Naweza kukaa Gongo la Mboto nikasoma UDSM?

Wewe ni me/ke? Kama ni ke kuna mwenzako njoo kaa nae hapa nae anapiga ud 1st yr
 
kijana autaweza asee,sababu mimi nishajaribu kitunda to udsm wiki sikumaliza,utachoka,usafiri changamoto na utamiss badhi ya vipind,ili bidi nipange tyu hk msewe
Nakushauri kaa hostel au panga room
 
mkuu mtoa mada kwanini unataka kukaa gongolamboto ni matumizi gani unabana, umekosa mkopo? umekosa hostel? labda kuanzia hapo tunaweza kukusaidia..
 
tafuta mwenzako ambae nae anataka kupanga lakin awe mwaminifu , tafuteni chumba mta share cost.

ndivyo wanavyofanya wadau wengi hapo udsm,
hapo msewe kuna vyumba vya bei nafuu tuu
 
Hostel zimejaa

na pia hostel hapo udsm kuna watu wanauzaga vyumba unaweza ukanunua kwa mtu na kukaa mwaka mzima..

mm nilikaaga hapo mabibo hostel mwaka wa kwanza na wapili

mwaka wa kwanza nilimbeba mtu akanipa nusu ya gharama za hostel..

mwaka wa pili nilinunua kitanda kwa jamaa mmoja alikuwa kashalipia first semester, so mm nililipia second semester nika kaa peke yangu mwaka mzima, sikubeba mtu.

kununua chumba ni kinyume na sheria , ila nilimfuata wadeni nikamwambia nina rafiki yangu kapata chumba lakini kasema hatokaa atakua akitokea nyumbani so alikuwa anaomba anikabidhi kile kitanda mm apa niwe nakitumia..

wadeni alikubali akachukua copy ya id yangu akaniambia nitakuwa responsible kwa kile kitanda na semester ya pili inabidi nihakikishe kinalipiwa.

Au nenda kwa wadeni moja kwa moja, mwambie umekosa hostel, unataka kitanda, atakusaidia wengi walikuwa wakisaidiwa..

huko gongo la mboto ni mbali sanaa..
 
Unapanda gari za gomz makumbusho unashukia mjengoni au hostel za magu unaingia chuo but kuchelewa lazma uzoee
 
Na hostel udsm huwa wanapangiwa kwanza ndio badae wanalipa, sasa sijajua wewe ni mwaka wa ngapi , ninachofaham asilimia kubwa wanapataga hostel
 
Maana ni kutoka ulongoni b
Kutoka ulongoni b hadi gomz mwisho unapanda bajaj sh 500 then uchukue daldala hadi mabibo hostel sh 500, halafu upande daladala za chuo kwenda main campus sijui nowdays sh ngapi. Hapo piga hesabu go and return kwa mwezi plus muda unaotumia kutoka ulongoni hadi udsm. Mimi nakushauri bora ukakae kibaha angalau unaweza kuwahi ila sio gomz.
Note: Vipi siku hizi raia wa gomz wamestaarabika hawagombanii magari asubuhi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom