Nawezaje kuanza maisha upya

Nawezaje kuanza maisha upya

Yaliyonikuta kwenye maisha yameumiza moyo na nafsi yangu. Leo sitosimulia mkasa wa maisha yangu.

Maamzi niliyofanya nime relocate mkoa kuanza maisha mapya. Mkoa huu Sina ndugu ila that day nashuka stend nlimfuata Mzee mmoja tuliekua tumepanda bus moja. Nikamweleza Mzee naomba uniamini, ni mara ya kwanza ndo nafika kwenye mji huu, simjui mtu, na Sina pa kufikia. Nakamuomba anihifadhi, Mzee aliniangalia Kwa Dk kazaa akiwa ananisikuliza nikijieleza na huku amenikazia macho na kuusoma uso wangu and all my body language, akanijibu nifuate.

Aliita tax akamuelekeza driver eneo analoishi na safari ikaanza. Baada ya kama dk 15 tukaingia mtaa flani, una miti mingi, eneo tulivu halina harakati nyingi . Tax ikasimama kwenye nyumba, tukashuka na kuingia kwenye makazi hayo .
Kumbe Mzee ni police mstaafu, anaishi anaishi na familia yake ndogo. Home alikuwepo mkewe, na dada ake , wote watu wazima, na wajukuu wawili. Vijana wao wana maisha yao mikoa mingine. Kulikua na nyumba kubwa na ingine ndogo. Ile ndogo alikua anishi shamba boy. Baada ya utambulisho-mfupi Mzee akasema tutakua na mgeni huyu Kwa siku kadhaa, badae akanitambulisha Kwa shamba boy na kusema mtakua mnalala huku.

Kufupisha mkasa huu, Mzee na familia yake wamekua wakalimu. Nilipata fursa ya kumuuleza Mzee my profile and background. Kiufupi ni msomi wa level ya degree ila ndo hizi course ambazo mtu una graduate afu ukifika kitaa wewe mwenyewe ukijiuliza ulisomea nini unapata shida kupata jibu clear. Tuachane na Hilo.

Ki personality sababu ya kupigwa na maisha na changamoto za maisha nimekua introvert pro. Mkimyaa sana, usipoanzisha story hainisumbui kubaki kimyaa. Kiukweli sio kuwa ni ujeuri , ila nikiwa kimyaa najiona Niko safe zaidi ya kufungua kinywa changu .

Kwa utangulizi huu naomba Nije kwenye hoja ya msingi. Nifanyaje ili niweze kuanza maisha mapya kwenye mji mgeni kwangu, bila network ya marafiki, ndugu na jamaa. Kwa wale waliowahi pitia scenario kama hii mliwezaje kupata marafiki wapya, mambo gani ya kuzingatia unapokua ugenini Kwa watu baki waliokuamini. Njia gani za kutumia kuongeza network?

Kuna stress naipitia hadi akili haifikiri vizuri. JF naombeni muongozo
Pole mkuu maisha haya wengine tunaishi hata Mungu akiangalia tu Anatusamehe maovu yetu.
 
Asante mkuu. Mzee pia anafanya business za mazao , na hapo home Kuna store, magari yanashusha mazao mara nyingi, nimekua najiongeza sana kubeba na kupangilia magunia. Jioni unala mgongo hoi
Nimekumbuka jinsi nilivyolala chini ,godoro nimelijua baada ya kwenda Advance,sonona imetafuna mpk ikaamua kuondoka yenyewe! Piga kazi bro ,acha ubishoo ,kuwa msikivu, piga x starehe. Utatoboa tu!
 
Nimekumbuka jinsi nilivyolala chini ,godoro nimelijua baada ya kwenda Advance,sonona imetafuna mpk ikaamua kuondoka yenyewe! Piga kazi bro ,acha ubishoo ,kuwa msikivu, piga x starehe. Utatoboa tu!
Asante mkuu Kwa kunitia moyo
 
Yes, Niko mtulivu , tatizo ukimyaa wangu pia najiona mgeni Kila siku
unajua kwanini upo hapo ulipo sasa? Jibu ni kwa sababu ulivunja ukimya ukaamua kuzungumza na huyo mzee aliekusaidia baada ya kukusikiliza.
Kuna la kujifunza kwenye hili tena kubwa na la muhimu mno.

Kuna muda unakosa fursa na kusaidika kwa sababu ya ukimya, kujifungia ndani. Na hii ni mbaya sana kwa kijana.
 
Uza simu Anza buashara ndogo ndogo kjana.hiyo smart yako ni mtaji tosha
Asante Kwa mtazamo wako ila kwangu simu ndo tool nimehifadhi taarifa nyingi. Hata hivyo sio muda wote naitumia. Kwa week naweza itumia Kwa masaa kadhaa tu. Nimebadiri namba ya simu sitaki watu wanitafute
 
unajua kwanini upo hapo ulipo sasa? Jibu ni kwa sababu ulivunja ukimya ukaamua kuzungumza na huyo mzee aliekusaidia baada ya kukusikiliza.
Kuna la kujifunza kwenye hili tena kubwa na la muhimu mno.

Kuna muda unakosa fursa na kusaidika kwa sababu ya ukimya, kujifungia ndani. Na hii ni mbaya sana kwa kijana.
Ni kweli, nimeelewa mtazamo wako chanya.
 
Back
Top Bottom