Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
Uamuzi wa madaktari kugoma haukuwa uamuzi rahisi; ni uamuzi ambao umekuja ukiwa na gharama kubwa kwao na kwa taifa vile vile. Lakini uamuzi ambao umekuja kwa sababu umelazimishwa. Sera ambazo zimekuwa zikisimamia sekta ya afya zimeonekana kushindwa na sasa haya ni mavuno yake. Upo mgogoro katika sekta hiyo na licha ya kuongezwa kwa vitu bado inaonekana watawala wameshindwa kabisa kujenga mfumo wa kisasa wa afya.
Hivyo, naamini madai ya madaktari ni hatua ya mwanzo ya kudai huduma bora na mfumo wa kisasa. Siamini kama ni suala la mishahara na maslahi ya madaktari tu; binafsi naamini ni suala linalohusiana na a comprehensive healthcare reform.
a. Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali inaendesha mahospita mengi ambayo haina uwezo wa kuyahudumia - wakati umefika wa kufikiria serikali kuachia hospitali - ibakie na hospitali kama za jeshi n.k Tunaweza vipi kuzitoa hospitali kutoka kwenye mikono ya serikali na kuzileta kwenye sekta binafsi au ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma?
b. Mfumo wa sasa wa centralized policy ya afya kwa taifa zima hata kwa mambo madogo umepitwa na wakati. Ipo haja katika kuangalia mfumo wetu wa afya kufikiria jinsi ya kufanya healthcare kuwa na a local outlook zaidi na hivyo kuwa ni ya sehemu ilipo.
c. Kuboresha maslahi ya watendaji wa sekta ya afya kwa kuweka motisha zaidi, uhuru zaidi na vile vile kuinua elimu. Mojawapo ya matatizo ambayo ni wazi yapo ni jinsi gani madaktari na wauguzi wetu wanakuwa upgraded katika ujuzi na elimu yao.
Ni kwa sababu hizi na nyingine naamini kuunga mkono mgomo wa madaktari ni jambo la kizalendo zaidi kuliko kuendelea kukaa kimya. Wao madaktari wanapodai maslahi zaidi na mafao zaidi wajue kabisa kuwa wananchi nao wanajiandaa kuwadai wao zaidi katika huduma na ubora wa huduma wanazotoa. Hivyo, wasikubali kuachilia kirahisi hadi wawe na uhakika kuwa madai yao ya msingi kabisa yameangaliwa na yanalenga katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Nawaunga mkono madaktari katika mgomo wao!
Msingi wa kuelewa Maadili ya Mgomo wa Madaktari - SOMA KABLA HUJACHUKUA UPANDE!