Nawezaje kubadili combination ya HGL kwenda CBG huku nikiwa na F ya hesabu?

Unaitafuta zero form six inawezekana bahati mbaya ila ukumbuke kuna bam yaani hesabu utazikuta na kemia ina vi element vya hesabu kidogo...
Unabadilishia shule ila sidhani km watakubali kwenye shule za serikali mtu mwenye f ya hesabu kusoma sayansi
Ntapata zero form six, kwasababu gani kaka naomba unijuze,na naomba unisaidie ni Nini maana ya BAED maana Kuna mtu kaniambia aliachana na science na kwenda kusomea hiyo baed art
 
Ntapata zero form six, kwasababu gani kaka naomba unijuze,na naomba unisaidie ni Nini maana ya BAED maana Kuna mtu kaniambia aliachana na science na kwenda kusomea hiyo baed art
Itakugharimu muda na nguvu kusoma kwa kuwa masomo ya sayansi hesabu ni lazima kwa tanzania..wakati unakomaa utapoteza muelekeo..maana kule kuna organic inorganica general na pysical chemistry zaitaji umakini...biology ndo usiseme kuna kitabu kinaitwa bs ndo kitakuwa km msaafu wako..sasa kwa kuwa kuna mambo mengi mapya na notice ni nyingi na hesabu mwalimu ataashumu kuwa o levo umepitia na una d na kuendelea atatwanga intagresheni na diferesheni km kawa kumbe ww hesabu ni mzigo. Ndo inakuja mtaka yote hukosa yote.
Iyo nyingine uliouliza ni shahada ya sanaa ya elimu. Km sijakosea...
Pia unajiwekea mazingira magumu km watafaulu sayansi wengi vyuo vikuu wanachagua walofaulu vema sasa km watakutafutia point kwenye masomo mawili yaaani c na b au b na g...wakasema added advantage ni yule alofaulu hesabu yaani bam ambayo pia si subsidiary subject. Na form six ukafeli hesabu itakubidi km unapenda sayansi uende kozi yyte utakayopata au km ukakomaa na unayotaka itakubidi uende diploma kwanza.ili upate sifa za kwenda shahada ya kwanza
 
Nakumbuka ile misemo yetu HGL"High Government Leaders".Comb yangu hiyo mimi mwenyewe nilibadili,maana nilipangwa HKL miaka hiyo.
 
JAMANI naomba kujua nitawezaje kubadili combination ya HGL ambayo nimepangiwa,ingawaje na combination ya CBG,imebalanca lakini mathematics nimepata alama "f"

Naombeni mnisaidie wakuu
Inawezekana kabisa . Ilimradi uwe umefaulu zaidi ya c katika masomo ya cbg
 
Fika shuleni, halafu jaribu kuomba kubadili combination yako.
Ingawa kuna ugumu na sababu imeshaelezwa,ni vigumu kusoma combination ya sayansi A'level iwapo umefeli hisabati O'level.
CBG ni lazima utasoma na Basic Applied Mathematics (BAM).
 
K
Nakumbuka ile misemo yetu HGL"High Government Leaders".Comb yangu hiyo mimi mwenyewe nilibadili,maana nilipangwa HKL miaka hiyo.
Kaka kwa miaka hii nikisomea comb ya HGL Kuna uwezekano wa kupata kazi, kuajiriwa mapema kweli?,na Kama unaijua kozi nzuri ya kusomea hgl naomba unisaidie nijue, kakaangu,kwa maana katika masomo yangu yote ni hesabu tu ndio iliyokuwa inaniyumbisha pekeyake,Ila hayo mengine nilikua nafanya vizuri Sana, naomba unisaidie kwa hapa kaka
 
