Nawezaje kuanza maisha upya

Nawezaje kuanza maisha upya

Pole sana mkuu na hongera pia
Kwanza ungeeleza upo mkoa gani na una nini kianzio, marafiki na connection ni kazi sana kupata kwa mtu Kama wewe uliyesema ni mkimya pro max
Ila haimaanishi huwezi kupata no unapata Tena unaweza pata marafiki wazuri kabisa


Kuhusu kukaa kwa watu bhana inategemea Ila jitahidi kwa namna yoyote Ile wasikuone wewe mzigo hapo jitahidi ku add value hapo home Kama kazi na huyo shamba boy fanya nae na siku zingine toka kazunguke huko upate mchongo kama Kuna vibarua fanya yaani usione aibu kwa hako ka degree Kako kamoja ambako Jane Sina Ukashindwa kufanya kazi zingine.


Kila la kheri
 
Sema kama sio muongeaji, ni ngumu sana ku force stories, ni ngumu sana Naandika kwa uzoefu...

Sijui uanzie wapi, ila kwa ufupi hapo ni ugenini, Jitahidi sana, najua ni ngumu..
Ukimya sana utawapa mashaka, kumbuka wao hawakujui..
Na ajitahidi asile binti wa hapo home hata kama ni beki tatu
 
Pole sana mkuu na hongera pia
Kwanza ungeeleza upo mkoa gani na una nini kianzio, marafiki na connection ni kazi sana kupata kwa mtu Kama wewe uliyesema ni mkimya pro max
Ila haimaanishi huwezi kupata no unapata Tena unaweza pata marafiki wazuri kabisa


Kuhusu kukaa kwa watu bhana inategemea Ila jitahidi kwa namna yoyote Ile wasikione wewe mzigo hapo jitahidi ku add value hapo home Kama kazi na huyo shamba boy fanya nae na siku zingine toka kazunguke huko upate mchongo kama Kuna vibarua fanya yaani usione aibu kwa hako la degree Kako kamoja ambako Jane Sina Ukashindwa kufanya kazi zingine.


Kila la kheri
Asante Kwa ushauri. Toka nifanye maamzi haya mawazo ya degree nimeshafungia kabatini na hata sipendi kuwaaambia watu. Niponipo tu, nimepigka vizuri tu na maisha jeuri yote imeniisha
 
Yaliyonikuta kwenye maisha yameumiza moyo na nafsi yangu. Leo sitosimulia mkasa wa maisha yangu.

Maamzi niliyofanya nime relocate mkoa kuanza maisha mapya. Mkoa huu Sina ndugu ila that day nashuka stend nlimfuata Mzee mmoja tuliekua tumepanda bus moja. Nikamweleza Mzee naomba uniamini, ni mara ya kwanza ndo nafika kwenye mji huu, simjui mtu, na Sina pa kufikia. Nakamuomba anihifadhi, Mzee aliniangalia Kwa Dk kazaa akiwa ananisikuliza nikijieleza na huku amenikazia macho na kuusoma uso wangu and all my body language, akanijibu nifuate.

Aliita tax akamuelekeza driver eneo analoishi na safari ikaanza. Baada ya kama dk 15 tukaingia mtaa flani, una miti mingi, eneo tulivu halina harakati nyingi . Tax ikasimama kwenye nyumba, tukashuka na kuingia kwenye makazi hayo .
Kumbe Mzee ni police mstaafu, anaishi anaishi na familia yake ndogo. Home alikuwepo mkewe, na dada ake , wote watu wazima, na wajukuu wawili. Vijana wao wana maisha yao mikoa mingine. Kulikua na nyumba kubwa na ingine ndogo. Ile ndogo alikua anishi shamba boy. Baada ya utambulisho-mfupi Mzee akasema tutakua na mgeni huyu Kwa siku kadhaa, badae akanitambulisha Kwa shamba boy na kusema mtakua mnalala huku.

