Nawatafuta ndugu zangu jamani

Nawatafuta ndugu zangu jamani

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
hay;

Marafiki, ndugu na jaama zangu wa hapa mwenzenu nimepotelewa na ndugu, rafiki, na jamaa zangu
tokea mwaka 2013, mpaka sasa sijawapata nimejaribu kuwatafuta katika mitandao mbalimbali, hususani
katika mtandao huitwao chefua kila kona ya mji ambao anauendesha Bujibuji, hukoi nikawakosa ndugu zangu,
Nikaona nijaribu tena kwenye TV ya acha kujipendekeza ambayo inaongozwa na kumilikiwa na Mtambuzi napo
huko nikawakosa kwani walitangaza sana kupitia matangazo yao ya television hawakujitokeza kabisa. Nikaenda
yambe kule kuna Redio inayoitwa NANE BINADAMU ambayo inamilikiwa na watu8, nako nikawa sikuambulia
kitu nikawa nimepoteza nauli kwa safari ndefu namna ile. Nikajiingiza tena kwenye mtandao wa uso kioo nako huko sikupata kitu kwani walinizungusha sana na kunipotezea Muda, Jamani nimetembea na kutembeaga lakini wapi. Isitoshe nikaenda tena kujaribu Mtumaini Bwana hata ukiuziwa na snowhite ambayo inamilikiwa na Arushaone yeye anajiita kuwa hakuna mwingine kule A-Town bila yeye, kwani nilipata nako heeeee! huko ilikuwa balaa kwani wakati naenda nilipanda ndege ya FASTJET kwani hakuna kitu ila ni pesa ilipotea. Na mume wangu Mentor akigundua hili mbona itakuwa balaa home sijui nitasemaje mie mwenzenu.yani sio siri mwenzenu nimezunguka Tanzania bara na visiwani mpaka nimekwenda nchi ya Chimbuvu lakini wapi nikaingia nchi ya Ben Saanane nako wapi. ILiyobaki
nimechoka na nimesema sasa basi siangaiki tena kuwatafuta hawa watajileta wenyewe.

Bandugu naomba msaada wenu kwani nimeaangaika sana sijawapata hawa ndugu zangu , naomba nanyi mkisikia wako mahali fulani iwe cc, mmu, mwongozo haa oops! (rekebisha kauli yako) au popote pale msisite kunitwangia hapa na
kuniambia waliko acha niwaorodheshee majina yao hapa ili iwe rahisi kuwapata nao ni: Passion Lady, sweetlady, charminglady, FirstLady, Lady, na wengine walikuwa wadogo nimewasahau majina yao naomba msijiratibu kwa maneno bali nisaidieni jamani kwani nawapenda.

Mheshimiwa spika Paloma naomba utambulisho na mwongozo
 
Last edited by a moderator:
nashukuru nimekupata maana nimekutafuta kwa muda mrefu sijakutia machoni pangu yaliyonipata ndugu yangu wewe acha tu kwani uko nilikuokokua ni jehanamu ya dunia watu wana hasira utadhani wamemwagiwa na tindikali nimekandamizwa ile mbaya bahati ndugu yangu uko utaokoa jahazi
Nipo cousin... sema!
 
Back
Top Bottom