Nawashukuru sana wana jf kwa........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawashukuru sana wana jf kwa........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nnunu, Aug 30, 2011.

1. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#1
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
Habari wana JF wote,
Naomba nitoe shukurani nyingi sana kwa wanajf wote walionipa ushauri kuhusiana na thread yangu niliyoanzisha hapa kuomba ushauri wa nn cha kufanya baada ya kupata dv 4 ya point 18(form 6). Nilikata tamaa sana, nilivunjika moyo kwa kiasi kikubwa sana, lakin NAWASHUKURU SANA KWA USHAURI WENU MLIONIPA,ULINIINUA,ULINAPA MWANGA MPANA SANA, NILIUFANYIA KAZI (baadhi...lol siyo ushauri wote). Sept naanza chuo rasmi kusomea diploma.
Kila jambo jema liwe sehemu ya pumzi yenu, MUNGU AZIDI KUWABARIKI ,AWAZIDISHIE UPENDO,HEKIMA NA BUSARA ZAIDI. NAWAPENDA ZAIDI, ASANTENI SANA.

2. Bishanga

Bishanga JF-Expert Member

#2
Aug 30, 2011
Joined: Jun 29, 2008
Messages: 15,347
Likes Received: 47
Trophy Points: 0
Hongera Nnunu,kujikwaa sio kuanguka,kwa kuwa umeona nuru baada ya giza totoro ifuate nuru hiyo ikupeleke katika mafanikio.Soma signature ya mdau wa MMU anayeitwa Mr. Rocky,mimi kwa kompyuta ni maimuna vinginevyo ningikopi na kuitumbukiza hapa.

3. Mtalingolo

Mtalingolo JF-Expert Member

#3
Aug 30, 2011
Joined: Aug 4, 2011
Messages: 2,188
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
Hongera vp umepata chuo gani? Na unaenda kusoma dip ya kitu gani? Blessing be wit you.

4. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#4
Aug 30, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Mkuu Mungu akusaidie na uweze kufanikiwa kaktika safari yako ya masomo
Na maisha pia Mungu akutangulie

5. Mtalingolo

Mtalingolo JF-Expert Member

#5
Aug 30, 2011
Joined: Aug 4, 2011
Messages: 2,188
Likes Received: 16
Trophy Points: 135

si vibaya kumjibia Ameni....

6. Desidii

Desidii JF-Expert Member

#6
Aug 30, 2011
Joined: Oct 2, 2007
Messages: 1,212
Likes Received: 5
Trophy Points: 135
Barikiwa sana na huo ni ushujaa unaotakiwa.

7. The Finest

The Finest JF-Expert Member

#7
Aug 30, 2011
Joined: Jul 14, 2010
Messages: 21,709
Likes Received: 43
Trophy Points: 145
Likitokea jambo lolote lile ni lazima maisha yasonge mbele badala kuanza kujilaumu, nakupongeza kwa kupata chuo ongeza juhudina kumuomba Mungu kwenye masomo yako utafanikiwa tu.

8. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#8
Aug 30, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Na umeonyesha moyo sana hata kurudi kuja kutoa shukrani maana wengi huwa wanaishia huko huko hawakumbuki kama walipata ushauri hapa

9. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#9
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

Nisingeweza kufanya ksb hali niliyokuwa kipindi hicho matokea kilikuwa kibaya sana, lakin ushauri wana Jf ndiyo uliyoniondolea na kunifuta machozi na huzuni yangu moyoni. Sitawasahau ktk safari yangu ya elimu, na naahidi hata nitakapomaliza hiyo diploma yangu sitasahau kuleta matokea yangu hapa.
Kila ninaposafiri sijawahi wala sikumbuki kama nimewahi kusahau sehemu ya kivuli nilichopumzikia wakati wa safari yangu. Wana jf ni sehemu ya kivuli changu pasipo nyie safari isingefika hapa nilipo leo na hata nitakapokuwa siku zijazo. ASANTENI SANA.

10. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#10
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
<br /
ASANTE SANA ,na WEPESI WA TATIZO UONEKANA PINDI UNAPOPATA WATU WA KUKUPA MOYO WA KUSONGA MBELE.
NAAHIDI KUSOMA KWA BIDII SANA, ILI NIWEZE KUTIMIZA NDOTO ZANGU.

11. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#11
Aug 30, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Mungu akutangulie katika kila ulilopanga kufanya na ubarikiwe sana sana

12. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#12
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

Asante sana kwa kuitambua shukurani yangu.

13. A

Ave Ave Maria JF-Expert Member

#13
Aug 30, 2011
Joined: Apr 22, 2011
Messages: 10,757
Likes Received: 34
Trophy Points: 0
Hongera mpenzi, safari ndo imeanza tena. Jitahidi usiwe mzembe ili ufanikishe malengo yako. Mwenyezi Mungu akutangulie!

14. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#14
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

Shukurani Bishanga, nuru niliyoiona imetoka kwenu ndugu na rafiki zangu wanajf. Nyie ndiyo mlionitoa kwenye ilo giza totoro ASANTENI SANA. Kuhusu signature ya Mr Rocky bahati mbaya siioni ksb natumia kasim hakaoneshi. Ila itabidi nitafute njia ya kuisoma hiyo signature.

15. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#15
Aug 30, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Problems are simply part of the curriculum that appear and fade away like algebra class but the lessons you learn will last a lifetime.

Signature yangu hiyo hapo mkuu isome

16. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#16
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

ASANTE SANA KWA MAOMBI YAKO YA BARAKA,NAAMINI MUNGU AMEFANYA.

17. The Finest

The Finest JF-Expert Member

#17
Aug 30, 2011
Joined: Jul 14, 2010
Messages: 21,709
Likes Received: 43
Trophy Points: 145
Ubarikiwe na Mungu akutangulie kwenye kila jambo

18. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#18
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

Nakuunga mkono % zote, Nimeisoma, asante kwa kunirahisishia kuipata.

19. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#19
Aug 30, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
karibu mkuu
ubarikiwe sana

20. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#20
Aug 30, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

ASANTE SANA Kapipi, ntahakikisha siwi mzembe ili nitekeleze kile kilichonipeleka huko. Nashukuru kwa kunipa moyo zaidi.

Loading...