Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Nayakumbuka Mateso ya Lyamungo Sekondari

Kama umepita shule hizi hapa tanzania,basi we tayari uko kwenye jeshi la akiba,maana maisha ya huko na jeshni hayana tofauti.
lyamungo
umbwe
old moshi
mara sec
musoma tech
iyunga tech
magamba
ndanda
tosamaganga
kilimanjaro boys
same
kibiti
pugu
minaki
mirambo
songea boys
Umesahau Tambaza na Azania? Vurugu zao z ilikuwa kama Wapalestina na Israeli
 
Kama umepita shule hizi hapa tanzania,basi we tayari uko kwenye jeshi la akiba,maana maisha ya huko na jeshni hayana tofauti.
lyamungo
umbwe
old moshi
mara sec
musoma tech
iyunga tech
magamba
ndanda
tosamaganga
kilimanjaro boys
same
kibiti
pugu
minaki
mirambo
songea boys
dah aseeeee same boys high school... I still remember this place it z my home place 4 realy.....2014/2016 advanced level
 
Ubabe wa haina huu ndo umesababisha mwaka huu mwez wa 8 viongoz zaid ya 13 wa lyamungo kufukuzwa,.

Shule pekee inayoendeshwa na viongoz hapa Tz, since day 1
 
Mimi nilifundisha hesabu Lyamungo 1975 hadi 1977 (Enzi za Mtui na Liviga). Shule ilikuwa yakistaarabu sana. Ila nikiri swimming pool ilionekana na kuanza kutelekezwa. Shughuli au elimu ya kilimo ilikuwa inakwenda vizuri kwa hiyo msosi fresh ilikuwepo.

Suala la ubabe na mateso nakubaliana na wewe kwa sababu utaratibi wa nidhamu ulipewa maana tofauti si mashuleni (sector ya elimu) pekee bali serikalini kote.

Samahani lakini ukweli nitausema 1977 kilizaliwa chama cha mapinduzi kipindi hicho hicho jumuia ya Africa ya Mashariki ilikufa. Kulikuwa na vuguvugu la vita na Uganda. Kisiasa chama kilishika hatamu. Kwa hiyo kulikuwa na mambo na changamoto nyingi sana.

Ikafuatia kufunga mikanda kwa maana ya changamoto za uchumi. Unaweza kujiuliza haya yana uhusiano gani na hoja yako. Kifupi yana uhusiano

1. Yako siyo isolated case ni hali ya taifa zima hususan kielimu kwa kukosekana kusustaon ideals za matakwa ya kielimu.

2 Kushindwa kuhimili changamoto za nabadiriko . Kitaalam tunasema failure ya kumanage transition. Hili linatuathiri hadi leo.

3. Ile shule ilikuwa ya KNCU mchepuo wa Kilimo. Lakini ilipinduliwa kusudio la awali na kurundikiwa jukumu lisilofanana na mazingira. Kwa hiyo kulihitajika usimamizi madhubuti ambao haukuwepo na haukuwepo.

Faida uliyopata moja ni ukomavu unaweza kukabiliana na mazingira yo yote magumu.

Hata hivyo nakupongeza maana umepikwa na tanuru la changamoto. Natumaini huna kinyongo maana umevuka ukiwa ngangari. Ila kwenye maisha kuna changamoto zaidi ya hizo za Lyamungo.

Naipenda Lyamungo ya KNCU
Mkuu, ulifundisha Lyamungo ukiwa na miaka mitano? Profile yako inasema ulizaliwa mwaka 1970.

Yote kwa yote heshima kwako na kuanzia sasa nitaanza kukufuatilia ili nijifunze busara zako. You are an inspiration!
6acc5ebcebe3b55d07695d3474d1ceed.jpg
 
Asante ila kazi ya mungu makosa
Ongezea na Sengerema High. Wanafunzi wa Kikurya huko waliwahi kuua askari kwa kumdondoshea jiwe kichwani wakiwa juu ghorofani. Pia waweke na wazee wa Ihungo kule Bukoba. Na wanaume wa Shybush karibu na almasi za Mwadui pale.
 
Mkuu, ulifundisha Lyamungo ukiwa na miaka mitano? Profile yako inasema ulizaliwa mwaka 1970.

Yote kwa yote heshima kwako na kuanzia sasa nitaanza kukufuatilia ili nijifunze busara zako. You are an inspiration!
6acc5ebcebe3b55d07695d3474d1ceed.jpg
Hiyo profile ni ya kukwepa sheria ya habari baada ya life ban.

Wakati huo naanza kufundisha ni baada ya kuhitimu Chuo Kikuu DSM nikiwa na miaka 26.

Be serious persue education it is an investment worth 100 years
 
Iyunga bhana kwa sasa ni kama seminary tu nafikiri ubabe umepungua

Ila enzi zetu ilikuwa ni shida aisee hahahah hasa kwa fomwaniii(ndivyo wanavyoitwa)

Mambo mengine yanashabiana na huyo maelezo ya jamaa hapo juu

Lakini kwa sasa nafikiri displine imetake place kwa hiyo usiwe na hofu na kijana wako kikubwa mpatie msaada wa kisaikolojia ataweza kuishi vizuri tu

Halafu mpatie mahitaji muhimu akitulia kwa ile shule atafaulu safi kabisa

Enzi zetu kupata div one ilikuwa jambo la kawaida unakuta mtu mtata sana lakini mbele ya pepa harembeshi


Mtafute mama mmoja ukimpeleka pale anaitwa madam kimani unaweza kumuomba awe watchdog wa mwanao

All in all maisha ya bweni shule za serikali ni kama jeshi tu hahahah

Levavi oculos

Dah umenikumbusha iyunga enzi za guantanamo nikiwa njuka, ebana ziliibiwag ela za jamaa flan iv chemban kwake kabla ya mpigo alaf sisi ndo huwa tulikuwa tunachezeaga draft mara nyingi kwenye iyo chemba.Iyo siku ya kufunga shule mi nikawai kusepa mapema tu saa 9.

Sasa kumbe wakati nimeondoka kumbe jamaa pale chemba tunapochezeag draft ndo akaibiwa ka elf 50 za nauli, Basi kengele ikagongwa alaf wahusika tukatajwa na mpaka apo mi sijui kitu yoyote. Wale jamaa wakabanwa wamtaje muhusika ila mwisho wa siku wakaachiwa warud home mpaka tulivofungua shule.

Ile kufungua shule mpaka apo mi sina ili wala lile, ila niliporud jamaa ndo wakanambia kwamba mi ni mmoja ya walioiba izo ela ndo maana niliwah kuondoka siku ya kufunga shule. Si ndo siku ya siku tukaitwa Gwantanamo chamber nikajua naenda kuisha na apo ni njuka na jinsi nilivokuwa naona wezi wakiwatreat ilikuwa ni balaa.

Ila uzur wake nilijitetea kwamba niliwah kuondoka kabla ya kuibwa na bahati nzuri jamaa yangu mmoja akanitetea ndo nkaponea apo ila walobaki na yeye mwenyewe walichezea vibaya mno. Nilichokifanya ni kuzunguka tu nyuma ya mesi tunapooshea makontena kuwaskilizia tu jamaa wanavolia uku nikimshukuru mungu kuponyeka
 
Kama umepita shule hizi hapa tanzania,basi we tayari uko kwenye jeshi la akiba,maana maisha ya huko na jeshni hayana tofauti.
lyamungo
umbwe
old moshi
mara sec
musoma tech
iyunga tech
magamba
ndanda
tosamaganga
kilimanjaro boys
same
kibiti
pugu
minaki
mirambo
songea boys
ungetuongeza na sisi wa kahororo
 
Daaaah nilikua mmoja kati ya waliofukuzwa,kati ya vita ya jamaa alieng'olewaga meno na simba wa nyika!nilifukuzwa kabisa na wandiba
 
dah aseeeee same boys high school... I still remember this place it z my home place 4 realy.....2014/2016 advanced level
Same beibi.....watu wametafuna sana wake za watu pale Masandare....Kundael (1996-1999)
 
aisee tumpiga sana scrumble,unakumbuka maputo,fongo,mbuzi na mabunda????
 
Daaah..! Umenikumbusha mbali mkuu..! Nakumbuka vita ya mwaka 2009 tarehe 27/28 August, kati ya Umbwe na Lyamungo..!
nakumbuka kutobelewa kwa mipira miwili 2003 kati ya lyamungo na vijana wa mti safi (umbwe).
 
Nimesoma maeneo ya jirani na Lyamungo,hakika mtoa mada umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa tunakuja sana kila jumamosi kupata da'awa kutoka kwa maustaadh wa Lyamungo,walikuwa wanatupikia vizuriiiiii wali maharage
Hahahaaaaaa

Yote uliyoyasema ni kweli kabisa.
I miss those days
mkuu ulisoma somsom?, lyasikika? au mlama?
 
Inaonekana umechezea sana kwanja mkuu na kuogeshwa, pole sana
 
Hahaaa! Hii thread imenikumbusha mbali ule ugomvi wa 2009 na Umbwe chanzo kilikuwa kufungwa kwenye mechi iliyochezewa uwanja wa Elyasikika.

Jamaa wa Elyamungo wakaona noma kufungwa mbele za mademu wao tena nyumbani wakaanzisha vurugu ambazo tuliwamudu ila tulikimbilia shuleni kujipanga.
Asubuhi yake tuliichakaza Elyamungo na ndipo hapo yule jamaa wa form 5 alipoteza maisha maana alikuwa mgeni na katika kukimbia akakosea direction kuingia ngome ya adui ndani zaidi.
Dah! Natamani kulia, so sad.
 
Back
Top Bottom