Daladala za Gongo la Mboto zabadili vibali vya njia kukwepa ukarabati BRT

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
222
435
Wanasema dhahabu hupitia moto ili kutengeneza Vito, hayo yanajidhihirisha kwa wakazi wa gongo la mboto ambapo kwa sasa wanapitia adha kubwa ya usafiri wakati ukarabati wa barabara ya mwendokasi ukiendelea.

Kipande cha barabara ya Pugu almaarufu kama Nyerere road kuanzia maeneo ya gold star mpaka kufikia Gongo la Mboto, kipo kwenye upanuzi ili kuwezesha magari yaendayo haraka.

Haya ni maendeleo ila kwa sasa hali ya usafiri imekuwa mbaya sana kwani daladala nyingi zimebadilisha vibali vya njia ili kukwepa kukaa kwenye foleni muda mrefu.

Akizungumza na snitch huyu moja wa dereva wa daladala anayefanya safari zake gongo la Mboto - Masaki alidai kwamba kipindi cha awali kabla ukarabati haujaanza alikuwa ana uwezo wa kupiga hadi trip 5/10 yani round trip tano ila kwa sasa anaenda 2/4 ambapo muda mwingi anamalizia kwenye foleni, na gari linaharibika sana kutokana na barabara ambayo inatumika kwa sasa kutokuwa ya lami. Hivyo kwa sasa wengi wamebadilisha vibali na kuenda maeneo mbali mbali tofauti nchi huku wengine wakilazimika "kuwanga" wakiwa wana maana ya kuiba route nyakati za usiku.

Dereva huyo aliendelea kumwambia snitch huyu kuwa hali hii inasababisha hasara kwani mafuta mengi yanapotea kwenye foleni na pia anachoka sana kiuno kupelekea kushindwa kufanya majukumu ya nyumbani (elewa neno majukumu ya nyumbani).

Kwa upande wa abiria snitch hiyu alifanikiwa kuongea na abiria mmoja aliyejitambulisha kama Maugado ambaye alisema kuwa wamekuwa wakitumia treni ya Mwakyembe ili kuweza kufika mjini au wakati mwingine wanatumia magari ya watu binafsi bajaji na boda boda ambapo inawagharimu mpaka kiasi cha shilingi elfu tano ili kuweza kufika mjini.

Snitch huyu alienda mbali zaidi kumuuliza mmoja wa wakandarasi ukarabati unategemewa kuisha lini ila mawasiliano hayakuwa na mafanikio kutokana na lugha gongana.
 
Back
Top Bottom