Kufupisha mkasa huu, Mzee na familia yake wamekua wakalimu. Nilipata fursa ya kumuuleza Mzee my profile and background. Kiufupi ni msomi wa level ya degree ila ndo hizi course ambazo mtu una graduate afu ukifika kitaa wewe mwenyewe ukijiuliza ulisomea nini unapata shida kupata jibu clear. Tuachane na Hilo.

Ki personality sababu ya kupigwa na maisha na changamoto za maisha nimekua introvert pro. Mkimyaa sana, usipoanzisha story hainisumbui kubaki kimyaa. Kiukweli sio kuwa ni ujeuri , ila nikiwa kimyaa najiona Niko safe zaidi ya kufungua kinywa changu .

Kwa utangulizi huu naomba Nije kwenye hoja ya msingi. Nifanyaje ili niweze kuanza maisha mapya kwenye mji mgeni kwangu, bila network ya marafiki, ndugu na jamaa. Kwa wale waliowahi pitia scenario kama hii mliwezaje kupata marafiki wapya, mambo gani ya kuzingatia unapokua ugenini Kwa watu baki waliokuamini. Njia gani za kutumia kuongeza network?

Kuna stress naipitia hadi akili haifikiri vizuri. JF naombeni muongozo
Well fanya hivi kwa kuanzia tu mengine mbele ya safali
1. Kuwa muamifu

2.nidhamu ya hali ya juu

3. Fanya kazi kwa bidii hapo sio unakaa kaa kama bwege.

4.njia yako inaenda kuwa njema sasa

5.naamini network utaipata nzuri MUNGU yu mwema hapo ukikaa vizuri mambo yananyooka utulivu subra na akili mtu wangu.
 
Well fanya hivi kwa kuanzia tu mengine mbele ya safali
1. Kuwa muamifu

2.nidhamu ya hali ya juu

3. Fanya kazi kwa bidii hapo sio unakaa kaa kama bwege.

4.njia yako inaenda kuwa njema sasa

5.naamini network utaipata nzuri MUNGU yu mwema hapo ukikaa vizuri mambo yananyooka utulivu subra na akili mtu wangu.
Asante mkuu
 
Huo Ukimya wako ni kama Mimi tu aisee... Unanitesa sana huwa inafika stage najiuliza huu ukmya wangu utaisha lini nimepoteza na kukosa vitu vingi sana.
Mungu anasaidie.
Tunapata shida sana hasa tukiwa mbele za watu wanaopenda kuongea
 
Mkuu Dodoma ulikuwa unafanya kazi gani ,umesoma umefanya Kazi Dodoma miaka 3 ,unafamilia na mtoto ....

Je wanajua kama saizii upo Kwa MTU umejiweka ?

Hio Kazi uliyokuwa unafanya dodoma ukaacha Si ufate pesa nssf uanzishe mtaji ...Tena serikalin kabisa umeachaje Kazi serikali saizii uko na shamba boy [emoji23]

Au umepewa Kazi ya kumchunguza Huyo Mzee Askari na familia yake [emoji23]
 
Mkuu Dodoma ulikuwa unafanya kazi gani ,umesoma umefanya Kazi Dodoma miaka 3 ,unafamilia na mtoto ....

Je wanajua kama saizii upo Kwa MTU umejiweka ?

Hio Kazi uliyokuwa unafanya dodoma ukaacha Si ufate pesa nssf uanzishe mtaji ...Tena serikalin kabisa umeachaje Kazi serikali saizii uko na shamba boy [emoji23]

Au umepewa Kazi ya kumchunguza Huyo Mzee Askari na familia yake [emoji23]
Ya dunia mengi mkuu
 
Yes, nasaidiana sana na mshikaji huyu na ananipa ushirikiano. Mungu ambariki. Angenikazia ningekua sipati hata usingizi
Akukazie yeye kwakeee? Akikuzingua niambie namtimua yeye unakaa wewe. Kuwa makini sana na mabinti zangu kijana
 
Back
Top Bottom