Nawezaje pata mkopo kuanzia mln5 hadi 10 bila dhamana kwa kutegemea mshahara usio na permanent contract

nyotanjema

Senior Member
Sep 24, 2011
136
170
Habari zenu!
Naombeni msaada wa namna ya kupata mkopo wa haraka sana wa kiasi cha mln 5 hadi 10

Mimi nafanya kazi katika mashirika binafsi kwa miaka 6 sasa. Na shirika hili tunapewa mikataba ya mwaka mmoja mmoja, hivyo nimejaribu kwenda kwenye taasisi mbalimbali za mikopo naambiwa nipeleke dhamana, permanent contract, na vyote havipo.

Na nina uwezo wa kulipa 1, 000,000/= endapo nitapata mkopo na ningeweza kukusanya lakini majanga ni mazito sana
Mimi ni mtu mzima mwenye familia na nategemwewa na wazazi.
 

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
971
1,000
Siyo rahisi kihivyo. Watu wanaofanya kazi private mna tabu sana, poleni.
Taasisi za fedha wanaangalia security ya hela zao kwanza, ndio maana wanakomaa na salary ndo wana uhakika nayo.
Hayo mengine labda upeleke hati ya kiwanja waje wathaminishe ndo wakiona inatosha watakupa wakijua ikibuma wanapiga mnada kiwanja au nyumba.

Angalizo: Siku ukifanikiwa ukawa na majumba, magari, biashara kubwa kubwa, wala hutahitajika kwenda benki kuomba mkopo. Watakutafuta wenyewe wakubembeleze ukope maana tayari unakopesheka
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,246
2,000
Kama Unakopa ukatatue Majanga ya Kifamilia

Nakushauri "acha" NDUGU yangu.

Vinginevyo,
Unakopa kwenda Kuizalisha kwenye Biashara.

By the way,
Ingekua vema kabisa, Ungeelezea lengo halisi LA mkopo.

Huenda ungeweza saidiwa kifedha na Usiingie Madeni tena .

Au hata Ushauri pia ukaweza litatua tatizo lako kwa style tofauti.

TULIZA AKILI MKUUSent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom