Naweza kukaa Gongo la Mboto nikasoma UDSM?

Unaweza mie niliishi kimara na nikasoma duce... Zipo gari za sm2000 to gongolamboto tena nyingi ni weee kuamka tu
 
Ili uweze kufaulu katika masomo yako comfortability ni suala la msingi, Gongo la mboto mpaka UDSM ni mbali, itakulazimu uwahi kuamka na utarudi late, sometimes hata saa tano usiku, hii ratiba itakufanya urudi umechoka, na inaweza ikawa tiketi ya kutokumaliza shule, kuliko kujipa kibarua cha kuamka mapema na kurudi late nyumbani, ni bora utafute malazi karibu na Chuo, ili uweze kusoma comfortable, nimeyaandika haya with my own experience on that!🙏🏼
 
Nakuhakikishia huwezi. Watu wa NIT kutoka uko Gongolamboto wanapanga sembuse wewe wa Udsm mbali hivo. Nikupe facts,siku za jumatatu ukitoka Gmboto 07:00 muda wa wastani kufika Mawasiliano ni 08:20, huu ni wastani maana kuna siku utachelewa sana au utawahi chini ya dakika 8 tu hapo. Siku za jumanne mpaka alhamisi utafika 08:08 hivi. Jumamosi mara nyingi gari za kwenda nje ya nchi haziwi nyingi pale Mandela road hivo utawahi kidogo sana. Jumapili kunakuwa na raha kusafili,dakika 50 tu ushafika. Kurudi itakuwa tabu sana utakumbana na foleni pale interchange ya ubungo,ukutane nayo matumbi,uikute kabla ya kuvuka Mfugale uikute Njiapanda Segerea baada ya hapo mkeka mpaka Gmboto. Niishie hapa
 
Unaweza na unawahi kabisa iwatu wanakaa mvuti(mvuti ni mbele kutokay chanika) wanafanya kazi makumbusho mwenge na kila siku wanaenda na kurudi ni mazoea tuu utapanda magari matatu au mawili kma unatokea ulongoni mana utapanda zile daladala zinazotokea mnadani mpk gmboto mwisho then gongo la mboto mpk mawasiliano pale inategemea unaweza panda daladala au ukatembea za kukufikisha chuoni sehemu husika

nauri kwenda na kurudi si chini ya 2800/=

kutoka gmboto mpk mawasiliano asubuhi ni kati ya lisaa limoja mpk matatu kutegemea asubuhi unatoka saa ngapi hvyohvyo kurudi jioni ni masaa hayohayo kutegemea na muda utakaorudi
 
Ili uweze kufaulu katika masomo yako comfortability ni suala la msingi, Gongo la mboto mpaka UDSM ni mbali, itakulazimu uwahi kuamka na utarudi late, sometimes hata saa tano usiku, hii ratiba itakufanya urudi umechoka, na inaweza ikawa tiketi ya kutokumaliza shule, kuliko kujipa kibarua cha kuamka mapema na kurudi late nyumbani, ni bora utafute malazi karibu na Chuo, ili uweze kusoma comfortable, nimeyaandika haya with my own experience on that!
Asante
 
Unaweza na unawahi kabisa isipokuwa watu wanakaa mvuti(mvuti ni baada ya chanika) wanafanya kazi makumbusho mwenge na kila siku wanaenda na kurudi ni mazoea tuu utapanda magari matatu au mawili kma unatokea ulongoni mana utapanda zile daladala zinazotokea mndani mpk gmboto mwisho then gongo la mboto mpk mawasiliano pale inategemea unaweza panda daladala au ukatembea za kukufikisha chuoni sehemu husika

nauri kwenda na kurudi si chini ya 2800/=

kutoka gmboto mpk mawasiliano asubuhi ni kati ya lisaa limoja mpk matatu kutegemea asubuhi unatoka saa ngapi hvyohvyo kurudi jioni ni masaa hayohayo kutegemea na muda utakaorudi
Asante
 
Utafeli mkuu kuwa makini na haya maamuzi yako, chamsingi wewe doja kwanza hostel tafuta jamaa msalimie ongea nae shida yako atakusaidia, isikuoe majukumu mengi ambayo mwisho yatafanya uone shule ngumu na ushindwe kufocus kwenye masomo.
Pia hela ya usafiri utaenda mno kila siku elfu 2 piga hesabu kwa semester utakuwa umetumia kiasi gani
 
Back
Top Bottom