ikafuatia kufunga mikanda kwa maana ya changamoto za uchumi. Unaweza kujiuliza haya yana uhusiano gani na hoja yako. Kifupi yana uhusiano

1. Yako siyo isolated case ni hali ya taifa zima hususan kielimu kwa kukosekana kusustain ideals za matakwa ya kielimu.

2 Kushindwa kuhimili changamoto za nabadiriko . Kitaalam tunasema failure ya kumanage transition. Hili linatuathiri hadi leo.

3. Ile shule ilikuwa ya KNCU mchepuo wa Kilimo. Lakini ilipinduliwa kusudio la awali na kurundikiwa jukumu lisilofanana na mazingira. Kwa hiyo kulihitajika usimamizi madhubuti ambao haukuwepo na hautakuwepo.

Faida uliyopata moja ni ukomavu unaweza kukabiliana na mazingira yo yote magumu.

Hata hivyo nakupongeza maana umepikwa na tanuru la changamoto. Natumaini huna kinyongo maana umevuka ukiwa ngangari. Ila kwenye maisha kuna changamoto zaidi ya hizo za Lyamungo.

Naipenda Lyamungo ya KNCU

Ongera sana Baba,kwa mwaka huo wewe ni kama Baba kwangu na hii iwe ni fundisho kwa baadhi ya vijana ambao wanatoa lugha chafu
Na kuandika upuuzi jf.Hakika humu kuna vingunge
 
Back
Top Bottom