Nisikilize mimi kwa umakini...hapo ulipo huiwezi mathe na kwenye Chemistry advance kuna hesabu napia kuna BAM, na hatakama ikitokea umepata chance ya kusoma CBG na ukafaulu form 6...huwezi kwenda kusoma Course za afya chuo kwa sababu TCU guidebook yao kwa course za afya inataka o level Mathe uwe na atleast D, hivo utarudi tu kusoma course nyingine za arts...kuliko kupoteza muda ni heri ukomae na hiyo hiyo waliokupangia... Usiforce mambo ndugu yangu.. Utakuja kujutia baadae...ohoo
 
Hesabu imekuharibia mdogo wangu huwezi kusoma CBG katika government schools kama huna atlest D ya hesabu!
The only alternative you can do is kuhamia private schools huko watakupokea kwa huo ufaulu wako!
CBG anasoma government school ata Kama ana "F" ya maths bwana sema itampa shida University wakati wa kuchagua kozi maana Kuna kozi nyingine at least uwe na pass ya maths o'leval hasa chuo cha Ardhi hawezi kusoma kozi yyte, Ila kwenye Afya chemistry na Bios itambeba, kikubwa asilazimishe kusoma CBG maana Kuna BAM na Chemistry nazo zahitaji kidogo solving Kama hayuko vizuri ata mbwela
 
Kaka na
nap unijulishe BAED ndio Nini kaka maana bado sijafahamu naomba unisaidie kaka
Dogo utapasuka kichwa hayo Mambo ya BAED Siyo level yako fuatilia ushauri unaotaka, ukimaliza form6 ingia TCU uanze kuona hizo BAED za DUCE, MUCE na kwingineko
 
Kaka kwa miaka hii nikisomea comb ya HGL,Kuna uwezekano was kupata kazi,kuajiriwa mapema kweli?naomba unijuze kaka
Dogo unawaza ajira mbona mm nimehitimu Bachelor Toka 2018 nipo sijapata kazi life linaenda kwakujiongeza, ukisoma ili uajiriwe Wafwaaa sasahivi kila kukicha mkuu anaajiri wajeda na mapolice tu, Kama unataka kuajiriwa government nenda JKT ukajenge jiko la Ikulu ajira fasta
 
Masikini nimeona huruma huyu dogo anauliza sana maswali pengine sababu hana mtu wa kumuuliza mitaani, huwezi jua yuko wapi katika mazingira gani ndio maana ameona JF kama only option yakupata information.

Binafsi sikumbuki sababu yakutoka huko siku nyingi, kipindi chetu ilikuwa ukipangiwa combi ya arts kama huna C ya hesabu basi usijihangaishe kubadili sababu hauruhusiwi, ilikuwa ni kama vile ukifeli maths O-level automatically umedisqualify kusoma combi yoyote ya science ndio maana wanakupangia arts.

In other way option ilikuwa kwenda shule ya private, ukasome combi unayoihitaji kama ulifeli maths unajisajili kurudia maths kama private candidate hadi pale utapochomoa maths ndio utaruhusiwa kufanya mtihani wa form 6 kwa Combi hiyo ya science uliyojichagulia huko private. (Opsss nimeeleza kwa kujaribu kurecall mambo ya miaka hiyo na sidhani kama nimeeleza sahihi)

Chakufanya mdogo wangu hebu jaribu kumtafuta mwalimu wako hasa academic teacher umuulize kuhusu hilo, nadhani anaweza kukupa muongozo mzuri, maana inaonekana JF hakuna walimu.
 
uwezekano upo mkuu, kuna dogo hapa mm ndo nmemfanyia application miez miwil ilopita,jana nmeona matokeo kachguliwa cbg, moshi tech, na ana F ya mathe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ohh basi vizuri mkuu, msaidieni kumwelekeza mdogo wenu huyu.
ndo hivyo namwambia hapa akifika, akakomae mana hiyo comb ni science na hesabu kwake ni changamoto, akatie msuli wa maana, na ajitahid mana kuna BAM kule, hesabu haikimbiliki, akifika chuo ndo kabisaaa hesabu ni lazma ktk kozi za cbg..
ila naamini mungu atamsimamia, kila la heri ndugu.ila asiende na cm shule mana naona jf imemkolea sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom