na pia hostel hapo udsm kuna watu wanauzaga vyumba unaweza ukanunua kwa mtu na kukaa mwaka mzima..
mm nilikaaga hapo mabibo hostel mwaka wa kwanza na wapili
mwaka wa kwanza nilimbeba mtu akanipa nusu ya gharama za hostel..
mwaka wa pili nilinunua kitanda kwa jamaa mmoja alikuwa kashalipia first semester, so mm nililipia second semester nika kaa peke yangu mwaka mzima, sikubeba mtu.
kununua chumba ni kinyume na sheria , ila nilimfuata wadeni nikamwambia nina rafiki yangu kapata chumba lakini kasema hatokaa atakua akitokea nyumbani so alikuwa anaomba anikabidhi kile kitanda mm apa niwe nakitumia..
wadeni alikubali akachukua copy ya id yangu akaniambia nitakuwa responsible kwa kile kitanda na semester ya pili inabidi nihakikishe kinalipiwa.
Au nenda kwa wadeni moja kwa moja, mwambie umekosa hostel, unataka kitanda, atakusaidia wengi walikuwa wakisaidiwa..
huko gongo la mboto ni mbali sanaa..